Uvumilivu kwenye ndoa

Uvumilivu kwenye ndoa

Aurora

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2014
Posts
7,308
Reaction score
5,275
Habari zenu.

Mara nyingi wanandoa huambiwa au hushauriwa swala zima la UVUMILIVU huenda ikawa kabla ya kuingia kwenye ndoa au hata baada ya kuingia kwenye ndoa.

Lakini nimeona kama watu hawa wenye busara zao kama wazee/wazazi au viongozi wa dini huwa hawasemi huu UVUMILIVU UWE TO WHAT EXTENT.

Mfano unakuta mwanamke anapigwa na mumewe au mwanaume anapigwa na mkewe lakini akienda kwa viongozi wa dini au wazee/wazazi wanamwambia avumilie tu ndio ndoa zilivyo.

Ndipo nilipopata hili swali HUU UVUMILIVU HAUNA KIKOMO humu ndani najua kuna watu wenye busara na hekima najua tutapata cha kujifunza.

Ni hayo tu.

KARIBUNI.
 
Hakuna kiongozi wa imani anayetoa nasaha kwa mwanandoa anayeumia kuwa na uvumilivu hususani linapokuja suala lolote ambalo ni tatizo ndani ya ndoa...

La hasha, endapo kutakuwa na matumizi ya neno 'vumilia' basi ujue ni katika harakati za kupata usuluishi...

Hivyo basi mtu huambiwa avumili kwa mantiki kuwa uvumilivu na usubiri suluhisho la kadhia inayoendelea...
 
Habari zenu,

KARIBUNI..........

Kikomo cha uvumilivu ni pale utakapo tokwa na uhai, lakini " UVUMILIVU HAUNA MIPAKA, MIPAKA HULETWA NA MAADUI WA UVUMILIVU" . Na ili uitwe uvumilivu ni lazima iwe kwenye mambo magumu na mazito
 
Kwani haujui mvumilivu hula mbivu???
 
Ni kweli ndoa ni pamoja na uvumilivu lakini hizi ndoa za sasa inafikia kipindi unaona maji ya shingo na hiyo inaweza sababishwa na mke/mume au hata wazazi wa mke/mume.

Kwa kweli ndoa sio jambo rahisi kama tunavyofikiria
 
Kikomo cha uvumilivu ni pale utakapo tokwa na uhai, lakini " UVUMILIVU HAUNA MIPAKA, MIPAKA HULETWA NA MAADUI WA UVUMILIVU" . Na ili uitwe uvumilivu ni lazima iwe kwenye mambo magumu na mazito

Kumbuka katika kila jambo unatakiwa uwe na kiasi
 
kwa upande wangu kuna mambo ya kuvumilia lakini kipigo sio mojawapo.....
 
  • Thanks
Reactions: lin
Hakuna kiongozi wa imani anayetoa nasaha kwa mwanandoa anayeumia kuwa na uvumilivu hususani linapokuja suala lolote ambalo ni tatizo ndani ya ndoa...

La hasha, endapo kutakuwa na matumizi ya neno 'vumilia' basi ujue ni katika harakati za kupata usuluishi...

Hivyo basi mtu huambiwa avumili kwa mantiki kuwa uvumilivu na usubiri suluhisho la kadhia inayoendelea...

tena hao ndio waguma kukubali ndoa ivunjike wanakwambia vumilia hadi kifo kitakapowatenganisha
 
Kikomo cha uvumilivu ni pale utakapo tokwa na uhai, lakini " UVUMILIVU HAUNA MIPAKA, MIPAKA HULETWA NA MAADUI WA UVUMILIVU" . Na ili uitwe uvumilivu ni lazima iwe kwenye mambo magumu na mazito

kwa hiyo as long as uko kwenye ndoa hata kuwe na tatizo linalohatarisha maisha yako lazima uvumilie?
 
Watu watakwambia vumilia kwa kuogopa lawama tu...Wengine deep down wanataka usivumilie
 
Back
Top Bottom