MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,784
Wasalaam,
Leo BBC wametangaza matokeo ya utafiti uliofanywa na wanasayansi na wanahistoria wa Uingereza kwenye baadhi ya miili ya binadamu ambayo ina miaka zaidi ya 10,000 kwenye visiwa hivyo. Professor Chris Stringer amesema amesema amemsoma huyo mtu ambaye walimpa jina "Chedar Man" kwa zaidi ya miaka 40 mfululizo.
Mwili huo waliupata mwaka 1903 kwenye pango na wanasayansi wakajaribu kutafuta DNA kama watapata na kweli walifanikiwa kukuta zilizobakia. Walichokikuta humo ndani kimewashangaza kwamba mtu yule mwenye asili ya pale alikuwa na nywele nyeusi, macho ya rangi bluu na ngozi nyeusi.
Wamesema huu utafiti umepingana kabisa na zile nadharia za kisayansi hasahasa Evolution ambazo wengi tumeziamini kwa muda mrefu kwamba Mazingira ndiyo yanafanya watu wawe weusi na weupe. Wao wamesema kwamba mtu huyu aliishia kipindi ambacho kilikuwa ni cha baridi sanaa, hivyo basi kama hakuwa mweupe kuna uwezekano kwamba mazingira hayana madhara yoyote.
Amekiri na kusema kwamba hii dhana ya Wazungu weupe imekuja zama hizi zetu,
Hivyo walivyomtengeneza yule mtu kutokana na sifa za DNA wakapata sura ya mtu kama ilivyo hapa chini.
MY TAKE: Huu utafiti haujapokelewa vizuri sana na wazungu maana mpaka sasa wanatukana sana wakisema hii ni agenda ya kufanya Historical Revisionism: Wanaweza wakawa wana hoja kubwa kama kweli huu utafiti utakuwa tu umepikwa. Kwasababu kuna watu hadi leo hii wanaamini kwamba Wayahudi hawakuuliwa na Wanazi na hadi wengine wamediriki kusema kwamba yale mauji ya Rwanda hayakuwa ya halaiki.
Lakini tusikosee hata kidogo,
Kama wanasayansi wamethibitisha hili jambo basi tunaomba hoja zijibu hoja.
Binafsi nimefurahishwa sana, siyo kwasababu Waafrika ndiyo walikuwa wa kwanza huko Barani Ulaya: Lah, hasha bali kwasababu Ukweli ambao dunia ilijaribu kuuficha kwa ajili ya manufaa ya kundi fulani fulani linalokandamiza watu weusi unaanza kutoka.
Mungu alivyomuumba kila mwanadamu,
Mzungu, Mwafrika, Mwarabu na Mchina alikuwa na makusudi yake.
Wala hakuna jamii yenye maana sana kuliko nyenzake: Leo hii maendeleo haya tuliyonayo ni juhudi za kila jamii iliyopo hapa chini ya jua. Ndiyo maana huwa nasema kwamba tunaweza kuwa na historia yetu kama Waafrika, lakini kwa ujumla HISTORY IS A COMMON HERITAGE TO MANKIND. Mwisho wa siku tutakuja kujua kwamba wote tumetokea sehemu moja na yanayotuunganisha ni mengi kuliko yanayotugawanya. WHITE-WASHING of human history was a very major crime against humanity.
NB: Ukimsoma mwanahistoria wa Kigiriki wa karne nyingi zilizopita Herodotus anasema alisafiri kwenda Ulaya maeneo ya Vilima vya Kaukasia (Caucasian Mountains), ambapo kando kando ya mito alikutana na watu weusi ambao walikuwa ni wakazi wa pale. Neno alilolitumia kuwaelezea hawa watu ni Ethiopians ambalo lina maana kwamba "aitho"- Ulioungua na "ops" -Uso. Hivyo watu wenye nyuso zilizoungua ambalo pia alilitumia kuwaelezea sana watu wa Misri ya Zamani kipindi hicho inaitwa Kemet......(Leo hii wasomi wanasema Wamisri walikuwa ni waarabu)
Hiki chanzo cha Herodotus kilipingwa sana kwamba ni "Unreliable" and "Unverified" kama yalivyo matukio ya kwenye Biblia na Quran. Japo sasa leo tumepata Blue-Print kwamba wazazi wa hawa wazungu walikuwa ni weusi na Bara la Ulaya lilikaliwa na watu weusi.
ANGALIZO:
Hili bandiko halina dhumni la kuchochea mjadala wa Ubaguzi wa rangi,
Dhana nzima ni kusema kwamba kuna madhara makubwa sana ya kutaka kufukia ukweli.
Pia, kuna madhara makubwa sana ya jamii moja kuwabagua jamii ya pili kutokana na rangi au maumbile. Haya sasa Wahenga wao walikuwa weusi tiii.....(Wonders shall never cease)
CHANZO CHA HII HABARI:
1. First modern Brits were black, groundbreaking DNA test on 10,000-year-old fossil reveals
CC: ISIS , zitto junior , Consigliere , UmkhontoweSizwe , Red Giant , Safari_ni_Safari , Fantasia , Da'Vinci , neo1 , Bukyanagandi , mng'ato