Uvuvi na Biashara ya Sangara chini ya 50cm

Uvuvi na Biashara ya Sangara chini ya 50cm

Radical-1

New Member
Joined
May 31, 2023
Posts
2
Reaction score
4
Hili jambo nimekuwa nikijiuliza na sijawahi kupata ufumbuzi..
Naombeni msaada wadau.

Ni kosa kisheria kuvua, kusafirisha na kuuza sangara (Nile Perch) wa ziwa Victoria wenye urefu chini ya sentimita 50.
Screenshot_20250319-173544_1.jpg

Hii nimeitoa kwenye kanuni za uvuvi 2009.

KINACHONITATIZA NI HIKI HAPA:
Wavuvi wanatakiwa wafanye nini ili wasiwakamate Sangara hao kwenye nyavu zao?
Kwa mfano wavuvi wa dagaa ziwa Victoria hutumia taa(mwanga) kuvua. Na Sangara hufuata mwanga ili kula hao dagaa waliokusanyika kwenye taa za wavuvi.
Pindi wavuvi watakapotumia nyavu halali (mm 10) kwajili ya uvuvi wa dagaa hujipatia pia Sangara wa size tofauti tofauti.
Wakati mwingine hadi Sangara wenye 3cm yaani vitoto kabisa.
Je wawafanye nini hao Sangara wakijinchnganya kwenye nyavu za dagaa?

Ukisema wawarudishe ziwani Sangara hao wachanga hakuna mvuvi atakuelewa kwasababu uvuvi wao unahitaji kufanyika haraka haraka, basi wanapata wapi muda wa kuchambua watoto wa Sangara wawarudishe ndani ya maji?
(Nazungumza haya yote kwasababu nimewahi kuvua dagaa kwa muda zaidi ya miezi 9 mwaka 2023)

Na kawaida tulikuwa hatuwachambui sangara waliochini ya cm 50 ili kuwarudisha majini.
Na hata kama ukisema ufanye hivyo, utakuwa haujasaidia kitu, maana Sangara ni wachovu sana kuliko samaki kama Kambare..
Kitendo cha kumbwaga Sangara kwenye mtumbwi, kisha umrudishe majini tena kuna uwezekano mdogo wa kuendelea kuishi kama awali

Na kwa kuwa wavuvi hawatupi Sangara waliozuiliwa kuvuliwa je wafanya biashara huku nchi kavu wafanye nini?

Nimetembea sehemu nyingi Mkoan Mwanza ambazo wavuvi wa dagaa huuza dagaa wao pamoja na Sangara waliojichanganya kwenye nyavu za dagaa, lakini sijaona watu wa mamlaka yoyote wakiwazuia wavuvi hao kwa kuja nchi kavu na watoto wa sangara.

Sasa kama wavuvi hawazuiliwi kuleta watoto wa Sangara nchi kavu, kwanini wanunuzi na wasafirishaji wazuiliwe kuuza ama kusafirisha?

Na je kama Watanzania wazalendo tuwafanye nini Sangara wachanga ambao wameshafika nchi kavu ama sokoni au nyumbani, au wapo mezani tayari kwa kuliwa
 
Kuwepo kwa mashamba ya bamgi msituni ama polini hakufanyi uuzaji wa bange uwe halali. Wewe umefanya uvuvi juzi ila mimi nimefanya uvuvi siku nyingi sana. Samaki anatafutwa kutokana na ubora wa soko. Hao samaki wachanga wasiponunuliwa tu hakuna mvuvi atakayewaleta
 
Mchango wako una point sana.lakini bado swali linabaki hapohapo mkuu wavuvi wafanyeje ili wasiwavue hao watoto (vifaranga) wa sangara?

Mimi nimevua mwaka 2009 Alichosema Ni kweli kabisa hata mimi nimewahi kujiuliza maswali hayo.
Binafisi niliona tunapoteza sangara wengi sana kwa kuwauza kama fulu ni mamilioni ya sangala hufa kila siku kiasi kwamba wakiachwa kwa mwezi tu na ukuaji wake ule wa kasi ziwa victoria lingebaki na samaki wengi sana.
 
M

Mbinu pekee ambayo itainusuru sangara ni kufanya utafiti wa mwanga katika taa za kuvulia dagaa. Pia wafanye utafiti wa miezi (majira) ambayo sangara hatumii dagaa kwa wingi kama chakula kisha hiyo miezi ndo ihalalishwe kwa uvuvi wa dagaa. Kuna kitu ambacho kwa utafiti wangu nimekigundua. Kama taa ya kuvulia dagaa itaongezwa ukali wa mwanga kutakuwa na upungufu wa sangara wachanga kuzolewa na kokolo la daga
 
Ni sawa lakini mwanga mkali ni hatari pia kwa wavuvi mkuu
 
Back
Top Bottom