chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,376
- 24,928
Utaitwa uwanja wa Ndesamburo kwa heshima yake!
Leo katika shughuli za kuaga mwili wa nguri na mwanasiasa mkongwe, mashuhuri, maarufu, tegemeo kwa chama na wananchi wa manispaa ya Moshi...kumetokea ombi la kuteua mtaa maarufu na upewe jina la Ndesamburo. Ombi hilo lilitolewa la Mh. Zitto Zuberi Kabwe alipokuwa anatoa salamu zake.
Aidha Mstahiki Mayor wa Manispaa ya Moshi akauambia umma wa waombolezaji kuwa anaagiza Madiwani katika mpango wa ujenzi wa uwanja huo (majengo) upewe jina la Ndesamburo kama kumuenzi na kumkumbuka. Jambo hilo lilipokelewa kwa furaha na wato wote.
RIP Ndesa Pesa.