UVCCM yajibu mapigo ya Lowassa

UVCCM yajibu mapigo ya Lowassa

MBONA BOSS WENU ANALAZIMISHA TANZANIA NZIMA TUWE CCM,AMWAMBI MAMBO KAMA HAYA
Kwanza CCM hatuna boss tunamwenyekiti boss yuko huko kwenye sacoss Dj alieng'angania.

Ukiweza kusema ni wapi na lini amelazimisha watu wote wawe CCM itakua poa.
Ila upinzani itakufa natural death manake unafiki wao unazidi kujioambanua
 
H

Hivi hiki ki-NGO bado kipo hai? hopeless kabisa, utafikiri sio vijana wa chama tawala.
Kuna Chama kilicho na jumuiya imara ya Vijana tanzania na Afrika mashariki kama CCM?
Anza kujiuliza maswali ya kabla ya kujifunga kitambaa usoni kana kwamba hauoni kwamba UVCCM ndio taasisi imara ya Vijana Tanzania kwa upande wa kupika vijana Kisiasa na uzalendo.
 
Wazee wao si ndo wale wanaenda bandarini wanaambiwa kuna meli 30 per day wanachekerea ata awashituki kuwa huu ni uongo ambao ata tahira anaelewa kadanganywa
ALAFU WANATAKA TUWAONE WANA MAANA
Sijui itakuaje Uzee wa hao vijana! Ni faraja ya Moyo na akili kutumia UBONGO bila shuruti.
 
Umoja Wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ( Uvccm ) umemtaka aliyekuwa waziri mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu ya chadema Edward Lowassa kufuta fikra ya kuwa Chadema itaibwaga CCM hata kama kutakuwa na UKAWA.

Kauri hiyo imezungumzwa na kaimu katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi taifa (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka na kusema kuwa.

“Kwa bahati mbaya Lowassa amesukumwa na hasira na kujikuta akijitoa CCM mwaka 2015 kama mtu aliyekuwa anacheza ngoma kwa kwenda upinzani huku akiwa na matumaini ya kuukwaa urais.Alisema kama kuna kosa kubwa ambalo Lowassa amelifanya ni kitendo chake cha kuhama CCM na kwenda upinzani hasa Chadema ,Kwa sababu yeye mwenyewe alishawahi kutamka hadharani akihutubia mkutano wa hadhara mwaka 2006 akilinganisha upinzani ni watoto wanaokimbilia mdundiko”.Lowassa asikubali kucheza tombola katika siasa,Siasa ni hesabu na ina formula zake.Nafikiri amekurupuka kujiondoa CCM ameupanda mkenge kwenda Chadema ajue kuwa si Ukawa wala Udeta wenye ubavu wa kuiondoa CCM madarakani alisema Shaka.

Alimtaka Lowassa kujua kuwa hata viongozi na wanachama wa upinzani hawamwafiki mwanasiasa huyo kwa asilimia kubwa,kwani wapo viongozi aliowakuta ambao wametoa jasho jingi kuvijenga vyama vyao hivyo hawapo tayari kumpisha agombee tena urais.

Pia Kaimu katibu mkuu Shaka alifafanua kuhusu kauri iliyotolewa na Lowassa kwa kusema kuwa Tanzania kuna ukandamizwaji wa demokrasia..Shaka alisema

“ Haiba ya demokrasia iliyopo Tanzania huwezi kukutana nayo popote Afrika mashariki,Afrika na duniani kwa ujumla,Ila uamuzi wa serikali ya awamu ya tano ni kuwahimiza wananchi kufanya kazina kuzalisha mali viwandani na mashambani.Uhuru wa demokrasia au watu kujitawala bila shibe na maendeleo ya kisekta ni upuuzi.

Alisema kwa msisitizo ndugu Shaka.Pia aliendelea kusema kuwa

“Tumemaliza kampeni na uchaguzi mkuu kila mmoja sasa afanya kazi, kukusanya watu kwenye makongamano na kuwapa bahashishi ni kuwapumbaza kiakili ikiwa bado ni Maskini" alimaliza kusema ndugu Shaka..

Source
Gazeti la Mtanzania la mei 15,2017 toleo Na.8546
Ukurasa wa 8.
a9977692f35a5f63b95261aa955bbc3f.jpg

4d5435d0bff966df4f51fb6d520aa3c3.jpg
Hivi sheria ya copyright haihusu mtu kuhamisha habari nzima ya kwenye gazeti kama ilivyoandikwa kisha ukaileta hapa? Naomba wenye uelewa wajambo hili wanisaidie tafadhali!
 
Eti “ Haiba ya demokrasia iliyopo Tanzania huwezi kukutana nayo popote Afrika mashariki,Afrika na duniani kwa ujumla"! Hii ni kauli/statement ya kijinga ambayo nimewahi kusoma mwaka huu...
 
Shaka na UVCCm yake ni wakupuuzwa sana tu huyu jamaa huwa hajui anachokiongea uwa anaongea kama ana garantee na hiyo ccm au na Mungu, aweke akiba ya maneno
Anaongea kweli ambayo kama Vijana wa CCM ufundishwa kusema kweli,
Wanakumbuka mafundisho yao hivyo acha waseme ukweli UVCCM wanaenenda katika hilo.
 
Eti “ Haiba ya demokrasia iliyopo Tanzania huwezi kukutana nayo popote Afrika mashariki,Afrika na duniani kwa ujumla"! Hii ni kauli/statement ya kijinga ambayo nimewahi kusoma mwaka huu...
Pole muhimu ujumbe umefika naimani umesoma vema
 
Kwanza CCM hatuna boss tunamwenyekiti boss yuko huko kwenye sacoss Dj alieng'angania.

Ukiweza kusema ni wapi na lini amelazimisha watu wote wawe CCM itakua poa.
Ila upinzani itakufa natural death manake unafiki wao unazidi kujioambanua
Kuna vitu vingine sio mpaka utamkiwe pambanua anavyo minya democracy lengo si kuuwa upinzani na ukisha uwa upinzani si ni sawa unataka chama kimoja,uyo ndo boss wako cha msingi ulielewa ni namaanisha
 
Sijui itakuaje Uzee wa hao vijana! Ni faraja ya Moyo na akili kutumia UBONGO bila shuruti.
UVCCM utoa vijana thabiti kama ufafanuzi muulize mzee wowote wa chama chako, ila kwa maelezo na mifano tazama viongozi wa leo Tanzania.
 
Imepita miezi sasa nawaza hivi Vyama vingine vinawasaidia vipi vijana katika kuwapika kizalendo maana naona UVCCM pekee ikiwakoka Vijana wengi viongozi wazuri wazalendo kwa taifa letu.
Siwasikii tena Bavicha wala wale wa CUF.
BAVICHA amesikitishwa sana ujinga wa chama chao kuwa kimbilio la watu wa Ovyo.Kwa sasa inasikitisha wamekisusia chama chao kabisa.
 
Awana lolota ao waalibu nchi tu kama wangaipenda nchi tungeona wakimshauli rais wao mbona nchi inaendeshwa ndivyo sivyo wakowapi ao wanafki tu
 
Hivi akili zako bado zipo kwenye Viroba tu.
Hakuna dictator hapa nchini ila mnatengeneza mazingira ya kuwapambanisha watawala na wananchi
Tumewapuuza ukweli utasimama
Sudy, rejebisha hili neno tumewapuuza ili lisomeke kuwa nimewapuuza. Hii ni kwasababu nyingi tu ikiwa wewe siyo uvccm yote na wala sio ccm yote na huenda wewe ni member na si msemaji wa vyote hivyo punguza mapovu tuelewane.
Unadiriki kuwa msemaji wa serikali pale unapoitetea demikrasia inayopraktisiwa gizani na hilo jingine uliloliandika kuwa hayupo kihivyo bali ni uchonganishi tu sikubaliani nawe.
Hivi hujajua kuwa watu wanaitumia milango yao ya fahamu ipasavyo kwa sasa? Pita mitaani usikie wanavyoponda kila kinachofanyika. Jukwaani utaongopewa, ingia field kitaa na huyo uvccm wako mjitambulishe muisikie misonyo!
 
Awana lolota ao waalibu nchi tu kama wangaipenda nchi tungeona wakimshauli rais wao mbona nchi inaendeshwa ndivyo sivyo wakowapi ao wanafki tu
Nadhani ww mkongo wa tz hutuongei ivo
 
Chadema hawa hawa, wawatoe ccm madarakan? Hiz ndoto za mchana iz
Bado sijamuona wakuing'oa CCM wapinzani wote ni wazandiki na nimegundua wanategemea pesa za CCM kuiondoa CCM [HASHTAG]#WatashindwaTu[/HASHTAG]
 
UVCCM utoa vijana thabiti kama ufafanuzi muulize mzee wowote wa chama chako, ila kwa maelezo na mifano tazama viongozi wa leo Tanzania.
Ni kweli UHURU wa Kidemokrasia na kujitawala ni UPUUZI bila shibe na maendeleo ya kisekta??? Ni kwa nini KATIBA YETU inatamka Nchi yetu ni ya UHURU wa Kidemokrasia??
 
Sudy, rejebisha hili neno tumewapuuza ili lisomeke kuwa nimewapuuza. Hii ni kwasababu nyingi tu ikiwa wewe siyo uvccm yote na wala sio ccm yote na huenda wewe ni member na si msemaji wa vyote hivyo punguza mapovu tuelewane.
Unadiriki kuwa msemaji wa serikali pale unapoitetea demikrasia inayopraktisiwa gizani na hilo jingine uliloliandika kuwa hayupo kihivyo bali ni uchonganishi tu sikubaliani nawe.
Hivi hujajua kuwa watu wanaitumia milango yao ya fahamu ipasavyo kwa sasa? Pita mitaani usikie wanavyoponda kila kinachofanyika. Jukwaani utaongopewa, ingia field kitaa na huyo uvccm wako mjitambulishe muisikie misonyo!

Acha kupotosha umma kwa kuzunguka katika jimbo lako linalomilikiwa na Ukawa ambapo mpaka sasa haujapata maendeleo yoyote toka kuwachagua.
Jimbo ninalotokea mimi ukijitambulisha wewe ni Ukawa sijui Chadema maana bavicha hawatambuliki kabisa juwa kabisa jinsi utakavyodharaulika ni zaidi ya teja maana tunaamini hakuna mkweli katika upinzani kwakuwa wamejikita kupotosha kila kweli ambayo kwa waelewa wa mambo dhahiri wanatupeleka chaka.....

Kuhusu usemaji wa Chama naomba utambue hapa sipo kwenye kukisemea chama wala taasisi ya chama, ila nipo katika kutetea kweli dhidi ya wapotoshaji......rejea habari ya hapo juu.
 
Back
Top Bottom