Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu wenye uwezo wa kubeba mashabiki 15,000 kujengwa Geita

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,207
4,703
Mkoa wa Geita umeanza maandalizi ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu utakaokuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 15,000 kwa wakati mmoja.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema uwanja huo utajengwa na SUMA JKT kwa awamu kutegemea vyanzo vya mapato ya ndani unatarajiwa kuchukua miaka minne kukamilika.

“Uwepo wa uwanja utasaidia kuvutia wawekezaji na pia kukuza vipaji vya vijana wa mkoa wa Geita lakini pia kukuza sekta ya michezo mkoa wa Geita,” amesema Mhandisi Gabriel.

Uwanja huo utakapokamilika unatajwa kuwa chachu ya kupata timu shiriki kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

443992ba2a69e417cc15acc4d2814423.jpg
 
Suma uwezo wa kujenga viwanja vinavyoitwa vya kisasa wametoa wapi? Kwa nini wasijenge kiwanja cha Nyamagana, labda km kinajengwa kwa bajeti ya mkoa. Kujenga Nyamagana kutawezesha taifa ku-host mashindano makubwa sababu Mwanza miundombinu mingine inaruhusu
Nyamagana hapatoshi ni eneo dogo sana. Lilifaa wakati ule mji wa Mwanza ulikuwa na watu wachache. Pale ni pafinyu sana.
 
Mkoa wa Geita umeanza maandalizi ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu utakaokuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 15,000 kwa wakati mmoja.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema uwanja huo utajengwa na SUMA JKT kwa awamu kutegemea vyanzo vya mapato ya ndani unatarajiwa kuchukua miaka minne kukamilika.

“Uwepo wa uwanja utasaidia kuvutia wawekezaji na pia kukuza vipaji vya vijana wa mkoa wa Geita lakini pia kukuza sekta ya michezo mkoa wa Geita,” amesema Mhandisi Gabriel.

Uwanja huo utakapokamilika unatajwa kuwa chachu ya kupata timu shiriki kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

View attachment 1546965
Daaah huyu jamaa atafilisi nchi kwa ufisadi,yani kila kitu anapeleka geita ila ajue tu kuna siku vitamgeukia ajibu ufisadi wake
 
Ngoja atoke madarakani kama vyote ivo vitakumbukwa viko geita! Majengo yatakuwa magodaun hifazi watawinda kila mtu atachukua chake litabaki pori kama mapori mengine yasokuwa na faida, uwanja utakuwa wa umitashumta
 
Back
Top Bottom