CPU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 3,863
- 687
Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere - Julius Nyerere International Airport (JNIA) umefunguliwa rasmi tena leo Feb 17, 2011 mchana saa saba na dk 4 baada ya kufungwa muda mfupi ilipotua ndege ya Shirika ya Swiss jana saa tatu usiku. Uwanja huo ulifungwa kutokana na milipuko ya mabomu kambi ya jeshi Ukonga jijini Dar es Salaam
Mabomu hayo pia yaliruka na kuingia mpaka ndani ya uwanja huo na kuharibu baadhi ya maeneo yanayotumika kupitia ndege, yaani TAXWAY pamoja na RUNWAY ambapo vipande vipatavyo kumi vya mabomu vilionekana ktk runway ya uwanja huo.
Ndege ya shirika la Ndege la Afrika ya Kusini, South African Airways kama ilivyokutwa leo Feb 17, 2011 majira ya saa Kumi jioni, ambapo ilishindwa kuendelea na safari
Ndege ndogo ndio zilianza kuruka baada ya kuruhusiwa kuruka leo Feb 17, 2011 mchana saa nane.
Ndege ya shirika la Ndege la Switzerland, Swiss Airways kama ilivyokutwa leo Feb 17, 2011 ambapo mpaka saa 12 jioni ilikuwa haijaondoka
Hata hivyo ktk tukio hilo la aina yake, jana usiku abiria waliokuwa ktk ndege hiyo ya Swiss waligoma kushuka ktk ndege hiyo kutokana na kupata hofu ya milipuko ya mabomu ambapo baadhi walisema ni bora wafie humo humo ndani ya ndege. Wakati abiria hao wakigoma kushuka, abiria wengine waliokuwa wanasubiri kuondoka walitaharuki na kuanza kukimbilia ndani ya ndege ya Swiss bila ya kuruhusiwa.
Ndege hiyo pia ilinusurika kupigwa na milipuko hiyo ya mabomu ambapo ilitua upande wa pili wa runway ya uwanja huo wa ndege kuelekea upande ambapo mabomu yalikuwa yanalipuka.
Picha za maeneo ya yaliyochimbika ktk uwanja huo nitawaletea muda si mrefu
All News by CPU