Uvivu wetu umeiangusha CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uvivu wetu umeiangusha CHADEMA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nikupateje, Nov 6, 2010.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2010
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wote tumeiangusha CHADEMA kwa uzembe ambao hampendi ujadiliwe kwa kina kila unapoletwa kama si makusudi.

  Tume ilitangaza matokeo ya urais, ubunge na udiwani vituoni kote kwa kuyabandika hukohuko hata kabla ya saa 06:00 usiku siku ya uchaguzi.

  Wagombea uraisi waliopigiwa kura ni sita akiwemo Kikwete, Slaa na Lipumba. Kila wakala ali-sign matokeo na kisha Tume ikampa kila mmoja kopi ajue atakavyoitumia. Kitendo cha Tume kumpa kila wakala kopi ya matokeo kituoni ni aina nyingine ya kutangaza maana baadhi ya kopi zile ndizo Slaa alizotumia kama ushahidi alipoongea na wanahabari juzi.

  Ukijumlisa idadi ya fomu za matokeo zilizotolewa na tume pale kituoni ni saba. Yaani ile iliyobandikwa kituoni na zilizogawiwa kwa mawakala. Kwa lugha nyingine ni kwamba Tume ilitangaza matokeo kituoni mara saba!

  Mara ya kwanza ni pale ilipobandika kituoni na mara sita ni zile ilizowapa mawakala kuondoka nazo wakajichagulie jinsi ya kuzitumia.

  Kituo kutopata watizamaji wengi wa matokeo ya pale haiondoi ukweli kwamba matokeo ya pale yameshatangazwa publically. Labda tu kwa wenye ugonjwa wa kudhani kutangazwa kwa jambo ni pale linaposikika duniani kote.

  Kutangaza ni pale unapoweka jambo lako hadharani kwa public consumption kama unavyobadika matokeo kituoni.

  Turudi kwenye hoja yangu ya uvivu .

  Hivyo basi hatukuhitaji kabisa matokeo mengine zaidi ya yale yaliyotangazwa kituoni. Kama jimbo lilikuwa na vituo 300 ilibidi kila apendaye ajumlishe kila kituo ili kujua kwa jimbo zima Kikwete kapata kura ngapi na Slaa na wenzake wamepata ngapi.

  Kama wapo wavivu wa kujumlisha basi hilo ni tatizo lao lakini binafsi sikuhitaji professa wa dunia hii kuja kunisaidia kujumlisha hata kama jimbo lingekuwa na vituo elfu kumi.

  Sikuamini macho na masikio yangu nilipoona hakuna pressure inayoshabikiwa ya kushinikiza matokeo ya kila kituo. Ni kweli vituo vilikuwa 52,000 na hivyo gazeti maalumu lingechukua siku nne kuyachapisha matokeo ya nchi nzima kituo kwa kituo.

  Ingefanyika hivyo basi leo hii kila mmoja angekuwa na haki ya kusema jimbo fulani SLAA kachakachulliwa kura kadhaa na KIKWETE kaongezewa kura kadhaa.

  Narudia utaratibu. TUme ilitoa kopi ya matokeo kituoni na kwa mawakala zaidi ya sita. Hivyo kulikuwa na source zaidi ya sita kupata matokeo ya kituo kwa kituo. Kama gazeti lingehitaji usahihi lingekaa jimboni ambako mawakala walikuwa wamekusanyika kuwapelekea matokeo wenzao waliokuwa wanajumlisha matokeo ya vyama vyao.

  Kumbe waandishi wa habari hawakuhitaji kupoteza petroli kwenda kituo kwa kituo kupata matokeo ya huko na kuyachapisha magazetini. Je, inawezekana na waandishi walikuwa wavivu wa kujumlisha hadi wasubiri yaliyojumishwa na Tume pale jimboni?

  Lakini waandishi wangejitosaje kwenye biashara hiyo ambayo nyinyi wote hamkuionyesha kama ni habari ya muhimu na badala yake mkawa mnasubiri kujumlishiwa na Tume pale jimboni?

  Mimi naona hiki ndicho kilichomuangusha kila mtanzania. Hata mwana-CCM aliyeshinda hawezi kujivunia ushindi na kumsuta mwana-CHADEMA kwa kuchanganua kituo kwa kituo. Sanasana mwana-CCM huyo ataishia kusema aliamua kujenga imani na Tume kama muumini anavyojenga imani kwa mchungaji wake.

  Namalizia kwa kuweka thread zilizosisitiza matokeo ya kituo kwa kituo na muone jinsi tulivyoisua hiyo mada kila ilipoletwa:


  Tulionyana hivi: { https://www.jamiiforums.com/matukio/83944-tumekataa-matokeo-kituo-kwa-kituo-uvivu-wetu.html}

  Kisha ikawa hivi: {www.jamiiforums.com/results-matokeo/83377-kujumlisha-matokeo-kunatushinda-tuweze-nini-duniani.html}


  Na baadaye hivi: {www.jamiiforums.com/results-matokeo/83558-poor-media-houses-and-journalists.html}
   
 2. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe chadema na watanzania wamejiangusha wenyewe kwa kusubiri tume ijumlishe,kumbe tungekuwa na projection result siku ya tar 1 asubui tu
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Some points inhere...!

  Japokuwa ni sehemu nyingi tu matokeo hayo yaliyobandikwa yamebadilishwa au kusomwa kinyumenyume!..Kuna ushahidi!
  Lakini tusi'pre-empt maongezi haya, maana Dr.Slaa kesho anaweka hadharani mambo mengi, hii ishu ikiwemo!
   
 4. w

  wakushanga JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  EBWANA kIUKWELI TUNA MSUBIRI KAMANDA WETU ATOE TAMKO HADHARANI LAZIMA SIRI ZA WACHAKACHUAJI ZIWE ADHARANI

  KAZI KWAO
   
 5. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  baregu na kampeni team ya chadema inabidi watupe majibu ya kutosha kwa nn hawakuliona hilo.kisha watubu kwa watanzania kwa kusaidia ccm kushinda na wasipewe tena timu hii ya kampeni.
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  It is more complicated than that. Kama kila mtu akiwa najitangazia matokeo kungekuwa na chaos kubwa sana. Tunakumbuka kuwa DTV wamewahi kutangaza matokeo ya sahihi ya uchaguzi Zanzibar, lakini baada ya kuchakachua yakabadilika na matokeo wengi tunakumbuka. No matter what CHADEMA wangefanya mpango wa kuchakachua ulikuwa umewekwa long before eclections. Tunaweza kuwalalamikia kwa kutolinda haki yetu, yaanai hawakufanya kazi vizuri kulinda kura tulizowapigia, na sisi wenyewe hatukufanya kazi nzuri vya kutosha.
  Lakini still CHADEMA imefanya vizuri kuliko tunavyosema, hakika tungependa ifanye vizuri zaidi ya hapo.
   
 7. w

  wakushanga JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  pamoja na kwamba CHADEMA imefanya vizuri, Lakini pia ni Imani yetu kuwa imefanya vizuri zaidi ya hapo

  unaonaje hili Mkuu
   
 8. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  JK alielezea vizuri wizi wa kura unavyofanyika siku alipofanya press conf. Na ndivyo ilivyotokea, what a coincidence! Katiba ndio yakulaumiwa kwani inaruhusu kura kuchezewa bila kupingwa. Na bila kubadili katiba Wananchi wataendelea kulalama tu kila baada ya uchaguzi. Bahati mbaya Katiba haiwezi kuboreshwa kama chama tawala kinashika hatamu. Labda iwe kama ilivyotokea Kenya au alichofanya Seif na Karume zenji ndio tutafanikiwa kuiboresha.
   
 9. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Matokeo kama yalivyotangazwa na NEC haya hapa. Jifungieni kutafuta wapi yamechakachuliwa.
  View attachment 16402
   
 10. K

  Kisanduku Member

  #10
  Nov 6, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bongolander,
  Kwenye hizo red sijui kama umeelewa subject ya mada hii. Hatuna haja ya kutoa lecture nyingine ya ku-define nini maana ya kutangaza.

  Hakuna chombo cha habari chenye mamlaka ya kutangaza jambo lolote. Chombo cha habari kina-habarisha yale yaliyotokea kwenye jamii au yaliyotangazwa na mamlaka husika.

  Jamaa kaeleza vizuri kwamba matokeo yalikwisha tangazwa kwa kubandikwa vituoni na mamlaka husika ambayo ni Tume ya Uchaguzi.

  Ingekuwa kule vituoni yamebandikwa na taasisi nyingine usingesema Tume imetangaza.

  Chombo cha habari kutaja matokeo ya kituoni si kutanganza. Kama chombo cha habari kikipata matokeo ya uhakika ya kituoni, kisha kikapata kopi zenye signature za matokeo hakuna ambacho kingezuia haki yake ya kuwahabarisha yaliyotokea kituoni ikiwamo idadi ya kura zilizobandikwa pale.

  Kikitangaza tofauti na yale ya kituoni hata mimi ningetetea kifungiwe maana kinasababisha vurugu kwa kusema uongo. Lakini kama KIKWETE alipata kura 200 kituoni na SLAA akapata 250, halafu mwandishi akalihakiki hilo kwenye kopi ya wakala mmojawapo au hata akachukua photocopy ya ile result voucher hakuna ambacho kingetokea.

  Hakuna mwenye mamlaka au anayeweza kukiadhibu chombo cha habari kama hakijakiuka sheria. Wanacholalamika wanahabari ni sheria yenyewe ilivyo lakini si kwa hili.

  Mfano wa DTV ni tofauti. Kwanza tuangalie mazingira yalivyokuwa. Je, DTV ilikusanya ushahidi wa kutosha kujilinda na suala lile? Kama DTV ilienda kituo kwa kituo lakini haikukusanya ushahidi wake basi hilo halitoshi, kwani jamaa hawa wanaweza kwenda kituoni na kubandika matokeo mengine mapema na DTV ikapigwa bao.

  Mazingira sasa hivi yamebadilika. Chombo kama TANZANIA DAIMA inajulikana kabisa halina ruzuku au uhusiano wowote na serikali. Gazeti hilo halibebwi kwa namna yoyote na serikali. Hivyo halikuwa na haja ya kuogopa kujizatiti kisheria iwapo itahitajika.

  Labda tunasahau kwamba Tume hiyohiyo ilitoa tishio kwamba mkimaliza kupiga kura ondoka kituoni mrudi nyumbani. Wakati sheria inasema kuwa usiwe ndani ya mita 200 toka kituoni. Kama tungekuwa mambumbumbu basi tume ingenufaika na watu wasingelinda kura zao kule walikolinda. Lakini hilo lilielimika mapema pale Dr. SLAA na Zitto Kabwe walipohimiza kwamba hakuna aliye juu ya sheria na hivyo hakuna wa kukuadhibu iwapo ulinzi wako wa kura utaanzia mita 200 na Dr. SLAA akaongeza mita zake 100 na hivyo wana-CHADEMA wakalinda kura zao mita 300.

  Huu ni mfano wa kupuuza maagizo yaliyo nje ya sheria. Vivyo hivyo magazeti yangepuuza na kudharau kilichotokea kwa DTV kwa kuchapisha matokeo ya vituoni. Ni haki ya kikatiba na uhuru wa kisheria.

  Kama gazeti au wewe mwenyewe una hakika kwamba unalolifanya limo ndani ya sheria, ni nini cha kuogopa?

  Kumbuka mfano mmoja bungeni aliyekuwa Waziri Philip Marmo alitishia kwamba mle bungeni imetokea tabia ya watu kutoa vieleleza ambazo ni nyaraka za serikalini. Akatishia kwamba kuanzia hapo wenye tabia hiyo wakikamatwa shauri yao.

  Kesho yake Dr.SLAA si kwamba alitii amri ile badala yake akaja na vielelezo vingine zaidi na kumuuliza Marmo kwamba "vielelezo kama hivi nilivyoshika vya ufisadi vina faida gani kwa taifa hadi tuviweke viwe siri".

  Philip Marmo akaishia kusema "Dr. SLAA ana mtandao mkubwa wa kupata nyaraka za siri" na hakumfanya chochote. Alikuwa ndani ya sheria.

  Woga ule unaousisha DTV ni kutojiamini au kutojiandaa na jambo ambalo limo ndani ya sheria.

  Na kama wangefikishana mahakamani pale ndipo gazeti lingepata nafasi ya kuuliza je tume kuweka matokea kituoni si kutangaza?
   
 11. M

  Membensamba Senior Member

  #11
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Asante kwa angalizo hili. Nadhani tuchukue hii kama changamoto ya kufanyia kazi chaguzi zijazo. Tuwe askari kweli kweli, tusifanye mzaha katika swala la kulinda kura zetu.
   
 12. T

  Thesi JF-Expert Member

  #12
  Nov 6, 2010
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana nawe 100%
   
 13. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu hoja yako ni ya msingi, na mm nashauri mkakati huu utumike kwenye zile chaguzi za viporo vya ubunge na udiwani zitakazofanyika siku chache zijazo baada ya kuahirishwa pale october 31
   
 14. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #14
  Nov 7, 2010
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  Watazamaji na mashabik siku zote ndo wajua kucheza vizuri na mchezaji akiboronga tu wao ndo wa kwanza kusinya, Wacha hiyo Muo!
   
Loading...