UVCCM wawili waliotembea kwa miguu kutoka Dar hadi Musoma wapewa zawadi na Rais Samia. Hongera zao Km 1400 sio mchezo

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Vijana wawili(wa kiume na wa kike) wa uvccm wamepewa zawadi na Mh.Rais Mama Samia kwa kuonesha uzalendo baada ya kutembea kutoka Dar hadi Musoma kwa miguu ili kuhudhuria sherehe za miaka 45 ya CCM.

Mimi pia niwaoongeze maana kutoka Dar hadi Musoma Ni zaidi ya km 1400.

Ila muonekano wa huyu binti unanifanya pia niwe na mashaka ya kuweza kutembea kutoka Dar hadi Musoma.

Ila kwa kuwa jambo hili limefika kwa Rais na kaona ni sawa, basi mimi na wewe hatupaswi kuwa na doubt.


 
"Kwa kuwa jambo hili limetua mikononi mwa raisi mimi na wewe hatupaswi kuwa na doubt"

Kwa sababu yeye ni mungu
 
Vijana wana moyo sana hawa,kutembea umbali mrefu kama huo sio jambo rahisi,ingawa pia bado sijajua kuwa safari yao huwa inakuwaje...
 
Wangesema wametumia siku ngapi kwanza, ndio tungekuwa na pa kuanzia , ili tuone ki mahesabu inawezekana!!isije ikawa kama wale wa kigoma kuja dar, km 1500, mtu anatumia siku 14!! Uongo mkubwa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…