UVCCM Kufanya Mandamano August 31

UVCCM Kufanya Mandamano August 31

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) imepanga kuitisha maandamano nchini nzima Agosti 31 mwaka huu yenye lengo kumpongeza Rais John Magufuli kutokana utendaji kazi tangu aingie madarakani.

Kaimu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Shaka Hamdu Shaka alisema maandamano hayo ni ya amani tofauti na vyama vingine na tayari wameshatoa taarifa kwenye vyombo vya dola kwa ajili ya ulinzi.

Alisema Rais Magufuli amefanya mambo mengi katika kipindi kifupi alichokuwa madarakani hivyo hawana budi kumpongeza kwa njia ya maandamo ili kufikisha ujumbe kwa wananchi waliomchagua.

My Take: Hii ni kwa ajili wakinyimwa waseme ya UKUTA nayo yasitishwe. Mchezo huu hauitaji hasira poleni
 
MAANDAMANO UVCCM: UVCCM yatangaza kufanya maandamano nchi nzima Agosti 31 kwa ajili ya kumpongeza Rais Magufuli kwa utendaji wake mzuri, Shaka H. Shaka aeleza.

Mytake
Hii nikwajili wakinyimwa waseme ya UKUTA nayo yasitishwe. Mchezo huu hauitaji hasira poleni
Mbona yanajulikana na mingine yapo. Ila Sept 1 ni kurasimisha UKUTA.
 
Tumeona kutatokea machafuko baina ya vyama viwili....
Hivyo tumeikataza na kuinyima kibali cha mandamano UVCCM ...
Na pia operation UKUTA bado tumeipinga...
 
Unajua hii nchi ina drama za kipuuzi sana kwahiyo maana ake ni nini hasa hahaha aisee
Watu hawataki kufanya kazi....!!!

M/Kiti wa CCM taifa awe makini vijana watamvurugia. Mimi nilitegemea vijana wa UVCCM sasa waonyeshe njia kwa kufanya kazi kwa kuanzisha miradi mbali mbali ya kuwaletea maendeleo watanzania, kwa kutumia vitegauchumi walivyonavyo wawasaidia vijana kupata mitaji nk. Wawatembelee vijana kwenye maeneo yao wakusanye kero za vijana na kuziwasilisha kwa sekeretarieti ya chama na kisha afikishiwe mwenyekiti wa Chama taifa. ndiyo maana nasema UVCCM nayo inatikiwa kufumuliwa. Kama ni kweli wanataka kufanya hivyo eti kuandamana kumuunga mkono Rais...na sema watakuwa hawafai. Rais ninayemjua hataki kuungwa mkono kwa staili ya maandamano. Wajiangalie hao viongozi wa UVCCM.
 
MAANDAMANO UVCCM: UVCCM yatangaza kufanya maandamano nchi nzima Agosti 31 kwa ajili ya kumpongeza Rais Magufuli kwa utendaji wake mzuri, Shaka H. Shaka aeleza.

Mytake
Hii nikwajili wakinyimwa waseme ya UKUTA nayo yasitishwe. Mchezo huu hauitaji hasira poleni
Hao ndio think tank ya chama, copy n paste
 
Hao ndio think tank ya chama, copy n paste
Tatizo lao liko kwenye fikra zile za enzi za chama kimoja kilichokuwa kinajinasibisha na siasa za kishoshalisti au ukomunisti. Naukumbuka wimbo mmoja wa miaka ya themanini uliokuwa unaimbwa "Naani naani naani anapinga chamaa, anayepinga chama serikali imtoee!" Wanatamani sana turudi zama hizo!!
 
  • Thanks
Reactions: t2t

Tanzania ni Nchi huru. Kila mtu ana uhuru na haki ya kuwaza anavyoweza. Huna mamlaka ya kubana uhuru huo
 
Back
Top Bottom