Habari zenu Wakuu.
Kwenye pitapita zangu JF nikakuta na Uzi kuna dada analalamika kuwa Uchumba na mume mtarajiwa kuelekea ndoa unakizuizi cha Dhehebu la Dini.
Aisee! Ukiusoma ule uzi utaona ni jinsi gani yule dada anampenda mume mtarajiwa lakini imani ndio huenda ikafanya wakavunja uchumba, maana jamaa kakataa kabisa kubadili dhehebu lake na dada kagoma japo katoa option ya ndoa ya serikali ambayo ilikataliwa na jamaa.
Nikiangalia hii inshu inanifanya nijiulize maswali mengi ambayo siwezi kujijibu, maswali yenyewe ni haya yafuatayo;
1) Itakuaje kama huyu dada akiolewa na mtu mwengine wa dhehebu lake na ilhali bado anampenda jamaa alievunja nae uchumba kwasababu ya Dini?
2) Huyu dada atakuwa na upendo wa kweli kwa jamaa atakae muoa ambae yupo dhehebu moja?
3) Wenza wapya wataooana nao ikitokea wanakasoro, je watajilaumu kuachana kwao?
4) Ndoa zao mpya baada ya kuvunja uchumba zitakuwa na muunganiko wa upendo au ndio ni bora liende tu?
Ushauri wangu
Vijana wenzangu kabla hamjapendana hakikisheni mnaongea future zenu mapema ili kuepusha kupotezeana Muda na kuvunja Uchumba.
NB: Kwa maelezo ya dada ni kwamba wamedumu kwenye uchumba kwa miaka 6.