Uwekezaji wa Uingereza nchini Tanzania

Uwekezaji wa Uingereza nchini Tanzania

HII THREAD NZURI SANA ILA WATACHANGIA WATU WENYE UPEO NA UELEWA WA NCHI YETU TUNAISAIDIAJE KATIKA KUPIGA HATUA
 
NGOs sijui kama huwa zina mchango kimaendeleo maana nyingi zinaajiri vijana wazungukezunguke eti wanafanya utafiti ili wawapotezee muda wa kufikiria kuunda viwanda/mashine/applications na kutoa matokeo yanayohamasisha mletewe msaada, na msaada utakuta una masharti fulani.
Mkuu una uhakika na ulicho kiandika?
Wana NGO yao moja inaitwa Equip T, acha kabisa wametumwa pikipiki kwa kila mratibu elimu kata, bado I pads kwa kila mwl mkuu mek, nk.
Hawa jamaa kwenye NGO zao huwa zinafanya vizuri Sana kimaendeleo.
Sema tu huwa wnakatishwa tamaa na hawa viongozi watu, serikalini.
 
Mkuu naomba univumilie na tutafakari kwa pamoja bila ugomvi. Ukiangalia kwenye hayo mazingira kipaumbele ni pikipiki na I-pads? Mimi narudi kulekule tu kwamba wanataka vijana wapoteze muda kwa kuweka mafuta kwenye pikipiki wazulule na watumie I-pad kupoteza muda kujifunza namna ya kuzitumia, wahangaike kununua vifurushi n.k Napendekeza kuwanunulia trekta la kijiji, kujenga mifumo ya umwagiliaji, kujenga maghala ya kuhifadhi nafaka, kujenga vyoo bora vya wanafunzi, kukarabati madarasa/madawati nk. Hizo bidhaa ulizotaja hazinufaishi umma moja kwa moja ila wananufaika watu binafsi halafu umma baadae.
 
wafanye yote hayo,nyie wenyewe mnafanya nin'g
 
tumejipanga sana,MO,gsm,barhesa wamedhamilia kuporomosha maviwanda ya kila aina ndani ya miaka 3,
kwa kanda ya ziwa yupo JAMBO nae anakuja juu kwa speed ya nyati aliejeruhiwa
Dah ila spidi anayokuja nayo JAMBO ni balaa
 
Hivi kweli China ni wawekezaji au ni wachafuzi wa mazingira tu? Mie nadhani serikali haijaisimamia vilivyo mwekezaji anayejiita mchina
 
ni bora tukareview vizuri hiyo mikataba mara nyingi sana waingereza wako fair ukilinganisha na mataifa yaliyobaki kwenye European Eunion . na mtoa uzi nimuulize wachina ni lini waliwapiku uingereza uwekezaji Tanzania?

Kama kumbukumbu zangu zipo sahihi, nilisoma article moja labda miaka 2 hivi imepita. Naweza kuwa nimechanganya na report ya Afrika nzima. Nadhani tutegemee miaka michache ijayo kuona Ujerumani na wenyewe wakiongeza mahusiano yao na Tanzania.
 
NGOs sijui kama huwa zina mchango kimaendeleo maana nyingi zinaajiri vijana wazungukezunguke eti wanafanya utafiti ili wawapotezee muda wa kufikiria kuunda viwanda/mashine/applications na kutoa matokeo yanayohamasisha mletewe msaada, na msaada utakuta una masharti fulani.

Una maana utafiti hauna faida? Si afadhali hao wanaozunguka zunguka lakini wanalipa kodi kubwa kuliko wanaoshinda vijiweni kwa kukosa ajira?
 
Financial Markets ie bonds, stocks, euro bonds etc.
 
Asanteni kwa kunipa mwangaza, hii kitu nimekuwa najiuliza kwa muda mrefu sana. Kwa hiyo kiufupi, uhusiano wetu na Uingereza upo vizuri sana. Kwenye sekta ya elimu vipi, hawajawekeza na huko hasa katika vyuo?
 
Hivi kweli China ni wawekezaji au ni wachafuzi wa mazingira tu? Mie nadhani serikali haijaisimamia vilivyo mwekezaji anayejiita mchina

Nadhani na wachina wanahitaji tuwajadili. Takwimu zinaonyesha wamefungua maelfu ya makampuni hapa TZ. Sitashangaa kukuta zingine zinatuka tu kwa shughuli haramu.
 
Mkuu naomba univumilie na tutafakari kwa pamoja bila ugomvi. Ukiangalia kwenye hayo mazingira kipaumbele ni pikipiki na I-pads? Mimi narudi kulekule tu kwamba wanataka vijana wapoteze muda kwa kuweka mafuta kwenye pikipiki wazulule na watumie I-pad kupoteza muda kujifunza namna ya kuzitumia, wahangaike kununua vifurushi n.k Napendekeza kuwanunulia trekta la kijiji, kujenga mifumo ya umwagiliaji, kujenga maghala ya kuhifadhi nafaka, kujenga vyoo bora vya wanafunzi, kukarabati madarasa/madawati nk. Hizo bidhaa ulizotaja hazinufaishi umma moja kwa moja ila wananufaika watu binafsi halafu umma baadae.

Mkuu mimi nafikiri ungeuliza NGO ya Equip T ilianzishwa kwa madhumini/lengo gani? Hilo la kwanza, la pili: Usafiri na mawasiliona ni vitu muhimu katika kufanikisha uratibu wa Elimu, kumbuka Elimu ina umuhimu wa kipekee Duniani hakuna Taifa linalo puuzia Elimu kama linajitambua vizuri, kitu kingine Waingereza ni binadamu makini sana hawafanyi vitu kwa kukurupuka, kila kitu wanacho kubali kutoa msaada wanakifanyia utafiti wa kina kwanza na kujiridhisha kwamba kina mantiki. Binafsi nawapongeza sana kuanzisha NGO ya Equip T.
 
Kwa muda mrefu, Uingereza ndiyo walikuwa kinara wa uwekezaji kutoka nje nchini Tanzania. Inaonyesha wapo low key sana kwenye uwekezaji wao hauna makeke kama wa waChina na Marekani, kwa muda mrefu nimekuwa najiuliza uwekezaji wao upo katika sekta gani. Ilichukua muda mrefu mpaka China kuweza kuwapiku miaka michache iliyopita.

Natambua uwepo kwa mabenki ya Barclays na Standard Chartered ambao nao hawana hata muda mrefu Tanzania (huku nikisikia Barclays wapo kwenye mikakati ya kuondoka Afrika). Ningeomba mwongozo ni sekta zipi ambazo Uingereza wamewekeza Tanzania na ikiwezekana makampuni yanayohusika yatajwe.
Kaka hawa wenyewe kwao wameuza makampuni yote. Jina lao ni kubwa lakini uchumi wao unaendeshwa na wageni asilimia kubwa hivyo si ajabu ukaona wapo kimya. wanataka kubinafsisha hata huduma za afya sema tu kelele za baadhi ya wabunge na manung'uniko ya wananchi yamewafanya wasitishe. Ila zaidi soma hii taarifa hapa

UK Companies Investing in Tanzania Provide Positive Feedback - TanzaniaInvest
 
Wachina ndo wanatuharibia hi nchi..ila waingereza wamefanya vitu vingi kwenye nchi hi na wanaendelea kupitia miradi yao ya kibenki,NGO's,viwanda na migodi sema muda mwingine wanakwamishwa na viongozi wenye maslahi binafsi
 
tumejipanga sana,MO,gsm,barhesa wamedhamilia kuporomosha maviwanda ya kila aina ndani ya miaka 3,
kwa kanda ya ziwa yupo JAMBO nae anakuja juu kwa speed ya nyati aliejeruhiwa
Hawa ndo serikali ilipaswa ikae nao chini kwanza wapange pamoja ili akija mwekezaji awe na shea ya nusu kwa nusu na hawa jamaa, kama hawana mitaji serikali ni jukumu lake kuwa wekea dhamana kwenye mabenki ya nje ili wapewe mikopo. Like reli ya kati wale wachina wangekuwa na ubia na Mo au barhesa wa nusu kwa nusu ingekuwa poa sana
 
Mkuu naomba univumilie na tutafakari kwa pamoja bila ugomvi. Ukiangalia kwenye hayo mazingira kipaumbele ni pikipiki na I-pads? Mimi narudi kulekule tu kwamba wanataka vijana wapoteze muda kwa kuweka mafuta kwenye pikipiki wazulule na watumie I-pad kupoteza muda kujifunza namna ya kuzitumia, wahangaike kununua vifurushi n.k Napendekeza kuwanunulia trekta la kijiji, kujenga mifumo ya umwagiliaji, kujenga maghala ya kuhifadhi nafaka, kujenga vyoo bora vya wanafunzi, kukarabati madarasa/madawati nk. Hizo bidhaa ulizotaja hazinufaishi umma moja kwa moja ila wananufaika watu binafsi halafu umma baadae.
Mkuu ungekuwa unafanya au una interest kwenye sector ya elimu ungejua umuhimu wa hivyo Vifaa tajwa hapo juu.
Waratibu walikuwa hawatembelei shule, na kama ujuavyo idara ya ukaguzi ipo ipo tu siku hizi.
Hizi pikipiki zinawaraisishia kazi kuzunguka kila shule kwenye kata yake.
Pia zile I pads wameziprogram sio za face book na whatsaap, zile ni kwa ajili ya data kutoka kwa mwalimu mkuu to mratibu, Deo, Reo, mwisho tamisemi.
So hakuna kitu cha Anasa hapo hata kidogo.
 
Kaka hawa wenyewe kwao wameuza makampuni yote. Jina lao ni kubwa lakini uchumi wao unaendeshwa na wageni asilimia kubwa hivyo si ajabu ukaona wapo kimya. wanataka kubinafsisha hata huduma za afya sema tu kelele za baadhi ya wabunge na manung'uniko ya wananchi yamewafanya wasitishe. Ila zaidi soma hii taarifa hapa

UK Companies Investing in Tanzania Provide Positive Feedback - TanzaniaInvest

Article nzuri, fupi lakini ina maelezo muhimu. Barrick Gold naona wamiliki wamebadilishana sana. Kuna wakati nilisikia ni investors wa Canada, kuna wakati nikasikia familia ya Bush ni major investors. Lakini sishangai, dunia ya leo makampuni mengi makubwa yana investors kutoka kila sehemu, na wengi ni short term investors, watu wanapiga hela halafu wanahamia kwingine.
 
Hawa ndo serikali ilipaswa ikae nao chini kwanza wapange pamoja ili akija mwekezaji awe na shea ya nusu kwa nusu na hawa jamaa, kama hawana mitaji serikali ni jukumu lake kuwa wekea dhamana kwenye mabenki ya nje ili wapewe mikopo. Like reli ya kati wale wachina wangekuwa na ubia na Mo au barhesa wa nusu kwa nusu ingekuwa poa sana

Unaongelea serikali yetu kwa mawazo kama hayo?
 
Back
Top Bottom