Chademakwanza
JF-Expert Member
- Jun 11, 2014
- 6,346
- 1,873
BAVICHA Mkoa wa Mbeya,mnamo tarehe 12/5/2015 tulipokea taarifa za uwepo wa zoezi la kuandikisha wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kutumia fomu yenye kichwa cha habari "FOMU YA MAOMBI YA UTAMBULISHO/MPIGA KURA fomu hizo zina usajili wa Ref:Fomu ya usajili Name.1A.
Baada ya kufuatilia kwa umakini tumegundua utata ufuatao.
1 Zoezi linafanyika kwa kificho pasipo taarifa rasimi kwa jamii ya chuo kikuu na hata baadhi yao walipo uliza maswali maswali kwa wahusika hakuna majibu sahihi yaliyo tolewa.
2 Fomu husika hazina nembo maalumu ya utambulisho rasimi wa mamlaka gani ya serikali inaendesha zoezi husika isipokuwa kuna nembo ya serikali tu.
3 Wanafunzi wote wanaojaza fomu husika wamelazimishwa (ref.TEKU) ,Kupitia kipengele namba 37 cha fomu husika kujaza kama wakazi wa Mtaa wa Block T hata kama si wakazi /ama hawaishi eneo hilo.
4 Kupitia kipengere namba 59 hawapaswi kujaza ikiwa ni Wanataka kujiandikisha kuwa wapiga kura sawa sawa na mahitaji ya kifungu hicho.
5 Fomu hizi hazifanani na fomu zilozo tumika katika zoezi za NIDA Dar es salaam na Zanzibar,taarifa zinaonesha zile za DSM zlikuwa na kichwa cha FOMU YA KITAMBULISHO CHA TAIFA , tofauti na hii yenye nyongeza ya neno MPIGA KURA.
Tunaomba mamlaka nyingine za Chama kufanyia kazi taarifa hizi hususani wakati huu wa Daftari la kudumu la wapiga kura.
Gwamaka Mbughi (Katibu BAVICHA MKOA WA MBEYA)