UVCCM wameandaa Mkutano wa kuvunja amani Mwembe Yanga leo Oktoba 10, 2015

Sep 26, 2015
10
11
Kupita mkutano wa UVCCM unaofanyika muda huu hapo Mwembe Yanga, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Juma amesisika akisema kupitia televisheni ya Star TV kuwa "Lowassa anatokwa na mikojo barabarani" hii ni kauli yenye lengo la kuvunja amani ya nchi.

Ikumbukwe kuwa Lowassa anayeambiwa na UVCCM kuwa anatokwa na mikojo barabarani ni baba wa familia, ni babu wa wajukuu na zaidi ya yote ni kiongozi wa nchi hii aliitumikia nchi hii akiwa waziri mkuu (2005-2008), pia ni Mgombea Urais wa CHADEMA na UKAWA chama na umoja ambao una mashabiki na wapenzi wengi ambao wasingeweza kuvumilia kuona kiongozi wao anatukanwa hadharani na UVCCM.

Sadifa Juma na UVCCM ni mchochezi na wanavunja amani ya nchi hii wakiwa ni sehemu ya chama tawala CCM, hii inamaanisha kuwa CCM imemtuma Sadifa kumtukana Lowassa na ni dhahiri kuwa CCM ndio chama kinachoanzisha vurugu na uvunjifu wa amani.

Wakati Sadifa Juma wa UVCCM anamtukana Lowassa uwanja anaotumia umejaa askari ambao hawakuonekana kumchukulia hatua za kumkamata kwa kutoa lugha za uchochezi, matusi na udhalilishaji hadharani.

CCM inaimba wimbo wa amani lakini inavunja amani kwa matamshi yake yenyewe. CCM inaimba kama malaika na inacheza kama mashetani. CCM ni waongo sana, wanajifanya Kuimba amani kila kona ya nchi wakati huo huo wanavunja amani kwa kumtukana Lowassa hadharani. Shirika moja lililofanya utafiti limebaini Lowassa ameshatukanwa na CCM mara 121 katika majukwaa mbalimbali ya kampeni.

Mimi kama AdvocateMtetezi nalishauri "jeshi la policy", wamchukulie hatua Sadifa Juma mwenyekiti wa UVCCM kwa kumtukana Lowassa hadharani kuepusha vijana wa UKAWA na vijana wanaompenda Lowassa nchini kujibu mapigo. Nawashauri pia vijana wa UKAWA endapo "jeshi la policy" halitachukua hatua dhidi ya UVCCM na Sadifa Juma basi wao pia wajibu mapigo kwa namna watakavyoona wao inafaa, kama alivyofanya mwenzao Sadifa Juma akitumia jukwaa la UVCCM na kurushwa live na kituo cha Star TV.
 
Anahitaji fundisho liwe fundisho kwa wengine, ccm wana mdomo mchafu sana, matusi kama haya tulizoea zanzibar sasa kuhamia tanganyika, umekuwa ugonjwa wa ebola
 
asili ya matusi yametokea chadema ccm wakawa wanaduwaa na kuwa matusi mfululizo nao ccm wanajibu mapigo sasa machungu
 
Na nyie tukaneni humu, nyie si wazee wa mitandao?? mbona mnakuwa vigeu geu hivyo? mmesahau vijana wa mbeya walichofanya kwa magufuli? kule sio kuvunja amani? muwe neutral bhana, kama habari yako ni ya kweli basi uvccm wamekosea, ila yawezekana alisema hivyo akimaanisha kitu kingine na wewe ukamtafsiri kama alivyosema.
Mkuki kwa nguruwe ....
 
Mkuu umenena vyema lakini usishangae kuitwa mchochezi ni wewe after all lowasa katufundisha somo zuri sana la uvumiliv
 
Safifa ni mlemavu wa akili siku nyingi! Kuna kipindi CCM wenyewe waliwahi kulalamika kwanini Sadifa amepewa wadhifa huo kutokana na matatizo hayo.
 
Mtu kama Sadifa inawezekana ni chokoraa. Hana malezi na kwa sababu hiyo hana maadili. Eti hao ndiyo viongozi wa CCM. Hatuwezi kuongozwa na watu wasio na adabu. Hata kama Lowassa angekuwa ni mtoto wake bado siyo sawasawa kutamka huo ushenzi hadharani. Halafu atokeze Lubuva aseme ni vionjo vya siasa. Atakuwa anajiandaa kwenda ICC.
 
Bado siku chache kitaeleweka vichinjio tunavyo sisi kwa tar 25 Oct kitaeleweka tu mkojoa barabarani na vyovyote vile.
 
Twende kwenye ukweli alichosema ni kweli au siyo kweli kwani geita alifanya nini pia.
 
Waliomtukana lowassa karibu wote wamerest in peace na wengine wamepoteza viongo◀ huyo ajiandae kunywa mikojo yake mwenyewe na kushindia diapers. Mungu hadhihakiwi wajamani.
 
Kumtukana,kumkashifu,kumsengenya,kumkejeli na kumwombea mabaya mpumbavu,lofa na mbumbumbu mwenzetu ni sawa na kumpaka "Marashi" na kufanya aendelee kung'ara sana!
 
Sera CCM zimeisha, imebaki matusi tu.Wana Ubungo tunasema kura kwa Lowassa na ubunge kwa wakili Ngole wa CUF.
 
Dalili za ccm kushindwa, tulizoea kipindi cha nyuma kuona upinzani ndio wakitoa matusi na kwa kiasi fulani ccm wakiwa na kampeni za kistaarabu sasa ccm ndo wamekuwa kama wapinzini, nadhani ndo wanajiandaa kisakolojia, waacheni kwani kwao wakitukana ndo wanapata ahueni. Kwisha habari yao
 
Back
Top Bottom