Naweza kusema tatizo la Shaka hajui anachokiongelea, Na hili linaweza kuwa linasababishwa Na kuwa Na elim ndogo yakutambua Na kuchanganua mambo. Kipindi cha kampein nikipindi cha Chama cha siasa kutambulisha Sera za Chama Na mtu wanayemwona anaweza kutekeleza sera hizo za Chama chao(mgombea urais). Mtu hiyo atakae shinda kwenye kuuza sera za Chama chake atakuwa rais ambaye cheo chake anakipata kutokana Na kuuza sera za kisiasa.
Kwahiyo hata rais shughuli zote anazozifanya akiwa ikulu nukutekeleza sera za Chama chake cha siasa. Kwa maana hiyo kila siku yeye anafanya siasa. Sasa inakuwaje uwazui wenzako wasifanye siasa wakati wewe unaziishi?
Umoja Wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ( Uvccm ) umemtaka aliyekuwa waziri mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu ya chadema Edward Lowassa kufuta fikra ya kuwa Chadema itaibwaga CCM hata kama kutakuwa na UKAWA.
Kauri hiyo imezungumzwa na kaimu katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi taifa (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka na kusema kuwa.
“Kwa bahati mbaya Lowassa amesukumwa na hasira na kujikuta akijitoa CCM mwaka 2015 kama mtu aliyekuwa anacheza ngoma kwa kwenda upinzani huku akiwa na matumaini ya kuukwaa urais.Alisema kama kuna kosa kubwa ambalo Lowassa amelifanya ni kitendo chake cha kuhama CCM na kwenda upinzani hasa Chadema ,Kwa sababu yeye mwenyewe alishawahi kutamka hadharani akihutubia mkutano wa hadhara mwaka 2006 akilinganisha upinzani ni watoto wanaokimbilia mdundiko”.Lowassa asikubali kucheza tombola katika siasa,Siasa ni hesabu na ina formula zake.Nafikiri amekurupuka kujiondoa CCM ameupanda mkenge kwenda Chadema ajue kuwa si Ukawa wala Udeta wenye ubavu wa kuiondoa CCM madarakani alisema Shaka.
Alimtaka Lowassa kujua kuwa hata viongozi na wanachama wa upinzani hawamwafiki mwanasiasa huyo kwa asilimia kubwa,kwani wapo viongozi aliowakuta ambao wametoa jasho jingi kuvijenga vyama vyao hivyo hawapo tayari kumpisha agombee tena urais.
Pia Kaimu katibu mkuu Shaka alifafanua kuhusu kauri iliyotolewa na Lowassa kwa kusema kuwa Tanzania kuna ukandamizwaji wa demokrasia..Shaka alisema
“ Haiba ya demokrasia iliyopo Tanzania huwezi kukutana nayo popote Afrika mashariki,Afrika na duniani kwa ujumla,Ila uamuzi wa serikali ya awamu ya tano ni kuwahimiza wananchi kufanya kazina kuzalisha mali viwandani na mashambani.Uhuru wa demokrasia au watu kujitawala bila shibe na maendeleo ya kisekta ni upuuzi.
Alisema kwa msisitizo ndugu Shaka.Pia aliendelea kusema kuwa
“Tumemaliza kampeni na uchaguzi mkuu kila mmoja sasa afanya kazi, kukusanya watu kwenye makongamano na kuwapa bahashishi ni kuwapumbaza kiakili ikiwa bado ni Maskini" alimaliza kusema ndugu Shaka..
Source
Gazeti la Mtanzania la mei 15,2017 toleo Na.8546
Ukurasa wa 8.
![]()
Jeuri ya UVCCM ni kwenye goli la mkono na si kitu kingine. Ndio maana wakakwambia siasa ina fomula. Fomula hiyo si nyingine Zaidi ya bao la kiganja.
Mimi huwa sipigi bao la mkono na wala sitawahi kujaribu kufanya hivyo. Ninaamini sana katika kutenda haki. Uzalendo bila haki ni kitu kisichofaa kabisa. Sitakaa kimya kama utakavyo wewe, bali nitaongea maana uhuru wa kuongea ninao.Toka umeanza kupiga hilo bao la mkono wewe umepata jeuri?! Kaa kimya Wazalendo wanapoongea.
Shaka Hamdu ndugu yangu utaendelea mpaka lini kuandikiwa hotuba, makala na kukufanya wewe uwe kama kasuku kwa kuyiga wasemayo? Ndioo maana mpkaleo bado una kaimu tu. Kama wewe ni mweledi wa siasa za CCM kitu gani kinakuwa kikwazo ya kutambulika rasmi kuwa Katibu Mkuu.
Ushauri , anza kuchukuamafunzo ya jioni , hata ya madrasa alau upate sifa ka vile " sheikh" Hamid alau utanyanyuka kihadhi na utasita kutumiwa kasuku uwe ndio mtu wa kutangaza porojo
Sasa kama unakera na Upigaji wa bao la mkono nenda mahakamani katafute haki kwa unachokiona kinakunyima haki.Mimi huwa sipigi bao la mkono na wala sitawahi kujaribu kufanya hivyo. Ninaamini sana katika kutenda haki. Uzalendo bila haki ni kitu kisichofaa kabisa. Sitakaa kimya kama utakavyo wewe, bali nitaongea maana uhuru wa kuongea ninao.
Chama cha Mafisi huwa hawashindi kihalali. Ni mara chache sana waliwahi kushinda ufalme kihalali
Sijawahi kuona kijana mwenye akili hasa (pretty bright young man) halafu akawa mwanachama au shabiki wa UVCCM. UVCCM kwa kiasi kikubwa ni taasisi ambayo huwaondolea vijana uzalendo kwa Taifa na kuwatwisha ukasuku wa chama. Taifa hili tungenufaika sana kama laiti tungekuwa na vijana wazalendo kwa Taifa lao. UVCCM ni laana kwa Taifa kwa sababu ipo kwaajili ya kuua uhuru wa akili za vijana na kubakia kuwa waimba viitikio vya nyimbo za chama bila kutafakari wala kuhoji. Unapoua fikra za vijana umeua Taifa.
Mahakama ipi niende, hii hii yenu?! Yaani nipeleke kasi ya kurwa kwa doto! Nikipata mahakama iliyo huru nitapeleka kero yangu. Na isitoshe, mbona unaweweseka sana na mimi kusema ninavyosema! je ningekuwa mpiga bao la mkono kama ninyi ungefanyaje? Kwa Taarifa yako, Kama unadhani UVCCM ndio tanuru pekee la kuzalisha viongozi bora, usisahau pia kuwa ni tanuru hilo hilo ndio lililotuzalishia mafisadi papa walioitafuna nchi yetu, wanaoitafuna sasa na watakaoitafuna siku za usoni.Sasa kama unakera na Upigaji wa bao la mkono nenda mahakamani katafute haki kwa unachokiona kinakunyima haki.
Unaakili za kitoto......hakika ukapimwe maana unaweza kufanya mambo ya ajabu 2020.
UVCCM ndio tanuru pekee la kutengeneza Viongozi makini tulionao sasa na wanaokuja.
Kumbe unatafuta AJIRA 😱😱😱Mleta maada yupo kwenye special task ya kikinadi na kukitetea chama sijui ni kwa ujira ule au kuna ajenda ficho! Manake kwa utetesi huu usio na mpangilio sidhani kama 2020 atakuwa na nguvu hizi au zitakuwa zimekata.
Kama ni mkakati wa kuimiliki mitandao kwa misingi ya kukipigia chama chapuo, basi polepole keshaanza na kushindwa. Nimsaidie wazo tu, wapige msasa hao vijana wako jinsi ya ku-propagate na wawe na uelewa wa hoja. Au niajiri nikusaidie kuwanoa. Sudy kalale huna hoja!
Kama umeshindwa kuhamini hadi MAHAKAMA basi wewe ni ZWAZWA kipimo cha Checkup ya AKILI kinahitajika.Mahakama ipi niende, hii hii yenu?! Yaani nipeleke kasi ya kurwa kwa doto! Nikipata mahakama iliyo huru nitapeleka kero yangu. Na isitoshe, mbona unaweweseka sana na mimi kusema ninavyosema! je ningekuwa mpiga bao la mkono kama ninyi ungefanyaje? Kwa Taarifa yako, Kama unadhani UVCCM ndio tanuru pekee la kuzalisha viongozi bora, usisahau pia kuwa ni tanuru hilo hilo ndio lililotuzalishia mafisadi papa walioitafuna nchi yetu, wanaoitafuna sasa na watakaoitafuna siku za usoni.