Mi nakushauri usajili jina la hizo spika kama kampuni halafu endelea kujitangaza kwenye mitandao kama ulivyofanya kwa Millard Ayo na hapa JF. Pia tengeneza videos nyingi kuonesha uzuri wa spika zako (muonekano, sauti) halafu uziweke Youtube na kwingineko. Pia soma mrejesho wa 'comments' za watu ili ujue wateja watataka nini.
Katika biashara, kitu muhimu ni 'positioning', lazima ujiweke kiaina fulani hivi ili watu waweze kukufahamu.
Ntakupa mfano, zamani kulikuwa na 'search engines' nyingi kama (overture.com, ecosite.com na yahoo.com) zilizokuwa zinatoa 'results based on how many times a certain keyword appears'. Hii ilifanya index ya hizo search engines kutokuwa sahihi kwasababu ilijumuisha spam pages zenye keywords nyingi.
Google walikuja na model ya 'pagerank' ambayo ilitoa results based on number of links pointed to a particular page (relevancy). Same business, different positioning na wote tunajua matokeo yake.
Nimekupa mfano huo kuonesha kuwa 'google' waliweza kuchepukia kwasababu wao walisema (positioning) tutatoa 'the most relevant results' na wakatoka. Sasa wewe jaribu kujiweka tofauti, labda unaweza kusema, spika zangu zimenakshiwa na ngozi, au zina 'power' kubwa au nyepesi kubebwa na zinaweza tumika popote. Hiyo yote ni positioning. Kwahiyo tafuta kitu katika 'design' yako ambayo ita 'stand out'.