SoC02 Uwepo wa bidhaa bandia na halisi sokoni: Upi wajibu wa mlaji kabla ya kununua na kutumia bidhaa?

Stories of Change - 2022 Competition

Jerry Farms

Member
Jul 18, 2022
30
29
Kumekuwepo na mitazamo tofauti tofauti juu ya bidhaa zinazoingizwa sokoni kwa matumizi. Asilimia kubwa ya walaji wa bidhaa wamekua na kauli za; "bidhaa hizi za XYZ ( anataja jina la nchi) siwezi kununua kwani ni bandia...", mwingine yeye atarejea historia kwa kusema, " hii gari ni ya Mjerumani! Ni imara kweli kweli...!". Je kauli hizi mbili zina ukweli kiasi gani? Hemu tutazame dhana ya_ Matumizi ya bidhaa toka sokoni pasipo kusoma maelekezo ambatanishwa katika bidhaa.

Kufuatia tabia ya kutojali iliyojengeka miongoni mwa watu wengi, bidhaa sokoni zimekua zikitumika chini ya kiwango, ama juu( zaidi ya lengo pangwa) ama kwa *usahihi. Hali hii imepelekea malalamiko ya walaji kwa mamlaka za udhibiti wa bidhaa, wazalishaji na mwisho kwa muuzaji wa bidhaa. Je kuna uzembe mahali ama uholela wa bidhaa katika soko? Jibu ni hapana, Swali linakuja je tunafahamu matumizi sahihi ya bidhaa tuliyonayo?Matumizi ya bidhaa pasipo kuisoma vyema ni moja wapo ya sababu tosha ya malalamiko haya ya walaji.


FAIDA ZA KUTUMIA BIDHAA BAADA YA KUPITIA MAELEKEZO AMBATANISHWA.

Kusoma maelekezo ya bidhaa kuna faida kede kede kwa mlaji, miongoni mwa faida hizo ni pamoja na:


Kujua matumizi sahihi ya bidhaa

Kwa kusoma maelekezo ya matumizi ya bidha, bidhaa iliyonunuliwa toka sokoni itatumika katika viwango stahiki hivyo kuleta matokeo chanya.


Kuepusha athari za kiafya kutokana na matumizi yasiyosahihi ya bidhaa.

Kwa kurejea Ripoti ya Matumizi ya Antibiyotiki 2015( The State of the World's Antibiotic 2015), kumeonekana uongezekaji wa usugu wa magojwa kufuatia matumizi yasiyosahihi ya dawa. Moja ya sababu ni uzingatifu hafifu wa maelekezo ambatanishwa katika dawa! Kwa mwaka 2013 nchini Tanzania vifo vya watoto vilifikia 15% kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya dawa vivyo hivyo watu wazima 35000 walifariki kwa homa ya mapafu itokanayo na backteria sugu wa Streptococcus pneumonia. Athari hazijaishia hapo tu kuna walaji wengine wamekua walemavu kutokana na kutozingatia na kupitia maelekezo kabla ya matumizi ya bidhaa.
Je ndugu msomaji unakifahamu kwa undani kinywaji upendacho kunywa kila siku? Umewahi kujipa wasaa wa japo dakika mbili kusoma kilichoandikwa nyuma ya chupa ya kinywaji/ chakula ulichonunua dukani?


Kupunguza gharama zinazoweza kuepukika

Gharama nyingi zinaweza kuepukika iwapo tu mlaji atatumia muda wake kusoma na kufata maelekezo katika bidhaa. Mfano, katika maisha ya kila siku jiulize je bidhaa kama Sabuni nayotumia ninazingatia matumizi yake? Sabuni inakutaka uloweke nguo kwa dakika XXX...je unazingatia ama unatumia sabuni ya unga na ya kipande sambamba huku ukilalama?, Nguo inakutaka usiiloweke, uifue na kuianika kivulini! Je unazingatia? Ikichakaa mapema utalaumu kampuni na muuzaji wa nguo!!! Kuepuka haya basi hatuna budi kuzingatia maelezo kabla ya kutumia.

Vile vile kwa kusoma na kuzingatia maelekezo kabla ya kutumia bidhaa ajali mbali mbali zinaweza kuepukika, mfano matumizi ya gesi majumbani pasipo kua na uelewa wa gesi!


Utunzaji wa mazingira kufuatia utumiaji na uhifadhi sahihi wa mabaki ya bidhaa.

Mazingira yetu yanahitaji kutunzwa ili kuwa na faida kwetu na kizazi kijacho, haya yoote yataweza kufikiwa iwapo tu tutazingatia maelekezo ya jinsi ya kutumia na kutupa mabaki ya bidhaa. Mfano rahisi, Je ni wangapi tumewahi soma juu ya chupa za vinywaji nini yatupasa kufanya baada ya kunywa au hua tunatupa ovyo ovyo na kuchafua mazingira?


Kupunguza malalamiko ya walaji kwenda kwa wasimathibiti ubora,wazalishaji na wauzaji wa bidhaa.

Pindi mlaji atakapo soma maelezo ya bidhaa na kuzingatia kwa usahihi atapata matokeo chanya juu ya bidhaa hivyo kutokuwa na lawama kwa watajwa hapo juu.


CHANGAMOTO

 Elimu


Baadhi ya walaji hawajui kusoma na wana aibu kuuliza juu ya matumizi sahihi ya bidhaa hivyo huenda kutumia bidhaa isivyopaswa na kupata matokeo hasi.


Lugha isiyorafiki ya maelekezo katika bidhaa

Baadhi ya bidhaa aghalabu bidhaa zinazoagizwa toka nnje zimekua na maelekezo yenye lugha inayoleta mkanganyiko kwa mlaji hivyo matumizi yasiyo sahihi ya bidhaa. Mfano mafuta ya nywele yaliyoandikwa kiingereza/kiarabu yatampa wasaa mgumu mtumiaji asiyejua lugha tajwa hivyo kujikuta anapaka mwilini! Asalaleee, akipatwa na changamoto mtumiaji huyu lawama zitarudi kwa muuzaji na serikali kwa ujumla!


Mazoea ya matumizi ya bidhaa bila kujali.

Hili linachagizwa na kauli maarufu zilizopo mitaani, mfano wa kauli hizi ni;".....atanikifata maelekezo kufa kupo tu...", " we nipe hio bidhaa kwani kudhulika unadhulika wewe au mimi..", " hela yangu unipangie matumizi!", mtu huyu ndio utakuta kaambiwa kinywaji hiki usinywe zaidi ya chupa 3 yeye anatwanga sita! Je akidhurika ilaumiwe kampuni au muuzaji?


HITIMISHO



ELIMU

Elimu zaidi inatakiwa itolewe kwa wananchi juu ya umuhimu wa kusoma na kuzingatia maelekezo juu ya bidhaa iliyopo sokoni. Kampeni zifanyike katika vyombo vya upashanaji habari ( redio, runinga nakadhalika).


JUHUDI ZAIDI ZA UDHIBITI WA BIDHAA SOKONI

Taasisi zinazojihusisha na udhibiti wa uingizwaji, uuzaji na utumiaji wa bidhaa ziweke mkazo katika matumizi ya lugha ya kiswahili katika vifungashio vya bidhaa( lugha inayofahamika na kundi kubwa la walaji). Hapa lugha zaidi ya moja inaweza kutumika katika kutoa maelekezo ya matumizi ya bidhaa.


KUBORESHA NA KUVUMBUA MIFUMO SAIDIZI KWA WALAJI

Kufuatia maendeleo ya teknolojia ya upashanaji habari, wataalamu waje na ubunifu wa programu za mifumo ya simu zitakazo toa usaidizi kwa mlaji pindi anapokwama akiwa sokoni. Programu hizi si tu zitakua za msaada kwa mlaji bali zitasaidia katika udhibiti wa ubora wa bidhaa sokoni.


MABADILIKO BINAFSI YA MLAJI

Shime kwako msomaji kubadili tabia na kujenga zoea la kusoma maelekezo ya bidhaa kabla hujafanya maamuzi ya kununua toka sokoni na kuitumia.
 
Hongera kwa kutukumbusha wajibu wetu walaji, ni andiko lenye tija nakupa kura yangu.
Hata hivyo naomba maoni kwenye chapisho langu
SoC 2022 - Watu maarufu na bidhaa za wanyonge lililopo mtandaoni na ikikupendeza naomba kura yako.

Asante.
 
Hongera kwa kutukumbusha wajibu wetu walaji, ni andiko lenye tija nakupa kura yangu.
Hata hivyo naomba maoni kwenye chapisho langu
SoC 2022 - Watu maarufu na bidhaa za wanyonge lililopo mtandaoni na ikikupendeza naomba kura yako.

Asante.
 
Back
Top Bottom