SoC03 Uwazi Taasisi za Umma na Mashirika ya Serikali

Stories of Change - 2023 Competition

abdulatif

New Member
Feb 14, 2014
1
1
Uwazi unamaanisha uaminifu, maadili na uwajibikaji ambao serikali na mashirika ya umma wanapaswa kuwa nao ili kuwafanya raia kujua taratibu na shughuli ambazo uwekezaji wa kiuchumi unafanyika. uwazi na upatikanaji wa habari kwa umma Inahusisha kufanya maamuzi ya serikali mfano teuzi, sera na taarifa muhimu kwa wananchi.

Tunapoelekea hali inazidi kuwa mbaya, hii ni kutokana na baadhi ya watumishi kukosa maadili ya utumishi bora, Baadhi ya viongozi wamekuwa wakifanya maamuzi kwa utashi wao bila kuzingatia na kufuata kanuni na taratibu. Miongoni mwa sifa kubwa ya kiongozi bora ni uwazi, kukosekana kwa uwazi ni kiashiria kuwa utendaji wa kiongozi huyo hauridhishina huenda kukawa na ubadhilifu katika utendaji wake.

Hivyo basi ni vyema kama mtu anapopata ajira ama teuzi kwa miez 12 ya mwanzo achungunzwe kwa uhakika je, anavigezo vya kuwa mtumishi bora? Nje ya hapo ndio inaleta taharuki kwa utendaji wake mfano mkataba wa ujenzi bandari ya Tanga na mikataba ya madini, mikataba ya ununuzi wa rada na mingineyo.

Mikataba hii wengi tumeifahamu kupitia vikao vya bunge na kuonekana inamapungufu ama ukandamizaji kwa namna nyingine kutokana na vifubgu vilivyowekwa, swali ni je! Kungekuwa na uwazi katika mikataba hii na kushirikishwa kwa wananchi ni kweli ingefikia sintofahamu iliyotokea?

 
Back
Top Bottom