Uwekezaji kwenye elimu

Uwekezaji kwenye elimu

gmail mkulima

Senior Member
Joined
Jun 11, 2017
Posts
186
Reaction score
114
Mimi ni kijana miaka au ukipenda niite mzee miaka 48 si kidogo, sasa wakuu naomba ushauri wenu ni hvi, nimeajiriwa mshahara sio mbaya , nina watoto 3 sasa shida nimewekeza sana kwenye elimu ya hawa watoto nimewapeleka shule bora hapa bongo ada mpaka 3m kwa term watoto wapo vzuri sana masomo yanapanda.
Shida niliyonayo wenzangu tuioajiriwa nao wapo mbali magari nyumba wameshajenga mi hata baiskeli sina hela bado mpangaji hela yote mpaka na mkopo umeishia kusomesha mpaka kiwanja nilinunua zamani nimeuza kwa ajili ya ada. Juzi binti yangu na mama yake wanataka niuze kiwanja changu eti huyu binti aende south africa kumalizia masomo, sasa nashidwa kuelewa nilikosea njia au vpi, hvi kuwekeza kwenye elimu inatakiwa ubaki bila chochote? Naombeni ushauri wakuu presha ipo juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni mpuuzi. Wengine tumesoma shule za kawaida laki shwali. Ishu siyo aina ya shule.Bali jitihada na uwezo wa mtoto. Pili mbuzi hula kadiri ya urefu wa kamba yake. Weww ni limbukeni na mfuata mikumbo. Kwa mwendo huo utakufa masikini. Wasome shule za serikali. Ziko vizuri sasa.
 
Hongera sana mkuu kwa kuona mbali zaidi. Elimu yao itakuwa na manufaa kwao wenyewe, kwako, na kwa taifa zima!!. Je, umewalea pia katika maadili ya imani yoyote ya dini? Hii itawajenga katika hofu ya Mungu. Hofu hii itawa'force' kukumbuka jitihada zako na umuhimu wako mzazi hata kama ni wajibu wako kutenda na haki yao kutendewa hayo. Na hapo huku ukiendelea kuwaombea Mungu wafanikiwe, utaweza kujengewa nyumba na kununuliwa gari hata ndani ya mwaka mmoja.
 
Wewe ni mpuuzi. Wengine tumesoma shule za kawaida laki shwali. Ishu siyo aina ya shule.Bali jitihada na uwezo wa mtoto. Pili mbuzi hula kadiri ya urefu wa kamba yake. Weww ni limbukeni na mfuata mikumbo. Kwa mwendo huo utakufa masikini. Wasome shule za serikali. Ziko vizuri sasa.
Hana akili kama ni kweli, kwa nini wasisome hapa bongo mpaka waende S.A?
 
Somesha elimu ya kawaida kulingana na uwezo wako, una peleka mtoto S.A hapa bongo hakuna vyuo na wakati akirudi mshahara ni uleule? shame on you
 
Mi naona mkeo na watoto wako wanakuona boya ndio maana wanakuambia uuze hicho kiwanja, tena ukute huyo binti si wako na mtoto kajua ndio maana yeye na mama yake wameungana kukuambia ufanye hivyo.....

Elimu hata uwekeze vipi kama mtoto ni mjinga ni mjinga tu, wapo wanaosoma hizi hizi shule za kidumu na maji ila wana uelewa mkubwa kuliko huyo wa english medium, zaidi watazidiana lugha ya kiingeleza tu. Usipoteze hela ili kuwafurahisha wao wakati wewe unaendelea teseka na madeni
 
Nashukuru kwa ushauri ila naomba kuuliza hvi nikijenga ghorofa nikanunua magari bdae nikifa inabaki kuwa Mali ya nani? Jibu ni Mali ya watoto, sasa nikiwasomesha wakapata uelewa si ntawambia pesa yote iliishia kwenye elimu. Maisha sa hvi ni very unpredictable unatoka asubuhi asubuhi jioni marehemu potelea mbali acha watoto wangu wapate elimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom