Mapadri 3000 wagundulika kuwadhalilisha watoto kingono tangu 1950, Ufaransa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
Takriban watu 3000 wanaowadhalilisha watoto kingono wamekuwa wakiendesha maovu yao ndani ya kanisa katoliki nchini Ufaransa tangu mwaka 1950, hii ikiwa ni kwa mujibu wa mkuu wa tume huru inayochunguza kashfa hiyo, aliyezungumza na shirika la habari la AFP siku kadhaa kabla ya ripoti ya uchunguzi kutolewa rasmi.

Jean-Marc Sauve amesema uchunguzi wao umewagundua wadhalilishaji watoto kingono kati ya 2900 na 3200 wanaodaiwa kuwa mapadri na waumini wengine wa kanisa hilo.

Sauve amesema ripoti yao iliyo na kurasa 2,500 itatolewa siku ya Jumanne baada ya miaka miwili na nusu ya uchunguzi uliojikita makanisani, mahakamani, ukusanyaji wa nyaraka za polisi pamoja na mahojiano waliofanyiwa walioshuhudia kashfa hizo.

Tume hiyo ilianzishwa mwaka 2018 na Baraza la maaskofu la Ufaransa CEF na Mkutano Mkuu wa maaskofu wa Ufaransa CORREF kutokana na idadi ya kashfa za udhalilishaji wa kingono zilizoitikisa kanisa katoliki nchini Ufaransa na ulimwengu kwa ujumla.
 
Tuwapongeze wafaransa kwa kuanika huo uchafu
sehemu nyingi duniani ayo mambo ni marufuku kuzungumzwa hadharani japo yanafahamika
 
Takriban watu 3000 wanaowadhalilisha watoto kingono wamekuwa wakiendesha maovu yao ndani ya kanisa katoliki nchini Ufaransa tangu mwaka 1950, hii ikiwa ni kwa mujibu wa mkuu wa tume huru inayochunguza kashfa hiyo, aliyezungumza na shirika la habari la AFP siku kadhaa kabla ya ripoti ya uchunguzi kutolewa rasmi.

Jean-Marc Sauve amesema uchunguzi wao umewagundua wadhalilishaji watoto kingono kati ya 2900 na 3200 wanaodaiwa kuwa mapadri na waumini wengine wa kanisa hilo.

Sauve amesema ripoti yao iliyo na kurasa 2,500 itatolewa siku ya Jumanne baada ya miaka miwili na nusu ya uchunguzi uliojikita makanisani, mahakamani, ukusanyaji wa nyaraka za polisi pamoja na mahojiano waliofanyiwa walioshuhudia kashfa hizo.

Tume hiyo ilianzishwa mwaka 2018 na Baraza la maaskofu la Ufaransa CEF na Mkutano Mkuu wa maaskofu wa Ufaransa CORREF kutokana na idadi ya kashfa za udhalilishaji wa kingono zilizoitikisa kanisa katoliki nchini Ufaransa na ulimwengu kwa ujumla.
Ingewezekana wangeruhusiwa kuoa labda ingepunguza haya matatizo.
 
Mapadri na maaskofu katoliki kwa kunajisi vijana ni sawa na samaki na maji.

Siku kukiwa na uchunguzi wa wazi huku Afrika watu wanaweza kulia. Vijana wengi wanaohudumu kwenye madhabahu wananajisiwa sio kidogo.
Funga mdomo, acha kuongea maujinga yako
 
Mapadri na maaskofu katoliki kwa kunajisi vijana ni sawa na samaki na maji.

Siku kukiwa na uchunguzi wa wazi huku Afrika watu wanaweza kulia. Vijana wengi wanaohudumu kwenye madhabahu wananajisiwa sio kidogo.
Waache wale kondoo wao
 
Back
Top Bottom