Uwe makini sana na vyakula vya shoprite .....

kwa kweli mim sielewi kwa nini watz tule vitu vya kwenye makopo,hivi hadi mboga mboga kweli tule za kuvundikwa wkt kila kitu kipo fresh.
naombeni mnisamehe nikisema sisi watanzania ni malimbukeni sana,ulaya ili ule vitu fresh ambavyo havijapuliziwa madawa inabidi ugharamie zaidi wkt sisi vitu hivyo vimezagaa ktk magenge yetu.
Kuna siku niliwasindikiza rafiki zangu pale shoprite ya kariakoo nikaona wana cheese zina ukungu kabisa na baadhi ya viu vingine vingi tu vimeoza lkn viko ktk shelves vinauzwa.
KULA MAVITU YA MAKOPO YALIYOJAZWA MADAWA SIO UMATAWI YA JUU NI USHAMBA,ULIMBUKENI NA KUTAFAHAMU MADHARA YA KULA VYAKULA NA MATUNDA yaliyowekewa dawa ili yadumu kwa muda mrefu.
 
PHP:
nyambala una point... na kariakoo... na Ilala na buguruni na masoko yoanyate tanzania....bora hata shoprite wana packaging ambayo ni formal na wanaandika best before...

kula tano yangu nyambala instantly

Wakuu nadhani ulewa wenu ni mdogo sana hivyo hakuna haja yakuwaweka ya kuchanganya watu kifupi ninyi endeleeni na jankfood kujiona wajanja na nasisi tutakula vyakina maganga vyenye utonvu saafi kabisa japokua vinauzwa mwenge buguruni kariakoo na bila kusahau kuna tred inaongelea waongozao kwa sukari vibosile na wadosi sasa ninyi mungu awaepushe msije kuwa miongoni wa hao au wenye Kansa maana mnavyo jiona kanakwamba mlizaliwa kwenye hayo mashoping senta wakati umekulia kwenye hivyo mnavyo vikashif leo
 
Narudia tena, Jamani laiti ningekuwa huko nyumbani basi ningenunua matunda na mboga na vyakula vya aina yoyote kwenye masoko ya mtaani. Hizi canned juice, fruits, beef etc. sio vizuri kabisa kwa afya zetu sababu ziko very processed na sio organic!. Huku US tunanunua canned foodstuffs kwenye grocery stores sababu hatuna jinsi na ukitaka organic foodstuffs ni expensive.
Nawashauri watu mlioko nyumbani muache kabisa kununua boxed/canned foodstuff kwenye hizo supermarkets. nunueni vitu kwenye masoko yetu huko mtaani. Kama ni kuku nunueni wa kienyeji, mboga nunueni za masoko ya mtaani. Hizi Canned/packed foodstuffs za huko Shoprite zitatuua na tuelewe kuwa kununua chakula katika masoko ya mtaani sio ushamba. Ushauri wa bure ili kuokoa afya zetu!!!!
Ahsanteni
 
loh, asante ngoshwe umetushtua. nitajitahidi kuwa makini. ina maana ufisadi ama uzembe umeishaingia hadi TFDA? haha, basi tumekwisha jamani

Ufisadi unaweza ukawa upo kila mahali.
Cha kujiuliza kwa nini shoprite wanaleta matunda fresh kutoka S.A, kwa nini wasinunue ya hapa kwetu?
 
yaani nilivyo na usongo na vyakula natural halafu nasikia mtu yuko tz kaenda nunua vyakula supermarket nachoka kabisa

ngoswe masoko yapo kibao mtaani yanini ukauziwe matunda na mboga za mwaka jana toka south africa??

Tanzania pia kuna raia wa mataifa mengine ambo wamezoea kununua vyakula supermarkets. Vile vile kuna watanzania ambao kwa status zao wanaona shida kwenda kufanya shopping kwenye masoko ya mtaani kwetu kama buguruni, Kkoo nk. either kutokana na mazingira ya uchafu kwenye hayo masoko au kukosekana kwa ustaarab, wizi nk. Hivyo Shoprite wana target this kind of customers.
 
Tanzania pia kuna raia wa mataifa mengine ambo wamezoea kununua vyakula supermarkets. Vile vile kuna watanzania ambao kwa status zao wanaona shida kwenda kufanya shopping kwenye masoko ya mtaani kwetu kama buguruni, Kkoo nk. either kutokana na mazingira ya uchafu kwenye hayo masoko au kukosekana kwa ustaarab, wizi nk. Hivyo Shoprite wana target this kind of customers.

Bongo usipoenda supermarket utaonekanaje wewe ni mtu wa kisasa? Mimi naona ni ushambaa tu. Kwa mfano ukienda kariakoo unapata nyanya iliyotoka lushoto jana yake very fresh. Hilo la kwamaba kuna watu wana status zao na hawewezi kwenda buguruni silikubali hata kidogo. Pita pale soko la kisutu siku ya jumamosi uone magari ya balozi mbalimbali na mashirika ya kimataifa yalivyo mengi.Wao hawajisumbui kwenda huko mnakofagailia kununua vitunguu wakati hapo |Kisutu vipo fresh.Wabongo tunaona ni deal kweanye supermarket na nkununua vitunguu vilivyokatwa katwa tayri, sijui ni uvivu
 
Good topic! pia kwakuongeza ni kua kwa wale walevi wenzangu pia mkisikia kunaPromotion ya bia fulani si vizuri kwenda hapo, wanakwambia nunua mbili upate tatu mara nyingi vinywaji hivi utakuta vimeshakwisha muda wake na sio nzuri kwa afya ya mywaji! Hiyo ya kwenye Super Market imeshanikuta mara kama mbili, nilinunua Biscut kuzifungua tu nikakuta kuna wale minyoo nilipoawarudishia wakaniomba msamaha halafu wakashusha Biscut zoote zilizokua kwenye shelf, hii ndio Bongo mwendo mdundo.
 
Back
Top Bottom