Uwekezaji katika kilimo

changman

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2011
Messages
229
Points
195

changman

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2011
229 195
Habari zenu. Mimi nafikiria kuwekeza kwenye kilimo. Natarajia kuwa mwekezaji wa kati, sio mkubwa kama azam au mdogo kabisa, ila wa kati. Nachotaka kufahamu ni kwamba, kilimo kinalipa tz sana sana ukizingatia mvua ni za kubahatisha? Pia serikali inasaidia wakulima/wawekezaji na misamaha ya kodi? Natanguliza shukrani.
 
Mwanahisa

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2012
Messages
1,395
Points
1,195

Mwanahisa

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2012
1,395 1,195
Mkuu, kwa misamaha ya kodi, nafikiri karibia farm input zote hazina kodi,
Mvua za kuendeshea kilimo zipo wala sio za kubahatisha ila taarifa za mvua na hali ya hewa ndio za ubabaishaji. Wawekezaji wakubwa hapa kwetu wanajenga vituo vya meteorology vyakwao binafsi kwa shughuli za kilimo. Pia ni vizuri ukapeleka soil samples za hiyo sehemu unayotaka kuwekeza katika maabara zipimwe ili kujua ni suitable for which type of mazao. Kila kheri kamanda.
 
Penelope

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Messages
717
Points
1,000

Penelope

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2012
717 1,000
Habari zenu. Mimi nafikiria kuwekeza kwenye kilimo. Natarajia kuwa mwekezaji wa kati, sio mkubwa kama azam au mdogo kabisa, ila wa kati. Nachotaka kufahamu ni kwamba, kilimo kinalipa tz sana sana ukizingatia mvua ni za kubahatisha? Pia serikali inasaidia wakulima/wawekezaji na misamaha ya kodi? Natanguliza shukrani.
Hata mimi napenda sana,nshajaribu nkakwama sababu ya kutegemea mvua ila Mungu akipenda mwakani tena ntajaribu
 
Mama Joe

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2009
Messages
1,507
Points
1,225

Mama Joe

JF-Expert Member
Joined Mar 30, 2009
1,507 1,225
Kukabiliana na mvua mnaelekezwa kutumia umwagaliaji aidha kwa kuchimba visima au kuchepusha maji ya mito mbona vyanzo vingi tu. Mzuzu alitoa thread ya Project funding source ambamo wadau na yeye walichangia kuhusu vyanzo vya kupta mitaji ya kilimo nk. Dark city anayo thread ya mikopo zote zipo sticky ujasiriamali ukizisoma utapata pa kuanzia. all the best
 
Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,585
Points
2,000

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,585 2,000
Habari zenu. Mimi nafikiria kuwekeza kwenye kilimo. Natarajia kuwa mwekezaji wa kati, sio mkubwa kama azam au mdogo kabisa, ila wa kati. Nachotaka kufahamu ni kwamba, kilimo kinalipa tz sana sana ukizingatia mvua ni za kubahatisha? Pia serikali inasaidia wakulima/wawekezaji na misamaha ya kodi? Natanguliza shukrani.
Unataka kulima na kuuza au kulima na kusindika?
 
CHASHA FARMING

Verified Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
6,728
Points
2,000

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined Jun 4, 2011
6,728 2,000
Mkuu hata USA wakulima wake wanategemea Mvua, hata huko Urusi ni nvua inategemewa,

Hapa nu USA, mahindi yamenyauka na Ukame,Na ndo maana kuanzia Mwakani huenda bei ya nafaka ikapanda mara dufu sana katika Soko La Dunia na hii ni kutokana na USA, Canada na Urusi kukumbwa na Ukame, Ikumbukwe kwamba Canada ndo mzalishaji namba moja wa Ngano Duniani akifuatiwa na URUSI na USA anazalisha Mahindi sana, so hizi nchi zinatarajia kupunguza Export
 
changman

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2011
Messages
229
Points
195

changman

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2011
229 195
Hivi na kuhusu ruzuku za mbolea, ndege waharibifu na kama una shamba kubwa huku nje kabisa ya mji, je usalama wake vipi, nikimaanisha watu kuja na kuchuma mahindi yako au ngedere kula? mambo haya unajiandaaje wakuu?
 
Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,585
Points
2,000

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,585 2,000
nyanya morogoro,nikaishia katikati sbb ya kuchelewa kunyesha mvua
Safari hii anza vizuri, perishable zote zina high risk sana hasa kwa wenye mitaji midogo, ila zina lipa sana. Anza na kilimo cha muda mfupi na muda mrefu kidogo kidogo. Kama unaweza kupata shamba lenye maji tungeongea kitu.
 
matumbo

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2011
Messages
7,194
Points
1,250

matumbo

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2011
7,194 1,250
Hivi na kuhusu ruzuku za mbolea, ndege waharibifu na kama una shamba kubwa huku nje kabisa ya mji, je usalama wake vipi, nikimaanisha watu kuja na kuchuma mahindi yako au ngedere kula? mambo haya unajiandaaje wakuu?
yani wewe unataka kulima ila inaonekana hauna idea kabisa ya kilimo..kama umedhamiria haswa basi nenda kwenye mashamba uko ukafanye study..ukirudi uko mwanangu lazima ukanunue jembe mwenyewe ukalime tena bila mashaka..sisi wenzio tulianzia ivyo ivyo.
 
Kubota

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2012
Messages
533
Points
500

Kubota

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2012
533 500
Ukibahatika kwenda Misri, utafunguka kifikra na kugundua kuwa huna haja kuuliza iwapo kilimo Tz kinalipa au la! Kwanza huhitaji nguvu kubwa kama wenzetu kufanya shamba lizalishe! Misri mashamba yao ya asili kando ya mto Nile yalisha jaa hivyo wanapanua mashamba jangwani mchangani wanaurutubisha mchanga kwa mboji, samadi na mbolea zingine hadi unazalisha mazao! Ni gharama kubwa sana kutengeneza udongo huku wakipigana kuusukuma mchanga unaoletwa mashambani na upepo wa jangwa! Sisi Tanzania mashamba mengi udongo wake ni ready made! Mashamba mengi wala huweki mbolea na ikiwekwa kidogo tu! Kuna mazao mengi Tanzania si desturi kuweka mbolea na yanastawi vizuri tu!

Misri wanamwagilia maji na wanatumia gharama kubwa sana kwani wanayasukuma maji kwa mashine ambayo ni mitambo mizito kupandisha maji mashambani! Wataaalamu wa Misri katika kutetea tusipunguze maji yao Ziwa Victoria wanadai kuwa huku kwetu eneo la maziwa makuu mvua ni nyingi zinatutosha sana kwa uzalishaji bila hata kutumia maji ya mito, tatizo letu ni wavivu wa kufanya utafiti na wazito kutumia matokeo ya utafiti! Wamisri wanalima kwa mafanikio makubwa Mizeituni jangwani! Zeituni ni zao linalostawi vema huko ukanda wa kuelekea Gaza eneo la Sinai Peninsular kwenye mvua ndogo kabisa! Eneo lenye kilimo cha mizeituni kuna viwanda vingi vya kukamua mafuta ya mizeituni hivyo kufanya eneo hilo la jangwa kutoa ajira kubwa kwa wananchi wake!

Kwa hiyo kwa mwekezaji yeyote anachotakiwa hapa Tanzania ni kuwekeza kulingana na hali halisi ya hewa ya Tanzania! Kama tatizo ni ukame ni mkoa upi Mtama unagoma au unakauka kwa ukame kama ilivyo zao la mahindi? Nani anataka kutuaminisha kuwa mtama siyo dili! Au ni mkoa gani Mbaazi zinagoma? Nendeni Babati mkajionee mbaazi zinavyokubali na kuinua uchumi! Uhai wa mbaazi muda mwingi huwa wakati wa kiangazi. Haya ni baadhi tu ya mazao yanayostawi bila kuhitaji mvua na utashangazwa uonekane unayamwagilia! Hivi sasa Africa Mashariki chakula ni dili na haya mazao niliyotolea mfano yaani mtama na mbaazi hayauziki? Kunamazao mengi sana ya chakula hayahitaji mvua nyingi mfano, viazi, mihogo, alizeti, karanga, kunde n.k. Na haya mazao yanaweza kuwa mechanized!

Thailand inaongoza duniani kwa kilimo cha mihogo! Leo tumewaachia wazaramo wa mkuranga tu kulima mihogo kwa vijembe-mundu! Tatizo kila mtu ametolea macho kilimo cha mahindi tu na kulima mpunga! Tunaweza kuneemeka kwa kuendana na mazingira yetu jinsi yalivyo tukawekeza kwenye mazao yanayoendana na Hali ya hewa! Huko Dodoma zao la Zabibu linastawi sana na ni deal, mbona kilimo hicho hakisongi mbele, kama nitaelezwa tatizo ni ukame ni kwa vipi zao hilo halikushauriwa lilimwe mikoa mingine isipokuwa Dodoma kwenye ukame! Tuchague mazao ya kulima kulingana na ustahimilivu wake kwa hali ya hewa yetu!

Kaka mwekezaji njoo na mahela yako hayo wekeza kivyako, ukumbuke kuwa ujasiria mali ni kufikiria vile ambavyo wengine hawafikirii ili uwahi kuingia sokoni kabla wengine hawajaamka! Wakiamka wewe uwe uko mbali!

Niwie radhi sana kwa maelezo marefu saa zingine mimi nami mweeeeee!! Malila and El Nino heshima zangu pokeeni, you are my inspiration to join here!!
 
Dangote

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Messages
204
Points
0

Dangote

JF-Expert Member
Joined Mar 30, 2012
204 0
Kama umeamua kuwekeza kwnye kilimo fanya research ya soko ya unachotaka kulima pia nakushauri usitegemee mvua chimba kisima au chanzo kingine cha uhakika climate change inatesa ila ukifanya kila kitu kwa usahihi kilimo ndo njia rahisi ya kua tajiri
 
Sabayi

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
2,316
Points
1,225

Sabayi

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2010
2,316 1,225
Ukibahatika kwenda Misri, utafunguka kifikra na kugundua kuwa huna haja kuuliza iwapo kilimo Tz kinalipa au la! Kwanza huhitaji nguvu kubwa kama wenzetu kufanya shamba lizalishe! Misri mashamba yao ya asili kando ya mto Nile yalisha jaa hivyo wanapanua mashamba jangwani mchangani wanaurutubisha mchanga kwa mboji, samadi na mbolea zingine hadi unazalisha mazao! Ni gharama kubwa sana kutengeneza udongo huku wakipigana kuusukuma mchanga unaoletwa mashambani na upepo wa jangwa! Sisi Tanzania mashamba mengi udongo wake ni ready made! Mashamba mengi wala huweki mbolea na ikiwekwa kidogo tu! Kuna mazao mengi Tanzania si desturi kuweka mbolea na yanastawi vizuri tu!

Misri wanamwagilia maji na wanatumia gharama kubwa sana kwani wanayasukuma maji kwa mashine ambayo ni mitambo mizito kupandisha maji mashambani! Wataaalamu wa Misri katika kutetea tusipunguze maji yao Ziwa Victoria wanadai kuwa huku kwetu eneo la maziwa makuu mvua ni nyingi zinatutosha sana kwa uzalishaji bila hata kutumia maji ya mito, tatizo letu ni wavivu wa kufanya utafiti na wazito kutumia matokeo ya utafiti! Wamisri wanalima kwa mafanikio makubwa Mizeituni jangwani! Zeituni ni zao linalostawi vema huko ukanda wa kuelekea Gaza eneo la Sinai Peninsular kwenye mvua ndogo kabisa! Eneo lenye kilimo cha mizeituni kuna viwanda vingi vya kukamua mafuta ya mizeituni hivyo kufanya eneo hilo la jangwa kutoa ajira kubwa kwa wananchi wake!

Kwa hiyo kwa mwekezaji yeyote anachotakiwa hapa Tanzania ni kuwekeza kulingana na hali halisi ya hewa ya Tanzania! Kama tatizo ni ukame ni mkoa upi Mtama unagoma au unakauka kwa ukame kama ilivyo zao la mahindi? Nani anataka kutuaminisha kuwa mtama siyo dili! Au ni mkoa gani Mbaazi zinagoma? Nendeni Babati mkajionee mbaazi zinavyokubali na kuinua uchumi! Uhai wa mbaazi muda mwingi huwa wakati wa kiangazi. Haya ni baadhi tu ya mazao yanayostawi bila kuhitaji mvua na utashangazwa uonekane unayamwagilia! Hivi sasa Africa Mashariki chakula ni dili na haya mazao niliyotolea mfano yaani mtama na mbaazi hayauziki? Kunamazao mengi sana ya chakula hayahitaji mvua nyingi mfano, viazi, mihogo, alizeti, karanga, kunde n.k. Na haya mazao yanaweza kuwa mechanized!

Thailand inaongoza duniani kwa kilimo cha mihogo! Leo tumewaachia wazaramo wa mkuranga tu kulima mihogo kwa vijembe-mundu! Tatizo kila mtu ametolea macho kilimo cha mahindi tu na kulima mpunga! Tunaweza kuneemeka kwa kuendana na mazingira yetu jinsi yalivyo tukawekeza kwenye mazao yanayoendana na Hali ya hewa! Huko Dodoma zao la Zabibu linastawi sana na ni deal, mbona kilimo hicho hakisongi mbele, kama nitaelezwa tatizo ni ukame ni kwa vipi zao hilo halikushauriwa lilimwe mikoa mingine isipokuwa Dodoma kwenye ukame! Tuchague mazao ya kulima kulingana na ustahimilivu wake kwa hali ya hewa yetu!

Kaka mwekezaji njoo na mahela yako hayo wekeza kivyako, ukumbuke kuwa ujasiria mali ni kufikiria vile ambavyo wengine hawafikirii ili uwahi kuingia sokoni kabla wengine hawajaamka! Wakiamka wewe uwe uko mbali!

Niwie radhi sana kwa maelezo marefu saa zingine mimi nami mweeeeee!! Malila and El Nino heshima zangu pokeeni, you are my inspiration to join here!!
Mkuu I salute you Huu mchango wako ni nondo za kutosha kabisa umeongea ukweli Mtupu
Kwa kifupi watanzania sisi ni wavivu sana wa kufikiri na kufanya kazi na tumeshakariri kazi za maofisini tu ndo Kuna Mkenya mmoja nilikutana naye Mombasa katika kupiga stori akaniambia TZ is Mining site for a Kenyana
Nataka nichangie kwenye zabibu hapo ndo umenigusa kwa taarifa tu Dunia nzima ni Dodoma peke yake ndo zabibu zinazaa mara mbili kwa mwaka na ndo zabibu bora zaidi funny enough Kenya ndo wanaongoza kwa kuziexport ulay hizo zabibu za Dodoma hasa Spain sisi tupo tunapiga siasa za CDM na CCM tu,South Sudan na Ethiopia wanategemea chakula toka Kenya ambao wananunua Mahindi toka kwetu tungekuwa tunazalisha kwa wingi huu upuuzi wa serikali wa kuzuia exports ya chakula usingekuwepo,Shame on us Tanzanians
 
Shavania

Member
Joined
Feb 10, 2018
Messages
5
Points
45

Shavania

Member
Joined Feb 10, 2018
5 45
Ukibahatika kwenda Misri, utafunguka kifikra na kugundua kuwa huna haja kuuliza iwapo kilimo Tz kinalipa au la! Kwanza huhitaji nguvu kubwa kama wenzetu kufanya shamba lizalishe! Misri mashamba yao ya asili kando ya mto Nile yalisha jaa hivyo wanapanua mashamba jangwani mchangani wanaurutubisha mchanga kwa mboji, samadi na mbolea zingine hadi unazalisha mazao! Ni gharama kubwa sana kutengeneza udongo huku wakipigana kuusukuma mchanga unaoletwa mashambani na upepo wa jangwa! Sisi Tanzania mashamba mengi udongo wake ni ready made! Mashamba mengi wala huweki mbolea na ikiwekwa kidogo tu! Kuna mazao mengi Tanzania si desturi kuweka mbolea na yanastawi vizuri tu!

Misri wanamwagilia maji na wanatumia gharama kubwa sana kwani wanayasukuma maji kwa mashine ambayo ni mitambo mizito kupandisha maji mashambani! Wataaalamu wa Misri katika kutetea tusipunguze maji yao Ziwa Victoria wanadai kuwa huku kwetu eneo la maziwa makuu mvua ni nyingi zinatutosha sana kwa uzalishaji bila hata kutumia maji ya mito, tatizo letu ni wavivu wa kufanya utafiti na wazito kutumia matokeo ya utafiti! Wamisri wanalima kwa mafanikio makubwa Mizeituni jangwani! Zeituni ni zao linalostawi vema huko ukanda wa kuelekea Gaza eneo la Sinai Peninsular kwenye mvua ndogo kabisa! Eneo lenye kilimo cha mizeituni kuna viwanda vingi vya kukamua mafuta ya mizeituni hivyo kufanya eneo hilo la jangwa kutoa ajira kubwa kwa wananchi wake!

Kwa hiyo kwa mwekezaji yeyote anachotakiwa hapa Tanzania ni kuwekeza kulingana na hali halisi ya hewa ya Tanzania! Kama tatizo ni ukame ni mkoa upi Mtama unagoma au unakauka kwa ukame kama ilivyo zao la mahindi? Nani anataka kutuaminisha kuwa mtama siyo dili! Au ni mkoa gani Mbaazi zinagoma? Nendeni Babati mkajionee mbaazi zinavyokubali na kuinua uchumi! Uhai wa mbaazi muda mwingi huwa wakati wa kiangazi. Haya ni baadhi tu ya mazao yanayostawi bila kuhitaji mvua na utashangazwa uonekane unayamwagilia! Hivi sasa Africa Mashariki chakula ni dili na haya mazao niliyotolea mfano yaani mtama na mbaazi hayauziki? Kunamazao mengi sana ya chakula hayahitaji mvua nyingi mfano, viazi, mihogo, alizeti, karanga, kunde n.k. Na haya mazao yanaweza kuwa mechanized!

Thailand inaongoza duniani kwa kilimo cha mihogo! Leo tumewaachia wazaramo wa mkuranga tu kulima mihogo kwa vijembe-mundu! Tatizo kila mtu ametolea macho kilimo cha mahindi tu na kulima mpunga! Tunaweza kuneemeka kwa kuendana na mazingira yetu jinsi yalivyo tukawekeza kwenye mazao yanayoendana na Hali ya hewa! Huko Dodoma zao la Zabibu linastawi sana na ni deal, mbona kilimo hicho hakisongi mbele, kama nitaelezwa tatizo ni ukame ni kwa vipi zao hilo halikushauriwa lilimwe mikoa mingine isipokuwa Dodoma kwenye ukame! Tuchague mazao ya kulima kulingana na ustahimilivu wake kwa hali ya hewa yetu!

Kaka mwekezaji njoo na mahela yako hayo wekeza kivyako, ukumbuke kuwa ujasiria mali ni kufikiria vile ambavyo wengine hawafikirii ili uwahi kuingia sokoni kabla wengine hawajaamka! Wakiamka wewe uwe uko mbali!

Niwie radhi sana kwa maelezo marefu saa zingine mimi nami mweeeeee!! Malila and El Nino heshima zangu pokeeni, you are my inspiration to join here!!
 
antimatter

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2017
Messages
1,977
Points
2,000

antimatter

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2017
1,977 2,000

Madini kuntu haya!
 
Forum statistics

Threads 1,392,812
Members 528,696
Posts 34,118,688
Top