UWAJIBIKAJI: Albert Msando ajiuzulu nafasi ya Ushauri wa Chama cha ACT-Wazalendo

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Kwa Kiongozi Mkuu wa Chama,

YAH: KUJIUZULU NAFASI YANGU YA MSHAURI MKUU WA CHAMA.
Napenda kuchukua nafasi hii kukujulisha uamuzi wangu wa kujiuzulu nafasi yangu kama Mshauri Mkuu wa Chama. Uamuzi huu ni kutimiza hitaji langu la kuishi kama mfano kwa jamii inayonizunguka. Kama kiongozi nastahili kuwajibika kutokana na video clip iliyorekodiwa na kusambazwa. Ni wajibu wangu kwa chama changu na nchi yangu kuwajibika kama kiongozi.

Nitaendelea kuwa mwanachama mtiifu nikishirikiana nawe kujenga chama na kuhakikisha nchi yetu inaendelea mbele. Nakushukuru kwa kuniamini kwa kipindi chote tulichofanya kazi pamoja.
Wako
Albert G. Msando

Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Chama chetu cha ACT Wazalendo.

Ndugu Msando anawajibika Kwani anapaswa, nanukuu "kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka".

Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama. Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kuzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama.

Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake.

Ndugu Msando Alberto ameomba msamaha Kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Dar es salaam
Mei 23, 2017
 

Attachments

  • SABABU KUU YA WAKILI MSANDO KUJIUZURU UONGOZI WA CHAMA.mp4
    1.5 MB
Hahaha.. Kazi kwel kweli...

Sidhani Kama kulikuwa Na haja ya kudindia jambo dogo la kawaida kabisa katika jamii yetu....

Jesus once said "and the one without sin be the first to cast the stone"...,

Bad things happen to everybody, I'm sorry ...
I believe that Msando will bounce back....
 
Back
Top Bottom