Uvutaji Sigara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uvutaji Sigara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mahmood, Apr 10, 2013.

 1. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2013
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,829
  Likes Received: 1,323
  Trophy Points: 280
  Imeandikwa na: Mama yake Nasra

  Uvutaji wa sigara umeenea na kushamiri dunia nzima licha ya kuwa madhara yake yapo wazi. Baadhi ya Waislamu wametumbukia katika balaa hili na kuziathiri nyumba zao bila ya kujijua. Kuna sababu tosha zenye kuonyesha uharamu wa jambo hili kwa Muislamu. Sigara ina athari sana katika dini, afya, mazingira, familia, rasilimali na mengineyo.

  i. MADHARA KATIKA DINI

  Sigara inaathiri ibada ya mja na inapunguza malipo ya ibada hiyo. Kwa mfano ibada ya sala ambayo ni nguzo muhimu ya Muislamu; Kutokana na hadithi iliyosimuliwa na wengi; Amesema Mtume Swalla Llahu Alayhi wa Ssalam

  "Mwenye kula Kitungu maji au thawm, basi asiukaribie Msikiti wetu na akae nyumbani"
  [Bukhari na Muslim]

  Tunaona makatazo yamekuja kutokana na harufu mbaya inayotokana na vitu hivyo amabayo huwakirihisha watu pamoja na Malaika katika nyumba za Allaah (Misikitini).

  Bila ya shaka mdomo wa mvutaji sigara una harufu mbaya zaidi kuliko vitunguu, ima huwakera watu na Malaika kwa harufu hiyo au kukosa fadhila za sala ya jamaa msikitini kwa mwanamme.

  i. MADHARA KATIKA MWILI

  Hakuna anaepinga madhara ya sigara katika mwili wa binadam. Utafiti wa kiafya umeyaona haya na kuyaeleza kwa kina; hata imekuwa ni sheria kuweka wazi maandishi ya tahadhari kwa kila paketi la sigara angalau watu wazinduke.

  Ndani ya sigara hupatikana kemikali zenye sumu kama vile nicotine, arsenic, carbon monoxide na vyenginevyo ambavyo mvutaji huathirika kidogo kidogo hadi kuua sehemu muhimu za mwili wake. Athari za zake ni kubwa na ni nyingi; husababisha cancer, TB, mshituko wa moyo, pumu, ubovu wa meno, na huwa ni chimbuko la maradhi mengi mengineyo.

  Allaah Alietukuka anatuonya tusiwe wenyenye kujidhuru. Suuratu Nnisaa':29

  وَلَا تَقۡتُلُوٓاْ أَنفُسَكُمۡ-ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِكُمۡ رَحِيمً۬ا

  Wala msijiue, hakika Allah ni mwenye kukurehemuni

  Pia katika Suuratul Baqarah:195

  وَلَا تُلۡقُواْ بِأَيۡدِيكُمۡ إِلَى ٱلتَّہۡلُكَةِ

  Wala msjiitie kwa mikono yenu katika maangamizo

  Na Mtume Swalla Allahu ‘Alayhi Wasallam anasema katika Hadithi:

  " لا ضرر ولا ضرار "

  Kusiwe na kudhuriana wala kulipa dhara.


  ii. ATHARI KWA AKILI NA MATAMANIO

  Sigara huathiri akili ya mwanadamu kwa kiasi kikubwa. Mvutaji mzoefu anapoikosa huwa vigumu kwake kufikiri kitu, kutatua tatizo au kuwa makini katika jambo mpaka aipate. Badala kuwa mtumwa wa Mola wake, hugeuka na kuwa mateka wa sigara yake na kuifanya dhaifu akili na hisia zake.

  Allah Subhaanahu wa Ta'ala anatueleza katika Suuratu An-Nisaa':27

  وَٱللَّهُ يُرِيدُ أَن يَتُوبَ عَلَيۡڪُمۡ وَيُرِيدُ ٱلَّذِينَ يَتَّبِعُونَ ٱلشَّہَوَٲتِ أَن تَمِيلُواْ مَيۡلاً عَظِيمً۬ا

  Allah anataka kukukhafifishieni. Lakini wanaofuata matamanio yao wanataka mkengeuke mkengeuko mkubwa

  iii. MADHARA KATIKA MALI

  Mvutaji sigara hupoteza pesa nyingi karibu kila siku kununulia sigara isiyomletea tija yeyote bali ni kuwafaidisha hao wanaoendesha bishara hii haramu. Kumbuka kuwa mali tunayoipata tutakuja kuulizwa kwa njia gani tumeichuma na vipi tumeitumia.

  Katika Suurat An-nisaa':5 Allah Subhaanahu Wata'ala anatueleza:

  وَلَا تُؤۡتُواْ ٱلسُّفَهَآءَ أَمۡوَٲلَكُمُ ٱلَّتِى جَعَلَ ٱللَّهُ لَكُمۡ قِيَـٰمً۬اوَٱرۡزُقُوهُمۡ فِيہَا

  Wala msiwape wapumbavu mali zenu ambazo Allah amezijaalia kwa maisha yenu
  Pia katika Suuratul Israa:26 – 27

  وَلَا تُبَذِّرۡ تَبۡذِيرًا إِنَّ ٱلۡمُبَذِّرِينَ كَانُوٓاْ إِخۡوَٲنَ ٱلشَّيَـٰطِينِ-ۖ

  Wala usitawanye (mali yako) kwa ubadhirifu. Hakika watumiao kwa ubadhirifu ni ndugu wa mashetani

  Na kutoka kwa Mtume Swalla Allahu ‘Alayhi Wasallam anasema:

  " إن الله ينهاكم عن قيل وقال ، وكثرة السؤال وإضاعة المال

  Hakika Allah anakukatazeni na mazungumzo yasiyokuwa na faida (huyu kasema au kimesemwa) na kukithirisha kuuliza masuali na kupoteza mali
  .
  Licha ya nchi za Magharibi kutoa indhaari tu katika paketi kuonesha madhara ya sigara, Maulamaa wa kiislamu takriban wote wamekubaliana kwamba sigara ni haraam. Angalia Fatwa ifuatayo kutoka katika Fataawa Islaamiyah 442/3

  Kuvuta sigara ni haraam kwa sababu ya kuleta madhara mengi wakati Allah Subhaanahu Wata'ala amehalalisha kwa waja wake vyote vilivyo vizuri katika vyakula na vinywa na akaharamisha vibaya vyao. Na aina zote za uvutaji ni miongoni mwa vitu vibaya kwa sababu ya kuleta madhara na kulewesha.

  Ni vyema kutanabahi ndugu Muislamu na kuachana na mazoea sugu na potofu ya kuvuta sigara. Mvutaji sigara huwa hajali kuvuta mbele ya wale waliomzunguka ndani ya nyumba yake, kama mkewe/mumewe, watoto na wengineo. Huwasababishia kuvuta moshi wa sumu na wale walio karibu nae. Huleta hali mbaya hasa kwa mazingira ya ndani ya nyumba na ni mfano mbaya kwa kile kinachochungwa (mke na watoto) ndani ya nyumba hiyo.

  Ndugu yangu Muislamu , kama ni miongoni mwa wenye kuendeleza uovu huu basi rudi kwa Mola wako kwa moyo ulio mwepesi wenye kusikiliza nasaha na kukubali yale yote yanayotoka kwa Mola kwa ajili ya kuinusuru nafsi yako kwanza, kisha dini yako, kisha akili yako, kisha familia yako, kisha mali yako na kadhalika.


   
 2. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2013
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 29,338
  Likes Received: 8,475
  Trophy Points: 280
  Haya...
   
 3. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2013
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,829
  Likes Received: 1,323
  Trophy Points: 280
  Thank you.
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2013
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,610
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Eheee......................!:rockon:
   
 5. mahirtwahir

  mahirtwahir JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2013
  Joined: Jan 12, 2013
  Messages: 447
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Yaaani umeongea sawa ishaalkah mungu akujaalie kila la kheri
   
 6. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2013
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,010
  Likes Received: 2,790
  Trophy Points: 280
  mama yake Nasra ni nani.......?
   
 7. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2013
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,829
  Likes Received: 1,323
  Trophy Points: 280
  Mama Wa Nasra (The Mother Of Nasra)
   
 8. m

  matubara JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2013
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Smoking is a basic human right!
   
 9. V

  Vivax JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 353
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Vizuri! Tuambie kuhusu muislam kumloga mwenzake
   
 10. Home First

  Home First JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2013
  Joined: Feb 23, 2013
  Messages: 476
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Ugoro, je?
   
 11. M

  MWENDAKULIMA JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2013
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 961
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Simfahamu. Ni mtu maarufu hapa Darisalama?
   
 12. V

  Vivax JF-Expert Member

  #12
  Apr 10, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 353
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Enzi hizo potsman zilikuwepo?
  Jaribu kasema yalitoka kinywani mwa mtume(saw)
   
 13. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2013
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,829
  Likes Received: 1,323
  Trophy Points: 280
  Haishi Darisalama.
   
 14. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #14
  Apr 11, 2013
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,829
  Likes Received: 1,323
  Trophy Points: 280
  Ni haramu kwa Muislam kumloga mtu.
   
 15. J

  John W. Mlacha Verified User

  #15
  Apr 11, 2013
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 538
  Trophy Points: 280
  Cheafaya
   
 16. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #16
  Apr 11, 2013
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,796
  Likes Received: 171
  Trophy Points: 160
  Namna ya kuacha je?
   
 17. Nyanidume

  Nyanidume JF-Expert Member

  #17
  Apr 11, 2013
  Joined: Oct 24, 2012
  Messages: 2,130
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Kamuulize aliyekufundisha kuvuta sigara!
   
 18. john tongo

  john tongo JF-Expert Member

  #18
  Apr 11, 2013
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hujajibu bado
   
 19. john tongo

  john tongo JF-Expert Member

  #19
  Apr 11, 2013
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wanafunzi wa siku hizi wanauita 'memory card'
   
 20. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Apr 11, 2013
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 30,642
  Likes Received: 33,837
  Trophy Points: 280
  Kama wavuta sigara mnapenda sana sigara basi nawashauri muwe mnavuta moshi wote uishie huko tumboni msipulize nje hata tone moja ili mfaidi vizuri.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
Loading...