Uwanja wa Michezo au Uwanja wa Vita?

Ericus Kimasha

JF-Expert Member
Oct 27, 2006
488
470
Hii hali na maandalizi ya askari katika uwanja wa Taifa yanatoa tafsiri tata.
3965043cc7b5d3b1832b744bb9f75184.jpg

Haieleweki ni washabiki wataangalia mchezo wa mpira au vita kati ya majeshi yetu na adui asiyejulikana.
f4c21b69087df02ec067095532294af6.jpg

Maandalizi ya majeshi yanaonekana kuwa ya juu zaidi kuliko hata timu zilizopangiwa kucheza mechi leo!

Pasipokujua majeshi yanawakomaza wananchi kuzoea hali za vitisho na mazingira ya kivita. Na kama TFF haitakemea vitisho hivi, itakuwa inapalilia anguko la mchezo na mapato kwa ujumla.

Ninabashiri sarakasi kubwa za baadhi ya watu wazito kuzuiwa kuingia uwanjani leo hii. Au kudakwa kwenye mageti ya kuingilia na kupelekwa central kwa visingizio kama vile "tulikuwa tunamtafuta"
 
Haha. Hii inatokeaga tu pale ambapo unakuta nchi inatawaliwa na kiongozi ambaye hakuwa chagua la watu na pia hana mvuto wa kuvutia hisia za watu kwa kila akifanyacho, kiwe kibaya au kizuri..
 
Haha. Hii inatokeaga tu pale ambapo unakuta nchi inatawaliwa na kiongozi ambaye hakuwa chagua la watu na pia hana mvuto wa kuvutia hisia za watu kwa kila akifanyacho, kiwe kibaya au kizuri..
Unataka kusema mtawala havutii?
 
Back
Top Bottom