Uwekezaji katika kilimo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwekezaji katika kilimo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jasusi, Aug 30, 2012.

 1. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Kama waekezaji wageni hawatakiwi Isimani, hawatakiwi Tanzania nzima

  Lukuvi awakataa wawekezaji Isimani
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Wednesday, 29 August 2012 21:04 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG]Mbunge wa Isimani, wilayani Iringa, Willium Lukuvi

  Tumaini Msowoya, Iringa
  MBUNGE wa Isimani, wilayani Iringa, Willium Lukuvi, amesema kuwa jimbo hilo halihitaji mwekezaji yeyote kutoka ughaibuni ili kuwekeza katika sekta ya kilimo kwa sababu ardhi iliyopo inawatosha wananchi wake pekee.Kauli hiyo ya Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) inafuatia kitendo cha jimbo hilo kuwa na miradi mingi ya kilimo cha umwagiliaji, yenye lengo la kuwasaidia wakulima kuondokana na kilimo cha kutegemea.
  “Kama akija mwekezaji basi awe mswahili wa hapa hapa nchini, lakini sifikirii kama kuna ardhi inayoweza kuwatosheleza wawekezaji kutoka nje, hii iliyopo inawatosha wananchi wangu na si zaidi ya hapo,” alisema Lukuvi.
  Pia alisema kufuatia vitendo vya baadhi ya wanunuzi kuwanyonya wakulima wa mpunga katika eneo lake, ameamua kujenga mashine za kukoboa mpunga, ili waanze kuuza mchele kwa bei inayolingana na gharama za uzalishaji.
  Alisema mashine hizo zitaongeza thamani ya mazao ya wananchi hao na hivyo kuwafanya wafanyabishara kununua mchele kutoka katika soko moja la wakulima.

  Alisema mashine ya kwanza imeshajengwa katika eneo la Idodi na nyingine iko katika mchakato wa kujengwa huko Pawaga.
  “Nataka tuuze malighafi sasa, kilimo chetu kitusaidie na mfanyabishara yeyote akitaka kununu mazao yetu, basi atanunua mpunga uliofungashwa na kuonyesha kwamb, huu unatokea Idodi au Pawaga,” alisema Lukuvi.
  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Tina Sekambo, alisema halmashauri imeanza mkakati wa kuunganisha barabara za vijijini, ili kuwarahisishia wananchi kusafirisha mazao na kuondokana na ugumu wa maisha.
  Alisema halmashauri hiyo imetumia zaidi ya Sh400 milioni, kujenga barabara kati ya Isimani na Pawaga, ili kuwawezesha wananchi wa Paganga wanaolima mpunga, kuusafirisha hadi Isimani, na Isimani waweze usafirisha mahindi hadi Pawaga.“Mtandao wa barabara ndio utakaosaidia soko la uhakika la mazao yetu, wilaya ya Iringa tumeliona hili,” alisema.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,124
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Huwa nina wasiwasi sana na matamshi yanayotolewa na waliomo kwenye hama tawala. Hunichukua muda mrefu kuyaamini au kuthibitisha yana nia gani hata kama machoni yana nia njema.
   
Loading...