UVCCM kuvunjwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM kuvunjwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Oct 20, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  UONGOZI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi, (UVCCM), uko hatarini kuvunjwa kwa madai ya kuwa chanzo cha migogoro ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

  Duru za siasa kutoka ndani ya CCM, zilisema kuwa hoja ya kutaka umoja huo uvunjwe iko mezani kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, ambaye kwa kutumia kanuni na vikao vya chama, ndiye mwenye uwezo wa kufanya maamuzi hayo mazito.

  Habari hizo zinasema kuwa Rais Kikwete amekasirishwa na mzozo wa UVCCM ambao safari hii umefika mahala unaihusisha familia yake. Mmoja wa makada wa chama hicho, aliliambia gazeti hili kuwa kwa sasa umoja huo haukisaidii chama badala yake umekuwa chanzo cha migogoro kwa kutumiwa na makundi yanayowania urais mwaka 2015.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Riziwan at work
   
 3. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mhhhhhhhhhhhh
  nchi iko mikononi mwa familia
   
 4. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye Red ndipo paliponifanya nione habari hii ni Uzushi. Jamaa hana sifa wala uwezo huo.
   
 5. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Wakimaliza kuvunja jumuia zote kinachofuatia itakuwa ni kulivunja li-ccm lenyewe. Hongera sana JK
   
 6. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  yaani mwenyekiti akikasirika tu, yeye anaamua kuvunja tu. mbona mambo ya muhimu yakiletewa masihara yeye akasiriki. yeye anakasirikia vitu vya kijinga kijinga tu...
   
 7. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Acha waivunje tu haina msaada wowote kwa vijana watanzania zaidi ya kuchumia matumbo yao na sasa wako busy kujitengenezea mrija wa 2015. Kama hata Livingstone Lusinde alipitia huo umoja na ukilaza ule unategemea kuna taasisi hapo? Tena wasipoivunja itavunjika yenyewe. UVCCM SUCKS...
   
 8. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hivi lini vile wataifanya hiyo kazi nikanywe pombe za kienyeji kuenzi uhuru wetu.
   
 9. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ni kweli hauna msaada nakumbuka walipokutana Pwani chini ya Riziwani walisema ni zamu yao kula.
   
 10. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Vita ya panzi furaha ya kunguru
   
 11. b

  ben genious Senior Member

  #11
  Oct 20, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kisa! wamemgusa riz1
   
 12. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,912
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  Binafsi nilichokiona ni kwamba ndani ya UVCCM kuna watu ambao wameiweka pembeni ili kasumba ya ndiyo mzee, jambo ambalo linamkasirisha JK pale maagizo yake (kupitia mwanae) yanapopingwa wazi wazi.. Kuivunja UVCCM hasa katika kipindi hiki itakuwa ni ishara nyingine ya kuisigina Demokrasia ndani ya chama, Kikwete analazimika kukubali hali halisi ya uelekeo wa upepo wa kisiasa nchini, vinginevyo historia itakuja kumhukumu..

  Kwa kuanzia, afanye mpango wa kuitenganisha familia yake na siasa.
   
 13. M

  Makupa JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  uvccm ni muhimu sana ikavunjwa embu niambie ukimuondoa malisa pale uvccm kuna nani
   
 14. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  M/kiti ana nafasi kubwa sana ya kuyaunganisha haya makundi kwa sababu kila kundi linamsifu yeye na kusema wazi kuwa linamuunga mkono 100% akiamua kuondoa mgogoro huu m/kiti anaweza

  Kuvunja Jumuhiya hii si suluhisho kabisa
   
 15. F

  FUSO JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,297
  Trophy Points: 280
  ehee sasa dhambi ile ile imeanza kuwatafuna wenyewe kwa wenyewe!!!
   
 16. F

  FUSO JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,297
  Trophy Points: 280
  una maana huyu wa sasa au ajaye?
   
 17. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Si kweli kuwa kila kundi linamsifu yeye wengine wanalazimika kuonekana weupe usoni lakini ukiwatizama moyoni ni weusi tii.
   
 18. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu hata hao vijana wa chadema wote ni wachumia tumbo tu. hakuna la ziada. Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kifkira zaidi kuliko hata ya kichama na hata katiba.
  Uzalendo wetu unakaribia zero. Imegine hela za nmb ziliibiwa pale ubungo miaaka ile JK ameingia tu madarakani lakini nikiwa pale mlimani mwanafunzi mmoja alifikia hatua ya kusema eti hawa wangefanikiwa wangekuwa wame-win,
  kwa kweli kwa hasira niliyokuwa nayo sikumkopesha yule dogo. nilimpa ya ukweli hapo hapo.
   
 19. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #19
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Unaanza kuweweseka.
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,440
  Likes Received: 81,486
  Trophy Points: 280
  Kama kawaida ya usanii wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Magamba wanatafuta njia rahisi ya kuonyesha kwamba tatizo lao Magamba linasababishwa na UVCCM. Hivi ufisadi wa kutisha ndani ya Serikali unaofanywa na wanaojiita viongozi ndani ya CCM/Serikali ikiwemo wa sasa na waliopita waliaamrishwa wafanye ufisadi huo na UVCCM!? Kwa mwendo huu wa kisanii basi siku za magamba katika anga za siasa zinazidi kuwa finyu.
   
Loading...