Uwajibikaji wa mawaziri Tanzania

iron2012

JF-Expert Member
Feb 16, 2012
500
206
hivi hawa mawaziri wa Vasco Dagama wanajua maana ya uwajibikaji? maana kwa wenzetu walioendelea kashfa ndogo tu hata kama waziri hakuhusika moja kwa moja anajiuzuru hapa kwetu mpaka wananchi waandamane ?
 
Kuwajibika sio kujiuzulu tu!
 
Ukisoma vizuri Ibara ya 8 ya Katiba (siyo mpya bali iliyopo) wanaopaswa kuwajibika ni Wananchi wa Tanzania kwa kushindwa kuwawajibisha viongozi wao.........kwa nchi kama Kenya kwa uvundo ulioripotiwa Bungeni hao wangekuwa herstoria tu sasa
hivi hawa mawaziri wa Vasco Dagama wanajua maana ya uwajibikaji? maana kwa wenzetu walioendelea kashfa ndogo tu hata kama waziri hakuhusika moja kwa moja anajiuzuru hapa kwetu mpaka wananchi waandamane ?
 
JK anaongea wishful thinking, hatuwezi kukomboa nchi kwa matarajio pekee. He has to walk the talk.

Kama hataki ku-walk, let us walk over him. Tanzania itabaki kuwepo daima, JK atapita na kupotea kama kivuli kinavyopita mchana na kinavyopotea wakati wa usiku.
 
hivi hawa mawaziri wa Vasco Dagama wanajua maana ya uwajibikaji? maana kwa wenzetu walioendelea kashfa ndogo tu hata kama waziri hakuhusika moja kwa moja anajiuzuru hapa kwetu mpaka wananchi waandamane ?

Aisee ni Nyerere pekee yake aliyekuwa na ubavu wa kumfukuza kazi mtu yoyote hata awe mshikaji..
Sasa hivi watakujibu wanavyotaka sababu serikali ni yao..
Ni Mungu tu aingilie kati bila hivyo tutavurugwa na shetani mpaka tushangae.. watanzania hali ni mbaya..
 
Kitendo cha kutotoa tamko lolote juu ya mawaziri nane waliotakiwa kujiuzuru kimewaudhi wabunge na mkakati uliopo sasa ni kwamba katika Bunge lijalo la bajeti, ikiwa hao mawaziri bado watakuwapo madarakani basi wajue wazi kwamba bajeti za wizara zao hazitapitishwa. Wabunge wanasema hawawezi kupitisha bajeti ya wizara ikasimamiwe na waziri mtuhumiwa.

Nadhani ni mkakati mzuri pia. Sijui wabunge wakigoma kabisa kupitisha bajeti ya wizara nini kinatokea. Bunge lote linavunjwa?

Original source: Mwananchi
 
Pamoja na misukosuko na matusi yote yanayoelekezwa kwa baadhi ya mawaziri kushiriki katika ufisadi, bado wameng'ang'ania!

Kwa hali ya kawaida mtu mwadilifu angeisha achia ngazi zamani. Hivyo nashauri baada ya wanaotuhumiwa kwa ufisadi wakiondolewa katika nafasi zao za uwaziri vyombo vya dola viwachunguze na kuwafikisha mahakamani kwa kutumia madaraka yao vibaya.
 
Kitendo cha kutotoa tamko lolote juu ya mawaziri nane waliotakiwa kujiuzuru kimewaudhi wabunge na mkakati uliopo sasa ni kwamba katika Bunge lijalo la bajeti, ikiwa hao mawaziri bado watakuwapo madarakani basi wajue wazi kwamba bajeti za wizara zao hazitapitishwa. Wabunge wanasema hawawezi kupitisha bajeti ya wizara ikasimamiwe na waziri mtuhumiwa.

Nadhani ni mkakati mzuri pia. Sijui wabunge wakigoma kabisa kupitisha bajeti ya wizara nini kinatokea. Bunge lote linavunjwa?

Original source: Mwananchi

Mkuu, huo sio mkakati mzuri, hao wabunge ni wanafiki. Wanao uwezo wa hata kumtoa Rais madarakani. Unajua hata kuandaa budget kwenyewe kunagharama zitatumika, kutopitisha budget maana yake hutaki maendeleo yafanyike. Yaani wao wakae tu bungeni wanalipwa wananenepa halafu kazi yao kukwamisha budget zisipite ili wanachi waumie. Mimi nafikiri watumie uwezo tuliowapa kumlazimisha rais kutekeleza kile kinachofaa, vinginevyo basi inabidi wananchi wenyewe watumie veto yao waingie mtaani.
 
1.mwanainchi ya jumapili iliandika MAIGE alivyompatia dola 3000 girl mhudumu wa ndege

hata yule girl akasita ila jamaa akaomba girl azipokee na baadae ampigie

2.Ni raha kutembea na simu tatu, computa mbili, bunduki mbili na wake za watu
 
Tafakari: Mawaziri watishiana vifo - Source: Tanzania Daima

MAWAZIRI wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wako katika vita yawaziwazi ya kugombea kubaki madarakani kiasi cha kutishiana kifo.
Ugomvi huo pia uko kati ya wabunge na mawaziri ambaoumejionyesha zaidi katika mkutano wa Bunge wa saba, uliomalizika jana mjini Dodoma.
Mawaziri walio katika vita hiyo ya kupigana fitna, vijembe nipamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami na Naibu wake, LazaroNyalandu; na Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, ambaye yuko katika mnyukano wakisiasa na Naibu wake, Athuman Mfutakamba.
Duru za siasa kutoka ndani ya wizara hizo, zinasema kuwamawaziri hao licha ya kufanya kazi katika ofisi moja, wako kwenye uhasama kiasicha kushindwa kusalimiana.
Sababu kubwa ya mawaziri hao kugongana, imeelezwa kuwa ni uchuwa kutaka kubaki madarakani hasa katika kipindi hiki ambapo Rais Jakaya Kikweteanatarajia kufanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri.
Mmoja kati ya mawaziri hao ambaye jina lake linahifadhiwakwa sasa, aliliambia gazeti hili jana kuwa waziri mwenzake amemtishia kifo.
………………………..
Hata hivyo akifunga mkutano wa Bunge juzi, Spika Anna Makindaaliwataka mawaziri walioibuliwa tuhuma mbalimbali bungeni kutoweka kinyongo kwawabunge walioibua tuhuma hizo.
Alisema wabunge walijadili masuala mbalimbali kwa uwazi kwa lengola kuboresha ufanisi wa kazi katika wizara hizo hivyo kuwataka kuchukua masualahayo kama changamoto.
"Msichukulie hasira kuhusu yaliyozungumzwa humu mpaka mkapasukamifupa… waziri utasemwaje kama hujahusika?Hiyo mliyopewa ni changamoto; mnatakiwa kufanya kazi vizuri zaidi," alisema nakuwasihi waondoke bungeni wakiwa marafiki.
Walioshinikizwa kujiuzulu ni Waziri wa Viwanda na Biashara,Cyril Chami; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika; na Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu naWaziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.
Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja; NaibuWaziri wa Afya, Lucy Nkya; na Naibu Waziri wa Viwanda, Lazaro Nyarandu.
 
kugoma kupitisha bajeti ni sawa na kupiga kura ya kutokuwa na imani na serijkali. inabidi bunge livunjwe uitshwe uchaguzi
Kitendo cha kutotoa tamko lolote juu ya mawaziri nane waliotakiwa kujiuzuru kimewaudhi wabunge na mkakati uliopo sasa ni kwamba katika Bunge lijalo la bajeti, ikiwa hao mawaziri bado watakuwapo madarakani basi wajue wazi kwamba bajeti za wizara zao hazitapitishwa. Wabunge wanasema hawawezi kupitisha bajeti ya wizara ikasimamiwe na waziri mtuhumiwa. Nadhani ni mkakati mzuri pia. Sijui wabunge wakigoma kabisa kupitisha bajeti ya wizara nini kinatokea. Bunge lote linavunjwa? Original source: Mwananchi
 
Back
Top Bottom