UVCCM: Hussein Bashe amjibu Nape kiaina

Bashe kwanini unatumia jina la kificho? Unayoyasema yana mantiki na ingekuwa credit kwako zaidi kama ungekuja na jina lako hasa!
 

Mwengine huyu ndani ya Gamba, Kigwangwalla!
 

Just curious! Hivi Bashe kama anaona Lowassa ni kiongozi mzuri, na zaidi ya hapo anafanya kazi na Rostam kweli CDM wanaweza kufanya kazi na mtu wa hivi? Kuna usemi unasema " kama unataka kujua mimi ni mtu wa aina gani try to study those I hang out with." I am not a politician but; hizi siasa za kuhama hama ndio zinazovuruga vyama. Hivi Tanzania mwananchi hawezi ku-support kiongozi/viongozi wa chama kingine mpaka ujiunge na hicho chama? Kama kweli tunatanguliza nchi kwanza why are we supporting someone kutokana na itikadi/chama chake na sio uwezo wake?
 
Bashe unapiga porojo tu za siasa tu na nakuhakikishia ubunge wa Nzega utausikia tu kama ukiendelea kujaza orodha ya miaka 20 ya hujuma. We kiongozi gani unasema oooh nimesamehe lakini siwezi kusahau mwaka XYZ mara sina kinyongo lakini sitasahau mwaka XXX mara ooh sina tatizo na mtu lakini sijasahau mwaka XY! Hayo ya kuto kusahau unayaweka ya nini? Kama huwezi kusahau bwana mdogo siasa haikufai nenda kawe mvuvi tu.
 

Kabwela Mzito

Huwezi kupanga Mkakati wako wa kesho kwa kusahau Matukio ya Jana,Huyu dogo ameonyesha ukomavu wa Kisiasa na Uongozi,Kiongozi Makini ni Yule ambae anatumia Historia kama Sehemu ya Kumbukumbu zake Muhimu.Matukio yaliyomkuta Bwana Bashe hawezi kuyasahau kwani hayo ni sehemu ya Historia yake ya Maisha yake ya Kisiasa.

Angesema Sijasamehe,Angesema Atalipiza Kisasi hata Mimi Ningelimshangaa,Angesema Amesamehe na Amesahau Ningelimshangaa kwani Watanzania Wengi Tunalikumbuka Tukio la Mwaka Jana ambalo lilinifanya hata Mimi kutaka Kumfahau Bashe.

Umesema Ubunge Asahau kwakuwa anakumbuka Matukio yaliyomkuta katika siasa Nakushangaa ni namna gani unataka kiongozi ambae hana kumbukumbu ya Matukio yaliyomkuta yeye Binafsi,je atakumbuka matukio yaliyowakuta anaowaongoza?Leo hii sisi watu wa Kagera Tumesamehe Uzembe wa Serekali yetu iliyopelekea ndg zetu kufariki ktk tukio la MV BUKOBA lakini hatuwezi kusahau kwani ni sehemu ya Historia yetu.

Bashe samehe lakini Usisahau wana Nzega wanakumbuka Iweje wewe Usahau utakua kiongozi Dhaifu asiekuwa na Kumbukumbu ya Historia yake Binafsi.

Ila dogo CCM ndo mwisho wake ondokaaaaaaaaa
 
Hotuba imetulia kisawasawa... hatutaki majungu ila maisha ya Mtanzania yaboreshwe iwe CCM. CDM, CUF sawa ila maisha ya mtanzania yakae sawa
 
.....Akili za mwenzio changanya na za kwako.....hata malaika wa shetani ana mabawa...
 

Mzito kabwela, kuna tofauti kubwa kati ya Kusamehe (Forgive) , na kusahau (Forget) .Bashe mimi ni mpiga kura wako wa Nzenga na ni mmoja wa wanachama wa CCM waliokupigia kura kilichofanywa na JK a.k.a Mbayuwayu si tu kilikuhumiza wewe hata sisi wananzega kilituhuzinisha sana ,na Ninakuhunga mkono statement yako ''umesamehee lakini hautasahau'' Waziri mkuu wa Uingereza miaka ya 1930, s Benjanim Israel aliwahi kusema ili ufanikiwe katika siasa za ni vizuri umsamehee adui yako lakini usisahau jina lake ''Forgive your are Enemy but never forget is name".Na Tunapenda kukuhakikishia kwamba hatujamsamehee Mbayuwayu na mwanae shorti(mfupi kama mbilikimo) the way walivyo treat suala la jimbo la Nzega
Mzito Kabwela Please ya Nzega tuachie wana-Nzega
 
Kwa kweli katika hili Bashe ameongea vema . Nadhani Hata kikwete amesikia huko Mwanza ingawa yeye ndiye mdini wa kwanza. Watu hawataki hadithi wanataka kuona sukari ,unga mafuta vinapungua bei. Sasa haya magamba mengine hayaelewi yanakalia porojo kwenye majukwaa ambayo hata watu hawahudhulii kwa wingi. Dr Slaa endelea kuwaelimisha watu juu ya haki zao ili Mkwele achomoke kabla mambo hayajawa mabaya maana mi naona 2015 ni mbali sana na shida zitakuwa zimetumaliza.
 
Bashe hoja ulizotoa zinaua chama chetu nani kakuambia useme hayo yote? umekosa uzalendo katika chama
 
ni hotuba nzuri......lakini mapacha watatu lazima wahukumiwe kutokana na matendo yao ndipo wananchi tutakapo kuwa na imani na chama chenu.....
 
Huyu kijana ameongea pointi nzuri sana, sasa sijui kama wakubwa wake watakubali huo ushauri
 
Baada ya kusoma post ya kwanza ya thread hii nikajiambia " well saida Bashe" lakini majibu aliyotoa bashe kwa lampard (offcourse ana uhuru na haki ya kujibu kama alivyo jibu) ndipo nikaona kuna uwalakini ... kama kweli Bashe anamsapport Lowasa, basi ...
 

Heshima kwako Hussein Bashe.

Kwanza naomba kukupongeza kwa kuja jamvini na kujibu baadhi ya hoja na kutoa ufafanuzi katika masuala mbali mbali.Nikiri umejitahidi kujenga hoja lakini pia nikiri lugha unayotumia haifai kabisa ndani ya jamii iliyostaharabika,imejaa dharau,kiburi na zaidi ya yote inakatisha tamaa.

Umekiri mwenyewe umechezewa rafu kibao ndani ya chama chako baya zaidi umeonyesha dhahiri wewe ni mtu wa visasi na vinyongo.Vipi mambo uliyotendewa miaka mingi nyuma hutaki kusahau ? Labda imani na asili yako imekufunza hivyo,ukitendewa jambo baya siku zote ni lazima ujifunze kusamehee na kusahau.Ni uzushi na ubazazi kusema umesamee jambo fulani lakini huwezi kusahau.

Unakiri Lowassa akigombea urais utamuunga mkono hakika kati ya mambo ya kipumbavu uliyowahi kukiri hadharani hakuna kama hili na ikiwa msimamo wako ni huu hakika waliokunyima nafasi ya kugombea ubunge hawakufanya kosa kabisa walikuwa sahihi na ikiwa watakufanyia tena mwaka 2015 watakuwa wamelitendea taifa letu changa jambo jema.

Nikiri mwamzoni nilidhani Bashe ni miongoni mwa vijana wanaoweza kulisaidia taifa lakini baada ya kupitia andiko lako nimegundua hufai hata kurejeshewa uraia wa Tanzania.Vijana wa aina yako ndio wameifikisha Somalia hapo ilipo sasa [kukumbatia magaidi na wezi wa mali za umma]

Mwisho Mungu hawezi kuibarikia Tanzania wala Afrika kama tutawatukuza wezi na mafisadi.

Naomba kuwasilisha.
 
Jamani pamoja na yote inabidi jamaa asifiwe kwa kusema ukweli,hivi mtu hawezi kuwa na mawazo huru mpaka atumwe na watu wengine?jaribuni kusoma maudhui ya ujumbe acheni kumjaji mtu binafsi,ameongea ukweli kabisa kuhusu mstakabali wa maisha yetu amekikosoa chama cha magamba,amemkosoa Nape,nampa big up maana tunakokwenda kuna giza na mkulu mwenyewe chenga tupu.nawasilisha
 
suala sijui bashe katumwa anamuongelea nani hili si la msingi, la muhimu ni ujumbe aliousema una mashiko si mchezo. Saa nyingine hata vichaa na wendawazimu huongea ukweli judge the message not the messenger

jamali kassim naye anajua siasa??? Ccm mmekwisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…