Uturuki na Syria zapigwa tena na Matetemeko ya Kipimo cha Richa 6.4 na 5.8

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,722
45,128
BBC Swahili wamepost muda huu kuwa Uturuki na Syria zimekumbwa tena na tetemeko muda huu

Habari zaidi zinakuja.

559DABAA-22CB-4878-9C96-1DE0DC53C1F6.jpeg

====

Siku 14 tangu kutokea kwa Tetemeko la Ardhi lililoua zaidi ya Watu 47,000, taarifa mpya ni kuwa kumetokea Matetemeko mengine mawili kwenye Miji ya Antakya na Adana na Mpakani mwa Nchi hizo.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa majengo kadhaa yameharibiwa katika miji hiyo ingawa bado hakuna ripoti haraka za madhara kwa Binadamu.

Kwa mujibu wa Mamlaka, ndani ya wiki 2, yamerekodiwa Matetemeko zaidi ya 6,000 baada ya Tetemeko la awali lililosababisha madhara kwenye Nchi za Syria na Uturuki.

Kuhusu Ripoti za Tetemeko la kwanza lililotokea Febuari 6, 2023, soma: LIVE - UPDATE: Tetemeko kubwa lazikumba Uturuki na Syria. Watu zaidi ya 36,257 Wafariki Dunia
 
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.4 katika kipimo cha Richter limepiga eneo la mpaka wa Uturuki na Syria jioni ya Jumatatu, na kusababisha hofu na uharibifu wa majengo katika mji wa Antakya nchini Uturuki wiki mbili baada ya tetemeko baya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo na kusababisha makumi ya maelfu ya watu kupoteza maisha.

Mashahidi wawili waliambia shirika la habari la Reuters, tetemeko kubwa la ardhi na uharibifu zaidi kwa majengo katikati mwa Antakya, ambapo lilikuwa kitovu cha tetemeko.

Ilisikika pia huko Misri na Lebanon, waandishi wa habari wa Reuters wameongeza.

Kituo cha Ulaya cha Seismoloji (EMSC) kilisema tetemeko hilo lilipiga kwa kina kidogo cha kilomita 2 (maili 1.2).

Polisi walishika doria Antakya huku magari ya kubebea wagonjwa yakikimbilia eneo lililokumbwa na tetemeko karibu na katikati mwa jiji.

Watu wawili walizirai, huku wengine wakijaza mitaa kuzunguka mbuga hiyo ya kati wakipiga simu za dharura.
Screenshot_20230220-212552_Facebook.jpg
 
Kumetokea na tetemeko la.ardhi katika maeneo ya mpakani mwa Uturuki na nchi ya Syria ambapo kwa tathimini zimesema kuwa tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa magnitude 6.4

Tukumbuke kabla ya kutokea tetemeko hili leo katika masiku machache kulikuwa na tetemeko kubwa kabisa lililosababisha vifo vya watu zaidi ya 30,000 katika maeneo ya mpakani mwa Syria na Uturuki pia

Wanajiolojia wanasema kumetokea na mpasuko wa ardhi wa zaidi ya kilomita mbili

Nchi ya Uturuki imekuwa ikishambuliwa sana na janga hili la tetemeko tangu mwezi huu wa pili kuingia na huenda ni katika maeneo ya ukanda wa karibu na maeneo hayo yanekuwa wahanga sana wa matukio haya

Moudyswema
Tanzaniascienceyetu
AstronomyKiswahili

FB_IMG_1676920750279.jpg
 
AstronomyKiswahiliView attachment 2524426
Waache kuungeza maumbile ya wanadamu. #Matako #Matiti

Kama Nchi wanatakiwa watubu
 
Back
Top Bottom