Uwekezaji katika kilimo

Nimekuelewa vzr sn kaka
Ukibahatika kwenda Misri, utafunguka kifikra na kugundua kuwa huna haja kuuliza iwapo kilimo Tz kinalipa au la! Kwanza huhitaji nguvu kubwa kama wenzetu kufanya shamba lizalishe! Misri mashamba yao ya asili kando ya mto Nile yalisha jaa hivyo wanapanua mashamba jangwani mchangani wanaurutubisha mchanga kwa mboji, samadi na mbolea zingine hadi unazalisha mazao! Ni gharama kubwa sana kutengeneza udongo huku wakipigana kuusukuma mchanga unaoletwa mashambani na upepo wa jangwa! Sisi Tanzania mashamba mengi udongo wake ni ready made! Mashamba mengi wala huweki mbolea na ikiwekwa kidogo tu! Kuna mazao mengi Tanzania si desturi kuweka mbolea na yanastawi vizuri tu!

Misri wanamwagilia maji na wanatumia gharama kubwa sana kwani wanayasukuma maji kwa mashine ambayo ni mitambo mizito kupandisha maji mashambani! Wataaalamu wa Misri katika kutetea tusipunguze maji yao Ziwa Victoria wanadai kuwa huku kwetu eneo la maziwa makuu mvua ni nyingi zinatutosha sana kwa uzalishaji bila hata kutumia maji ya mito, tatizo letu ni wavivu wa kufanya utafiti na wazito kutumia matokeo ya utafiti! Wamisri wanalima kwa mafanikio makubwa Mizeituni jangwani! Zeituni ni zao linalostawi vema huko ukanda wa kuelekea Gaza eneo la Sinai Peninsular kwenye mvua ndogo kabisa! Eneo lenye kilimo cha mizeituni kuna viwanda vingi vya kukamua mafuta ya mizeituni hivyo kufanya eneo hilo la jangwa kutoa ajira kubwa kwa wananchi wake!


Kwa hiyo kwa mwekezaji yeyote anachotakiwa hapa Tanzania ni kuwekeza kulingana na hali halisi ya hewa ya Tanzania! Kama tatizo ni ukame ni mkoa upi Mtama unagoma au unakauka kwa ukame kama ilivyo zao la mahindi? Nani anataka kutuaminisha kuwa mtama siyo dili! Au ni mkoa gani Mbaazi zinagoma? Nendeni Babati mkajionee mbaazi zinavyokubali na kuinua uchumi! Uhai wa mbaazi muda mwingi huwa wakati wa kiangazi. Haya ni baadhi tu ya mazao yanayostawi bila kuhitaji mvua na utashangazwa uonekane unayamwagilia! Hivi sasa Africa Mashariki chakula ni dili na haya mazao niliyotolea mfano yaani mtama na mbaazi hayauziki? Kunamazao mengi sana ya chakula hayahitaji mvua nyingi mfano, viazi, mihogo, alizeti, karanga, kunde n.k. Na haya mazao yanaweza kuwa mechanized!

Thailand inaongoza duniani kwa kilimo cha mihogo! Leo tumewaachia wazaramo wa mkuranga tu kulima mihogo kwa vijembe-mundu! Tatizo kila mtu ametolea macho kilimo cha mahindi tu na kulima mpunga! Tunaweza kuneemeka kwa kuendana na mazingira yetu jinsi yalivyo tukawekeza kwenye mazao yanayoendana na Hali ya hewa! Huko Dodoma zao la Zabibu linastawi sana na ni deal, mbona kilimo hicho hakisongi mbele, kama nitaelezwa tatizo ni ukame ni kwa vipi zao hilo halikushauriwa lilimwe mikoa mingine isipokuwa Dodoma kwenye ukame! Tuchague mazao ya kulima kulingana na ustahimilivu wake kwa hali ya hewa yetu!

Kaka mwekezaji njoo na mahela yako hayo wekeza kivyako, ukumbuke kuwa ujasiria mali ni kufikiria vile ambavyo wengine hawafikirii ili uwahi kuingia sokoni kabla wengine hawajaamka! Wakiamka wewe uwe uko mbali!

Niwie radhi sana kwa maelezo marefu saa zingine mimi nami mweeeeee!! Malila and El Nino heshima zangu pokeeni, you are my inspiration to join here!!
 
Back
Top Bottom