SoC02 Jenga tamaduni ya kusoma maelezo ya bidhaa kabla ya kuitumia

Stories of Change - 2022 Competition

Jerry Farms

Member
Jul 18, 2022
30
29

BIDHAA BANDIA NA HALISI KATIKA SOKO HURIA: Wajibu wa mlaji kabla ya kununua, kutumia na kuharibu mabaki ya bidhaa.


Katika zama hizi za soko huria kauli hizi si nadra sana kusikika miongoni mwa wanunuzi katika masoko yetu huko tuishiko; kauli kama, "Hii ni ya kichina hivyo sidhani kama itanifaa...." na kauli ya "Bora hata zamani bidhaa zilikua ni bora na zinadumu..."

Je umewahi kujiuliza ni nini kinaweza kuwa chanzo cha yote haya? Je, ni kweli kumekuwa na uholela kiasi hicho wa uingizaji wa bidhaa sokoni au ni sintofahamu yetu juu ya matumizi ya bidhaa? Maswali haya yanaweza kuwa na majibu mengi tu kulingana na utashi wa mlaji lakini leo hebu tujikite katika dhana ya _ununuaji na utumiaji wa bidhaa sokoni pasipo kusoma maelekezo ya bidhaa husika.
Kufuatia uhuria uliopo katika soko la dunia na Tanzania ikiwa ni moja ya soko hilo, kumezuka tabia ya mlaji kulalama juu ya ubora wa bidhaa _lawama zinaelekezwa kwa watengenezaji, wauzaji na wasimamizi wa ubora wa bidhaa zinazoingizwa sokoni. Haya yoote yana chagizwa na kasumba yetu mbaya sisi walaji wa ama kwa kujua ama kutojua kutumia bidhaa pasi na kuisoma na kuielewa kwa upana hivyo kujikuta ama tunatumia bidhaa katika kiwango cha chini, juu ama wastani wa malengo ya mtengenezaji kwa mtumiaji.

FAIDA ZA KUSOMA MAELEZO AMBATANISHWA KATIKA BIDHAA
1-Kujua matumizi sahihi ya bidhaa nunuliwa toka sokoni.

2-Kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza kufuatia matumizi yasiyo sahihi ya bidhaa. Mfano siku hizi za karibuni kumekua na wimbi la ajali nyingi za mioto ya gesi majumbani(wahanga mara nyingi wakihojiwa hudai kua hawakua na taarifa sahihi za matumizi ya gesi),walinunua gesi na kuanza kutumia pasipo kujipa wasaa wa kujifunza matumizi sahihi ya gesi.

-Kuokoa gharama za kifedha na muda, mfano rahisi tu ni matumizi ya sabuni ya unga, je unajua ni muda gani unatakiwa uloweke nguo yako kabla ya kuitumia? ama na wewe ni mmojawapo wa wale tunaochanganya sabuni ya unga na kipande!!!! Nguo inamaelezo kua usiiloweke wewe unaloweka,usianike juani ama usipige pasi vyoote unakiuka, je tuendelee kulalamikia kampuni za nguo juu ya uchakavu wa mavazi? Jibu ni hapana...elimu sahihi na matumizi sahihi ndio suluhisho.

3-Kutunza afya ya mlaji
Kulingana na Ripoti ya matumizi ya Antibiotiki ya 2015( The state of the World's Antibiotic 2015) taarifa zinaonesha kumekua na ongezeko la usugu wa dawa hasa hasa kwa nchi maskini na zinazochipukia kiuchumi moja wapo ya sababu ya hili imechagizwa na ufinyu wa elimu ya matumizi ya dawa na kutozingatia maelezo ya matumizi ya dawa husika. Katika mwaka 2013 vifo vya watoto asilimia 15 vilitokana na usugu wa bacteria wa homa ya mapafu, watu 35000 walifariki kwa homa ya mafua sugu(Streptocus pneumonia) nchini Tanzania,( Ripoti ya matumizi ya Antibiotiki 2015). Swali rahisi tu ujiulize ndugu msomaji...Je hivi vinywaji vya kuongeza nguvu("energy drinks") navyotumia nimesoma maelezo yake? Nini mustakabali wa afya yangu kwa hiki nachokunywa/kula? na mengine mengi.

4-Bidhaa, taka na utunzaji wa mazingira
Kwa kuzingatia maelezo juu ya uhifadhi na uharibuji wa mabaki ya bidhaa baada ya matumizi mazingira yatatuzwa hivyo kua ya faida kwa kizazi cha sasa na kijacho. Maelezo yoote yanapatikana katika bidhaa, lakini je tunajali?

5-Kuongeza ufanisi wa utendaji wa bidhaa aliyonayo mlaji.
Chukulia mfano rahisi wa matumizi ya sabuni ya unga ya kampuni XYZ inamtaka mfuaji uloweke nguo yake kwa muda XX akifuata masharti hayo ufanisi utaonekana lakini pasipo kusoma maelekezo ya matumizi ya sabuni hii mtumiaji atamlalamikia ama muuzaji wa sabuni ama mtengenezaji! Hivyo atanunua sabuni ZKY na kuanza kufua akiwa na kinyongo juu! Alhali tatizo liko kwa mlaji!

6-Kupunguza malalamiko ya mlaji kwa serikali( mamlaka za uthibiti ubora wa bidhaa zinazoingizwa is sokoni TBS/TFDA) na mzalishaji. Kwa kujielimisha juu ya bidhaa mitazamo hasi ya watumiaji kwenda kwa watajwa yatapungua.

CHANGAMOTO KUFIKIA MATARAJIO TAJWA HAPO JUU
1-Uwepo wa walaji wasiojua kusoma na wenye aibu kuuliza kwa mtoa bidhaa juu ya matumizi sahihi.

2-Bidhaa za nnje kua na maelezo yenye lugha isiyo rafiki kwa mlaji mfano bidhaa imeandikwa kichina, kiarabu ama kiingereza alhali mtumiaji ni mswahili toka kijijini ndani ndani.

3-Mazoea na kutozingatia matumizi ya bidhaa.

HITIMISHO
Faida za ufahamu wa matumizi sahihi ya bidhaa ni nyingi kuliko hasara hivyo yafuatayo yazingatiwe na serikali na mlaji wa bidhaa:

Elimu itolewe kwa wengi ili kufuta tamaduni mbaya ya kutojali juu ya kusoma maelezo ya matumizi sahihi ya bidhaa.

Taasisi zinazojishughulisha na uthibiti wa ubora wa bidhaa na matumizi yake zisisitize katika matumizi ya vifungashio vyenye lugha agharabu tatu katika bidhaa moja ili kutatua tatizo la kutoeleweka kwa maelezo ya matumizi ya bidhaa.

Kuundwe mfumo rafiki wa kidigitali utakaokua unatafsili lugha iliyotumika katika bidhaa pindi mlaji anapotatizika, mfumo huu uweze kua katika simu za kawaida na simu janja.

Mabadiliko binafsi ya mtumiaji wa bidhaa bila kusubiri shurti toka sehemu nyingine. Waswahili wanausemi, "Asiyeskia la mkuu, huvunjika guu"!. hivyo shime kwako msomaji kubadili tabia na kufurahia bidhaa zilizopo sokoni.
 
Wengi ni wavivu kusoma, sometimes hata haya mnayoandika we just look main points tu, sijui nani katuletea huu uvivu wa kusoma.

All the best.

Shida ni kupiga kura, ni kama hicho kitufe kinaleta vitu sivielewi, saidieni hapo
 
Wengi ni wavivu kusoma, sometimes hata haya mnayoandika we just look main points tu, sijui nani katuletea huu uvivu wa kusoma.

All the best.

Shida ni kupiga kura, ni kama hicho kitufe kinaleta vitu sivielewi, saidieni hapo
Uvivu n mbaya saana! Tena likija suala la kusoma kwetu watanzania tuliowengi hua tuwavivu.
 
Wengi ni wavivu kusoma, sometimes hata haya mnayoandika we just look main points tu, sijui nani katuletea huu uvivu wa kusoma.

All the best.

Shida ni kupiga kura, ni kama hicho kitufe kinaleta vitu sivielewi, saidieni hapo
Unaclick tu kinacount vote
 
Back
Top Bottom