Uvutaji wa sigara kwa wingi una madhara ktk mbegu za kiume | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uvutaji wa sigara kwa wingi una madhara ktk mbegu za kiume

Discussion in 'JF Doctor' started by MR. ABLE, Aug 4, 2012.

 1. MR. ABLE

  MR. ABLE JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,476
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  KUMEKUA NA ONGEZEKO KUBWA LA KUZALIWA KWA WATOTO WENGI WA KIKE KULIKO WAKIUME. MOJA SABABU AMBAZO HAZIJATHITISHWA NA WATAALAMU NI KWAMBA, WANAUME WAVUTAO SIGARA KWA WINGI NI VIGUMU KWAO KUPATA MTOTO WA KIUME. SABABU YA PILI NI UMRI KATI YA MUME NA MKE, KWAMBA MUME ANAPOKUWA NA UMRI MDOGO KULIKO MKE AU WANALINGANA UMRI BASI KUPATA MTOTO WA KIUME NI SHIDA KWAO. Nami naamini hizo sababu kwa kuwa ninajirani yangu ni mvuta sigara mkubwa na ana watoto 4 wote wa kike na amekuwa akitafuta wa kike ila ameshidwa. kwa suala la umri pia naamini kwa kuangalia ktk ukoo wangu, KWAMBA; BABA YAKE BABU YANGU ALIMZIDI MKE WAKE MIAKA 12 NA WAKAPATA WATOTO 7, WAKIUME 6 NA WAKIKE 1, BABU YANGU MZAA BABA NAYE AMEMZIDI BIBI KWA MIAKA 20, NAO WAMEPATA WATOTO 7 WAKIUME 6 WA KIKE 1. BABA YANGU AMEMZIDI MAMA KWA MIAKA 10 TUMEZALIWA WATOTO 3 NA WOTE WA KIUME. MIMI MWENYEWE KTK HARAKATI ZA USHAROBARO, NINA WATOTO 2 WA MAMA TOFAUTI NA WOTE NI WAKIUME. NA SISI SOTE KTK UKOO WETU HAKUNA ANAYEVUTA SIGARA. HEBU NAWE NIAMBIE KTK UTAFITI WAKO KWA WATU UNAOWAFAHAMU JE HILI SUALA LINA UKWELI NDANI YAKE?
   
 2. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nishaisikia hiyo, shostito wangu kabahatika kamoja, maana mume ni chain smoker kaharibu mayai yote
   
 3. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Mr ebo, mr able? Kafufuka! Huo utafiti unaoonesha watoto wa kike kuzaliwa wengi kuliko wa kiume umefanyikia jamii ipi? Leta data zilizo na uhakika tujadili,
   
 4. joellincoln

  joellincoln Senior Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Fallacy! Tupe prove si kuleta data za ukoo wenu tu hapa! Kumbuka unaongelea dunia na tanzania kwa ujumla. Anyway mi rafiki yangu anavuta balaa tena sports na ana watoto watatu wote wa kiume anahangaika apate angalau wa kike sasa na shemeji naona kimeshaita,, yetu macho usikute ni kidume tena so hiyo si kweli. Nachojua na kuamini ni kuwa wanaovuta sana sigara mara nyingi au baada ya muda fulani effect za sigara huathiri mpaka sperm counts so mtu kama huyu anajikuta ana mbegu so weak kiasi kwamba anaweza asipate mtoto. Huyo jirani yako anayevuta na ana watoto wanne wa kike ana uhakika wote ni wake? Kumbuka kuna kusaidiwa mama akakausha hahaah! Chezea Wabongo!
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mh sidhani... Kuna watu wana watoto wa kike lakini si wavutaji na mifano iko mingi tuu
   
 6. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Mambo mengine bwana! Mimi natafuta mtoto wa Kike miaka minne sasa bila mafanikio itabidi nianze kupuliza kumbe
   
 7. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu kama hicho,nguvu za kiume maana yake ni kuweza kufanya tendo wakati unaitaji....Kupata mtoto aliusiani na nguvu za kiume unaweza ukawa na upungufu wa nguvu za kiume na ukapata mtto wa kiume!! Kuna mdingi anavuta sigara kinomaa anawatoto 7 wote wa kiume!!!
   
Loading...