Mlachake
JF-Expert Member
- Oct 13, 2009
- 4,412
- 4,559
Kuna kipindi fulani nikiwa nasota Kijiweni na Masela niliuziwa pete yenye kidani chekundu. Kuna rafiki yangu aliona nimevaa ile pete alishtuka sana akanipa nadharia nyingi sana kuhusu hizi pete.
Kiukweli baada ya kama miezi miwili baadae majanga yalianza kuniandama moja baada ya lingine likiisha hili linakuja jingine tena gumu zaidi, mitihani juu ya mitihani.
Kwa jinsi nilivyoteseka, nikaona isiwe taabu, nikaamua kutupa ile pete. Asubuhi niliamka nikairusha nje ya fensi, Niliporudi jioni nikaikuta ndani ya fensi nikajua labda watoto walikuwa wanacheza nje wakaikota wakairusha ndani kwasababu ile nyumba nilikuwa naishi mwenyewe. Ikabidi nimtafute yule aliyeniuzia nikamrudishia.
Sasa sielewi kama yale majanga ni kwasababu ya ile pete au ni misukosuko tu ya maisha kwasababu nilipoteza savings zangu zote.
Hivi ni kweli hizi pete zinahusiana na ushirikina?