It is more complicated than that. Kama kila mtu akiwa najitangazia matokeo kungekuwa na chaos kubwa sana. Tunakumbuka kuwa DTV wamewahi kutangaza matokeo ya sahihi ya uchaguzi Zanzibar, lakini baada ya kuchakachua yakabadilika na matokeo wengi tunakumbuka. No matter what CHADEMA wangefanya mpango wa kuchakachua ulikuwa umewekwa long before eclections. Tunaweza kuwalalamikia kwa kutolinda haki yetu, yaanai hawakufanya kazi vizuri kulinda kura tulizowapigia, na sisi wenyewe hatukufanya kazi nzuri vya kutosha.
Lakini still CHADEMA imefanya vizuri kuliko tunavyosema, hakika tungependa ifanye vizuri zaidi ya hapo.
Bongolander,
Kwenye hizo
red sijui kama umeelewa subject ya mada hii. Hatuna haja ya kutoa lecture nyingine ya ku-define nini maana ya kutangaza.
Hakuna chombo cha habari chenye mamlaka ya kutangaza jambo lolote. Chombo cha habari
kina-habarisha yale yaliyotokea kwenye jamii au yaliyotangazwa na mamlaka husika.
Jamaa kaeleza vizuri kwamba matokeo yalikwisha tangazwa kwa kubandikwa vituoni na mamlaka husika ambayo ni Tume ya Uchaguzi.
Ingekuwa kule vituoni yamebandikwa na taasisi nyingine usingesema Tume imetangaza.
Chombo cha habari kutaja matokeo ya kituoni si kutanganza. Kama chombo cha habari kikipata matokeo ya uhakika ya kituoni, kisha kikapata kopi zenye signature za matokeo hakuna ambacho kingezuia haki yake ya kuwahabarisha yaliyotokea kituoni ikiwamo idadi ya kura zilizobandikwa pale.
Kikitangaza tofauti na yale ya kituoni hata mimi ningetetea kifungiwe maana kinasababisha vurugu kwa kusema uongo. Lakini kama KIKWETE alipata kura 200 kituoni na SLAA akapata 250, halafu mwandishi akalihakiki hilo kwenye kopi ya wakala mmojawapo au hata akachukua photocopy ya ile result voucher
hakuna ambacho kingetokea.
Hakuna mwenye mamlaka au anayeweza kukiadhibu chombo cha habari kama hakijakiuka sheria. Wanacholalamika wanahabari ni sheria yenyewe ilivyo lakini si kwa hili.
Mfano wa DTV ni tofauti. Kwanza tuangalie mazingira yalivyokuwa. Je, DTV ilikusanya ushahidi wa kutosha kujilinda na suala lile? Kama DTV ilienda kituo kwa kituo lakini haikukusanya ushahidi wake basi hilo halitoshi, kwani jamaa hawa wanaweza kwenda kituoni na kubandika matokeo mengine mapema na DTV ikapigwa bao.
Mazingira sasa hivi yamebadilika. Chombo kama TANZANIA DAIMA inajulikana kabisa halina ruzuku au uhusiano wowote na serikali. Gazeti hilo halibebwi kwa namna yoyote na serikali. Hivyo halikuwa na haja ya kuogopa kujizatiti kisheria iwapo itahitajika.
Labda tunasahau kwamba Tume hiyohiyo ilitoa tishio kwamba
mkimaliza kupiga kura ondoka kituoni mrudi nyumbani. Wakati sheria inasema
kuwa usiwe ndani ya mita 200 toka kituoni. Kama tungekuwa mambumbumbu basi tume ingenufaika na watu wasingelinda kura zao kule walikolinda. Lakini hilo lilielimika mapema pale Dr. SLAA na Zitto Kabwe walipohimiza kwamba hakuna aliye juu ya sheria na hivyo hakuna wa kukuadhibu iwapo ulinzi wako wa kura utaanzia mita 200 na Dr. SLAA akaongeza mita zake 100 na hivyo
wana-CHADEMA wakalinda kura zao mita 300.
Huu ni mfano wa kupuuza maagizo yaliyo nje ya sheria. Vivyo hivyo magazeti yangepuuza na kudharau kilichotokea kwa DTV kwa kuchapisha matokeo ya vituoni. Ni haki ya kikatiba na uhuru wa kisheria.
Kama gazeti au wewe mwenyewe una hakika kwamba unalolifanya limo ndani ya sheria, ni nini cha kuogopa?
Kumbuka mfano mmoja bungeni aliyekuwa Waziri Philip Marmo alitishia kwamba mle bungeni imetokea tabia ya watu kutoa vieleleza ambazo ni nyaraka za serikalini. Akatishia kwamba kuanzia hapo wenye tabia hiyo wakikamatwa shauri yao.
Kesho yake Dr.SLAA si kwamba alitii amri ile badala yake akaja na vielelezo vingine zaidi na kumuuliza Marmo kwamba "
vielelezo kama hivi nilivyoshika vya ufisadi vina faida gani kwa taifa hadi tuviweke viwe siri".
Philip Marmo akaishia kusema "Dr. SLAA ana mtandao mkubwa wa kupata nyaraka za siri"
na hakumfanya chochote.
Alikuwa ndani ya sheria.
Woga ule unaousisha DTV ni kutojiamini au kutojiandaa na jambo ambalo limo ndani ya sheria.
Na kama wangefikishana mahakamani pale ndipo gazeti lingepata nafasi ya kuuliza
je tume kuweka matokea kituoni si kutangaza?