Uwekezaji katika ardhi nchini unatunufaisha?

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,797
12,239
Leo jioni katika kipindi cha dira ya dunia BBC, Prof. Tibaijuka - waziri wa ardhi na maendeleo ya makati atashiriki katika mjadala endapo watanzania wananufaika na wawekezaji wa nje katika ardhi yetu au wananchi wetu wanaporwa ardhi yao kwa manufaa ya mafisadi.

Mjadala huu utakuwa muhimu sana na hasa ukizingatia jinsi migogoro ya ardhi inavyoibuka siku hadi siku nchini.

WanaJF tujadili swala hili ili ifikapo jioni Prof. ajue nini maoni ya watanzania.
 
unufaishi na unaturudisha kwenye ukoloni mambo leo kwanza watanzania wenyewe ardhi hatuimiliki kikamilifu wenye ardhi kubwa wengi wao ni mafidai watanzania walio wengi ukiwauliza mmoja mmoja wana ardhi ya ukubwa gani wengi utakuta baba, mama na fanilia ya watoto wanane mpaka kumi ardhi wanayomiliki ni less than nusu heka na tena ni eneo ambalo haliko surveyed(halina hati)
 
Huwezi kuzungumzia juu ya ardhi Tanzania bila kuangalia mahitaji ya ardhi Dunia nzima na huwezi kuzungumzia ardhi bila kuzungumzia uzalishaji wa chakula.Kwa kifupi ardhi na uzalishaji wa chakula ni vitu vinavyoendana.Kuna uhaba mkubwa wa nafaka duniani kwani binadamu wamekuwa wakitumia moja kwa moja au kupitia kwa wanyama.Kwa sasa hivi sehemu pekee duniani yenye ardhi ni Afrika na Amerika Kusini .Ulaya na Asia ambao waliamini mapinduzi ya viwanda na maswala ya ujenzi wa majumba hawana ardhi kutokana na kukabiliwa na uhaba wa ardhi hivyo wameanza kuvamia kwa kasi Afrika na kulaghai viongozi wetu wawape ardhi kwa ajili ya kuzalisha chakula lakini ukweli hawatazalisha chakula kwa ajili ya Watanzania bali watazalisha chakula kwa ajili ya nchi zao lakini kitu kingine kibaya Tumetoa ardhi yetu kwa ajili ya kuzalisha mazao ya nishati kitu ambacho hakina umuhimu kwetu.Lakini nchi yetu imezungukwa na nchi zenye matatizo ya chakula juzijuzi tumegawa ardhi kubwa kwa kampuni ya Marekani kwa ajili ya kuzalisha mazo yenye kiini tete,katika mkataba huo ambao kabla ya kusainiwa kuna watu walisafirishwa mpaka Marekani hatujui walipewa nini na pia iwapo kutatokea matatizo itabidi swala hili liamriwe nje ya Tanzania hii ni aina ya mikataba iliyokuwa inasainiwa na Karl Peters.Lakini serikari yetu imekuwa inatangaza mikoa mipya bila kujua inapunguza ardhi kwa ajili ya kilimo.Sasa hivi tu katika jumuiya ya Afrika Mashariki baadhi ya nchi zinataka swala la ardhi liwepo katika maswala ya Afrika Mashariki kutokana na baadhi ya nchi Rwanda na Burundi kutokuwa na ardhi ya kutosha wakati Kenya sehemu kubwa ya ardhi imekuwa inamilikiwa na ma settler bado swala hilo halijaafikiwa kwa sababu Watanzania wengi hatuliafiki.Kwa sasa hivi kuna migogoro mingi ya ardhi kati ya wananchi na wawekezaji nikitaja michache mgogoro kati ya wananchi wa Babati na wawekezaji,wananchi wa Mbarali na wawekezaji pia kuna migogoro kati ya wakulima na wafugaji na baadhi ya migogoro hiyo imesababisha mauaji.Kuna mbunge wa Mpanda alikuwa ameandaa hoja binafsi kuhusu ardhi sijui amefikia wapi ningefurahi kama mngemhoji.Kwa kifupi hatuhitaji wawekezaji wa ardhi kwani wakulima wetu wakiwezeshwa tuna uwezo wa kulisha ukanda wote wa kusini mwa Afrika kumbuka mpaka sasa hivi wakulima wetu wanatumia kilimo cha jembe la mkono na kilmo cha kutegemea mvua wakati nchi kama Iran wanavuna maji ya mvua na wanatumia umwagiliaji na vyote vinawezekana iwapo wanasiasa wakaacha kuwaingilia wataalamu kwani hata hiko kilimo kwanza ni cha kisiasa zaidi wataalam hawakupewa nafasi Serikali yetu ingejifunza kwa yale yaliyotokea Zimbabwe na Madagasika.Ninayo mengi ya kueleza lakini kwa leo naon
 
Back
Top Bottom