Uvujaji wa aina hii ni kero | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uvujaji wa aina hii ni kero

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mchapa shughuli, Jun 4, 2011.

 1. mchapa shughuli

  mchapa shughuli JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 529
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 80
  Habari wanaJF,
  Kuna tabia nimekua nikiendelea kuiona ya madereva wa magari ya serikali ku-misuse viyoyozi vya magari hayo.Jana nikiwa maeneo ya posta nilushuhudia gari STK 3620 VX likitumia kiyoyozi kwa muda wa saa 2 bila kuzimwa huku bosi akiwa gorofani kwenye kikao na kumwacha dereva akitumia kiyoyozi hicho sehemu ya maegesho ya gari bila kujali uharibifu wa mafuta na gharama yake kwa sasa.Hii ni mara ya tisa sasa nikiona ubadhirifu wa aina hii kwa magari ya serikalini.
   
 2. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mali ya umma! Hutakiwi kuwa na uchungu nayo!
   
 3. i411

  i411 JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Ndo bongo yetu hiyo unakula na kujivinjari unapofanya kazi
   
 4. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Malalamiko mengine bwana? sasa dereva amebaki kwenye gari na joto la posta lile unataka azime AC aendelee kuvuja jasho bila sababu? Kama ni hivyo basi mabosi nao wawaambie kabisa madereva wao muda watakaoutumia kwenye vikao, ili madereva waende wakatafute mahali pa kupumzika wakati wanasubiri mabosi wao wamalize vikao. Hata kama mimi ndo ningekuwa dereva wala nisingekubali kuumia na joto wakati AC ipo. Yaani nyie mmeona la AC tu kuliko mamilioni ambayo watu wanalipana bila kufanya kazi?
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hivi hii tabia ya kutafuta kutukanwa kwangu inasababishwa na nini..
   
 6. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kula kwa urefu wa kamba yako
   
 7. Mjanga

  Mjanga JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 1,246
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  mkuu hiyo mbona cha mtoto, sehemu nyingine wananyonya na mafuta wanauza, kwa kanda ya Ziwa hili ni maaerufu kama KUPIGA NYOKA! WALA USISHANGAEV BANA!:dance::dance::dance:
   
 8. mchapa shughuli

  mchapa shughuli JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 529
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 80
  Haya aisee kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake ila tusilalamikie ufisadi wowote yaonesha hizi ndio tabia zetu,tukiwa hatuna kitu tunalalamika mno ila tukipata rungu tunasahau ni ubadhirifu tu..
   
 9. F

  Fenento JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu unashosema ni kweli, kwavile wanajua ile bajeti ya OC (Other charges) bado ipo na wanachofanya ni kuhakikisha wanaitumbua vilivyo. Cha ajabu ni kwamba mabosi wanaandaa mikakati ya kuweka kwenye makabrasha na siku ya siku watakuambia fedha ya utekelezaji haipo. Hii ndo tanzania ambayo mibango mingi sana lakini utekelezaji ni ziro.
   
 10. F

  Fenento JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu unashosema ni kweli, kwavile wanajua ile bajeti ya OC (Other charges) bado ipo na wanachofanya ni kuhakikisha wanaitumbua vilivyo. Cha ajabu ni kwamba mabosi wanaandaa mikakati ya kuweka kwenye makabrasha na siku ya siku watakuambia fedha ya utekelezaji haipo. Hii ndo tanzania ambayo mibango mingi sana lakini utekelezaji ni ziro.
   
 11. F

  Fenento JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu unashosema ni kweli, kwavile wanajua ile bajeti ya OC (Other charges) bado ipo na wanachofanya ni kuhakikisha wanaitumbua vilivyo. Cha ajabu ni kwamba mabosi wanaandaa mikakati ya kuweka kwenye makabrasha na siku ya siku watakuambia fedha ya utekelezaji haipo. Hii ndo tanzania ambayo mibango mingi sana lakini utekelezaji ni ziro.
   
 12. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  hivi lile tangazo la redio tanzania bado lipo?
  "wee acha kudokoa mali ya umma"
   
 13. mchapa shughuli

  mchapa shughuli JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 529
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 80
  Kweli hizo OC zingebanwa na kiasi kingine kiende mambo muhimu halafu tungeona hayo mafuta ya kuchezea wangetoa wapi..
   
 14. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Mleta mada uko sahìhi kabisa,yani tumeacha kodi yetu ipotee kihuni. Yani uwa napita pale mbele ya national audit opposite kuna wizara pale,kuna stk zaidi ya 7 hukaa pale na gari ya waziri na naibu waziri. Cha ajabu eti kama lisaa kabla ya bosi kutoka ofsini gari huwa tayari imewashwa! Ina maana hawa madereva hawana mawasiliano kujua anashuka ghorofani baada ya mda gani? Juzi tu nliona gari ya Mwakyembe hapo hapo ikimsubiri,nkaenda kitega uchumi nkamaliza kilichonipeleka,nkarudi pale nbc baharini,alaf wakati narudi ndo nkakutana na gari imeshambeba pale ppf towers,sasa fikiri muda gari ilivyokuwa on!! Acha wakati bosi anasubiriwa ok. Sasa nenda pale wanakopenda kula madereva wa serikali yan magenge yaliyopo ohio kuanzia pale SouthernSun Hotel,zaman holiday inn mpaka karibu ocean road mida ya mchana utakuta madereva wanakula kiyoyozi wakimsubiri mtu akila,na aibu wengine wanamabinti wa ifm kwenye viyoyozi pale baharini. Sina wivu ila roho inauma kwa misuse ya mafuta yetu!
   
 15. mchapa shughuli

  mchapa shughuli JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 529
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 80
  lakini mbona zamani hii tabia haikuwepo na AC ndani ya gari za serikali zilikuwepo au ndio utandawazi umechangia..
   
 16. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2011
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  ashuke asome magazeti na gari izimwe

  huu ujinga mwingine bana... Wangekopeshwa hayo magari halafu uone kama wangekua wanakuja nayo mjini
   
 17. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,759
  Trophy Points: 280
  is it uvujaji or ufujaji?refer your heading
   
 18. mchapa shughuli

  mchapa shughuli JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 529
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 80
  we unaonaje..
   
 19. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,759
  Trophy Points: 280
  ufujaji! bana if im not mistaken
   
 20. mchapa shughuli

  mchapa shughuli JF-Expert Member

  #20
  Jun 5, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 529
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 80
  Uko sawa,lakini uvujaji pia imetoka kwenye neno kuvuja yaani kupotea mfano kimiminika kinapovuja toka mahali..
   
Loading...