gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,274
- 20,673
habari za ijumaa wana MMU.
Leo nimekuja na hii mada hapa iitwayo uvumilivu hasa katika maisha ya ndoa. Mara nyingi sana nimekuwa nikisema ndoa yahitaj uvumilivu lakin sidhani kama naeleweka ipasavyo juu ya hili neno.
wataalamu wa lugha watanisaidia kuidefine vizuri bali mimi naomba nieleze nguvu ya uvumilivu panapo mapenzi ya kweli.
Jamani kwanza naomba mnielewe kwamba kwenye mapenzi ya dhati uvumilivu hutangulia, na hii hutokana na ukweli kwamba upendo huvumilia. Panapo upendo ule usiosukumwa na mambo ya nje bali ule wenye msukumo wa ndani tu uvumilivu hutangulia na hii ni kwasababu kuu mbili nazo ni:-
1) uvumilivu huona mapungufu ya mwenza wako kama changamoto wala si kama chuki.
2)uvumilivu hauhesabu gharama za kazi,upendo,kujitolea ama hela.
kwasababu hizi mbili siku zote mimi huwa naishi kwa kuvumilia mbele upendo ukafuata nyuma. na hii ni kwasababu ninapenda kwa dhati na wala si kwababu ya msukumo wa vitu ama kitu.
naona niifupishie hapa nisiwachoshe kwa maneno mengi mkashindwa kudadavua. nakaribisha maswali na maelezo ya nyongeza.