UVCCM wameandaa Mkutano wa kuvunja amani Mwembe Yanga leo Oktoba 10, 2015

Nimemshuhudia ktk star tv nikiwa nje ya nchi lakini walichosema tuliokuwa nao baada ya kusikia huyo Sadifa walikubali kuwa Afrika bado wenye akili za gorilla/nyani wangali wakitangulizwa mbele.
mwengine akasema kama Tanzania kuna malaika wa Mungu basi ni Lowasa maana majeshi yote ya kuzimu yamejipanga kumtukana lakini yeye amenyamaza kimya na wala hakuwajibu sawa sawa na upumbavu wao. Nami nikawaambia kuwa hakika Mungu wa mbinguni amemfanya jiwe la kukwaza kwao ambapo litawaponda adui zake wote na kuwasaga tiki tiki. HAYA YANATENDEKA PASIPO KAZI YA MKONO WA BINADAMU.
.
 
Sadifa anafahamika kwamba ni bingwa wa matusi , taarifa kutoka unguja zinasema malezi yake yamechangia , lakini naamini Mungu atamlipa .
 
Mbona mnababaika sana. Sasa hapo ni wapi kahatarisha amani?

Ivi aliesema kiongozi kapewa sumu na kulazwa hospitali na hawa wanaosema kiongozi kajinyea, mara kajikojolea mara ni marehemu kati ya hao ni yupi mwenye kosa kubwa zaidi ya mwenzie? This country bana...
 
Tatizo malezi, mtu kama umelelewa hovyo lazima utukane bila kujali huyu sawa na baba'ko au mama'ko, yaani mi nashangaa sana ccm inapohubiri amani wakati wanatumia jukwaa kukashfu na kutukana bila kujali kuna watoto wanaowasikiliza na kuwatazama, ni aibu sana kwa uongozi mzima wa ccm, tukumbuke kuna maisha baada ya uchaguzi, Mzee wa watu hata ajibu matusi na kashfa zao..!!
Bahati njema tulikuwa na umeme maeneo ya kwetu leo na kuutazama mkutano wa "vijana hawa wapumbavu wa UVCCM"

Maneno ya Sadifa Juma sijui ndiye mwenyekiti wa UVCCM huyo yalivuka mipaka na ni matusi. Nadhani hawana lugha sahihi ya kumnadi mgombea wao Magufuli na badala yake wana attack personality ya mtu. Ni kosa na nadhani kwa sasa wanastahili kujibiwa the same way!

Hawa si tu malezi mabovu kwa hawa vijana wa CCM, zaidi sana ni frustration za kipigo cha uchaguzi na kushindwa ambako dhahiri kiko mbele yao to the extent kwamba wamekosa akili kabisa!!

Mzee Kigunge ameshalisema hili vizuri. Kwamba CCM wamekosa watu kabisa wenye busara na wanafikiri wanaweza kueleweka na kushinda uchaguzi kwa kufyatua matusi midomoni mwao. Wazee wa CCM halisi, wenye busara zao wamesusa!!
 
mkuu kwani ubungo sio kubenea tena??

Mkuu Ubungo UKAWA hakuna.Kubenea anachofanya ni kuwanunua viongozi wa CUF wenye njaa kwenye baadhi ya mitaa nakata ambapo viongozi hao wa CUF wachumia tumbo wenzake wanachofanya ni kumpaka matope wakili Ngole.Lakini kiuhalisia Kubenea hakubaliki.Wapambe wa team Kubenea walijaribu kumhonga sana dogo asirudishe form lakini dogo akakataa.Kilichofuata Kubenea alichofanya ni kuwanunua CUF njaa. Ukweli ni kuwa wana Ubungo wanamtaka mzawa halisi anayejua matatizo ya wanaUbungo.Mashaka Ngole amesoma shule ya msingi Kawawa, Kigogo Luhanga vilabuni Uswazi.Secondary amesoma Azania na chuo ni Zanzibar University. Kubenea wala Masaburi wana Ubungo hawawajui.Ni watu tu wamezuka sidhani hata kama Charles Keenja wanamfahamu.
 
Wameishiwa sera yamebaki matusi wasiona na akili ndo wataowachagua mimi hamnishawishi hata mwanangu wa miaka 2 naona aibu kuangalia nae kampeni za ccm maana aliniuliza mbona yanga wanatukana nilishindwa kumjibu.
 
Gwajima alimsema Cardinal P ikawa kesi. Lakini ya Lowasa kutukanwa wanaona powa tu . Duu Jeshi letu noma. But Peoples Power always.
 
Back
Top Bottom