Uwanja wa Yanga: Ilala yamtwisha mzigo Rais

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
Dar es Salaam.

Hatima ya uwanja wa klabu ya Yanga, Kaunda sasa ipo mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.



Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa aliliambia gazeti hili jana kuwa hakuna mamlaka yoyote si manispaa, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wala Wizara ya Ardhi ambayo ipo tayari kubeba msalaba kwa kitu ambacho kinajulikana wazi hakiwezekani.



"Mwenye mamlaka ya kubadili matumizi ya ardhi, kuiruhusu Yanga ipewe eneo hilo ni Rais pekee, akitoa agizo, basi sisi tutatekeleza hatuna jinsi, lakini si mamlaka nyingine yoyote, lile eneo haliwezekani kujengwa bila kuharibu miundombinu, bila ya kuathiri watu wengine.



Mwananchi
 
Watu wanatafuta sababu za kuvuta muda wa kuendelea kuwepo madarakani kwa kitu ambacho inajulikana ni ngumu kufanyika.
 
kwa utaratibu huu naona kila kitu tayari na sheria za ardhi projeckt kubwa ni lazima rais asaini mimi sioni sababu kutokupewa eneo bahari au mito mikubwa inahamishwa itashindwa maji ya msimu
 
Mmm !!!
Hata cha kufanyia mazoezi ingekuwa msaada mkubwa wakukumbukwa kwa wana jangwani, Sasa watamaliza muda wa nyongeza pakiendelea kuwa hivi nyakati za mvua kweli ?
IMG-20140412-WA0049.jpg
 
kwa jins palivyo,kujenga jangwani ni gharama kubwa,hapo bado kulipa watu watu fidia
 
Yanga nao! Maeneo yote yaliyojaa Bongo bado wanang'ang'ania tu kujenga uwanja kwenye mto? Waambie waache utoto bwana.
Ova
 
Yanga wanaona mbali kibiashara katika hili na wanazo sababu lukuki za kuomba wapewe hapo hapo jangwani. Uholanzi imejengwa ndani ya bahari na hili lilifanyika baada ya kuisukumizia mbali bahari. Tatizo la watz wengi ni kwamba wana PhD za kwenye makaratasi lakini hawawezi kuzitumia katika maisha ya kila siku.

Yanga walishasema watalipa fidia, na wanajua wao watafanyaje ili hayo maji yasisumbue (kitaalamu inawezekana kabisa). Jambo la msingi hapa kwa watawala si kukatalia eneo kwa sababu eti kuna mkondo sijui maji machafu etc, wanachotakiwa kufanya ni kuwaambia Yanga (wataalamu wao) wawajibu maswali yao waliyonayo kwa kuwaelekeza na kuwafundisha ni namna gani watadhibiti hali ya hapo.
 
Mmmm!
Yanga toeni kitu kidogo kwa hako kabwana mdogo atawapa wala kwa rais isingefika.huyo bila hicho mnajisumbua
 
Back
Top Bottom