Uwanja wa ndege Dar waingia 10 bora Afrika

Uwanja wa ndege Dar waingia 10 bora Afrika

Mwandishi wa makala hii yaonekana hajawahi kutoka nje ya Tanzania. Uandishi gani huuu? Amefanya comparison na viwanja vipi?anazungumzia jengo la abiria au uwanja wenyewe! Hatuna waandishi
 
Hata kama ni vya ovyo!
Ndio maana yake Mkuu... kinyume na hivyo kuna kupimwa mkojo... kuhusishwa na madawa ya kulevya "outdated" kama si hivyo kuna kuhojiwa uraia.. utakatishaji... uhujumu... uhaini kama si ugaidi!!!
 
View attachment 1170535

Zaidi ya abiria milioni nane watahudumiwa katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) baada ya kukamilika kwa jengo la tatu la abiria (Terminal III), huku jengo hilo jipya likiwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka.

Uwezo wa kuhudumia abiria hao kwa mwaka unaufanya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kuingia katika viwanja kumi Afrika vyenye uwezo wa kuchukua abiria wengi. Jengo la kwanza la abiria (Terminal 1) lina uwezo wa kuhudumia abiria 500,000 kwa mwaka wakati jengo la pili (Terminal 2) likiwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 1.5 kwa mwaka.

Hata hivyo, jengo la Terminal 2 ambalo ndilo linatumika kwa sasa limekuwa likilemewa na wingi wa abiria mpaka kufikia milioni 2.6 kwa mwaka. Kukamilika kwa jengo la tatu la abiria kutapunguza msongamano wa abiria kwenye jengo la pili na kurahisisha shughuli za usafiri wa ndani na nje ya nchi.

Akizungumzia mradi huo jana Alhamisi Agosti Mosi, 2019 wakati wa hafla ya uzinduzi uliofanywa na Rais John Magufuli, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale alisema wazo la kujenga uwanja huo lilikuja baada ya jengo la pili kuelemewa na wingi wa abiria.
Huu uwanja bado mdogo sana tunataka kiwanja kihudumie watu million kama 15 tu hivi kwa mwaka
 
Wangejaribu kufanya maarifa ili runway iongezeke kidogo from 3 kms to 3.3 kms.
 
Kwanza ni uwongo kusema kwamba jengo la pili lilikuwa limeelemewa na uwingi wa abiria.

Tunaweza kuwa na jengo la kuhudumia abiria milioni 100 lakini tusipate hata abiria milioni 5. Jengo halileti abiria bali ni mwingiliano mkubwa wa shughuli za kiuchumi kati ya nchi moja na mataifa mengi na kati ya wananchi wa ndani ya nchi.
Ni kweli mkuu jengo lilishaelemewa kwa kiasi kikubwa kwa maana ya idadi ya watu wanaosafiri versus facilities zilizopo mfano mdogo tu ni vyoo, desk za immigration,check in counters,conveyer belts....na n. k ilikuwa ni vurugu tupu.
La shughuli za kiuchumi mia kwa mia sheikh wangu.
 
Haya huku ndanda siku ya sita umeme sio wa uhakika dakika kumi umeme masaa nane haupo. Bora msitujengee kiwanja cha ndege maana tutatia aibu
Umeandika maneno manne tu hapo na ikawa hivi; je, ukiandika maneno mia moja itakuwa vipi?
 
Ni makosa makubwa kumsahau mtu aliyeanzisha ujenzi wa terminal 3 hii ya kisasa na akaiacha 90% ikiwa imekamilika
Tutakuwa tunakosea kubinafsisha vitu vya kiofisi. Ni serikali hiyo hiyo inayotenda yote hata kama uongozi serikalini unabadilika. Wanaosema tumsifu Rais Mstaafu Kikwete kwa kuwa wazo la kujenga Terminal 3 lilianzishwa wakati wa utawala wake ni wale tu ambao kwa sababu zao binafsi hawataki Rais Magufuli asifiwe. Kama ni hivyo, basi hata kuhamia Dodoma asifiwe Mwalimu Nyerere.
 
View attachment 1170535

Zaidi ya abiria milioni nane watahudumiwa katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) baada ya kukamilika kwa jengo la tatu la abiria (Terminal III), huku jengo hilo jipya likiwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka.

Uwezo wa kuhudumia abiria hao kwa mwaka unaufanya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kuingia katika viwanja kumi Afrika vyenye uwezo wa kuchukua abiria wengi. Jengo la kwanza la abiria (Terminal 1) lina uwezo wa kuhudumia abiria 500,000 kwa mwaka wakati jengo la pili (Terminal 2) likiwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 1.5 kwa mwaka.

Hata hivyo, jengo la Terminal 2 ambalo ndilo linatumika kwa sasa limekuwa likilemewa na wingi wa abiria mpaka kufikia milioni 2.6 kwa mwaka. Kukamilika kwa jengo la tatu la abiria kutapunguza msongamano wa abiria kwenye jengo la pili na kurahisisha shughuli za usafiri wa ndani na nje ya nchi.

Akizungumzia mradi huo jana Alhamisi Agosti Mosi, 2019 wakati wa hafla ya uzinduzi uliofanywa na Rais John Magufuli, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale alisema wazo la kujenga uwanja huo lilikuja baada ya jengo la pili kuelemewa na wingi wa abiria.
Na hiki kimeingia kumi nn?😂😎😂😤😤😤
3.jpg

Cc: BAK
 
Tutakuwa tunakosea kubinafsisha vitu vya kiofisi. Ni serikali hiyo hiyo inayotenda yote hata kama uongozi serikalini unabadilika. Wanaosema tumsifu Rais Mstaafu Kikwete kwa kuwa wazo la kujenga Terminal 3 lilianzishwa wakati wa utawala wake ni wale tu ambao kwa sababu zao binafsi hawataki Rais Magufuli asifiwe. Kama ni hivyo, basi hata kuhamia Dodoma asifiwe Mwalimu Nyerere.
Hatusemi asisifiwe tumesema uwanja ulijengwa 85 % kipindi cha JK na sio wazo tu. Sasa kunatatizo gani kutambua juhudi zake mbona uwanja wa mpira alisema wazi tunamshukuru mzee mkapa kwa uwanja huu. Rais JPM kuna mengi mazuri anayafanya kama ujenzi wa SGR na Stieglers Gorge pamoja na wazo lilikua la mwalimu lakini kazi haikuanza kaianza yeye lazima tumpongeze kwa hilo na mengine mazuri ayafanyayo.
 
We si Umezoea DXB na Heathrow
Mpaka mwaka jana katika listi ya the worst airport in Africa tulishika namba saba katika ya kumi.
 
Kama hujui mpaka ufafanuliwe hizo ajira zitatoka wapi, basi ww ni nyumbu tu.

Sasa matusi ya nini tena?
Ungetufafanulia tu hizo ajira ni zipi maana yawezekana wengine hawazijui. Jambo lililo wazi linaonekana, hivyo huna sababu ya kutumia nguvu kubwa kulazimisha mtu/watu walikubali.
 
Back
Top Bottom