Utunzaji wa nywele za asili

Tumia mafuta ya mnyonyo yanapatikana katika maduka ya dawa za asili..kichupa kidogo buku
 
Zi sokote ziwe dread ,pamoja na kupaka mafuta Hayo ya nyonyo
 
Samahani....Umewahi kutimia product za texture my way au una uzoefu na aunt Jackie's tuu??
 
kuna mafuta yanaitwa t444z. haya mafuta ni kiboko! kila mtu ananiuliza kama nimeweka dawa lakini wapi. ukisuka ukapaka chini ya ngozi unaweza kusahau kama hata ulisuka. yaani unafumua unapoona umeichoka style. mimi siyauzi na wala si agent wao lakini nimeyakubali. japo ni expensive kidogo ila the result is worth it. bei yake ni 60,000/=
 
Samahani....Umewahi kutimia product za texture my way au una uzoefu na aunt Jackie's tuu??

Sijawahi kuzitumia kwa kweli na mwezi uliopita nimeziona SH Amon nikatamani kuzinunua(bei rahisi sana aisee) ila nikatoka nje ya duka nikasoma reviews zake mtandaoni(sababu sikuwahi kuzisikia kokote kabla ya siku hiyo) nikaona si nzuri. Wengi wanasema ni nzuri kwa mashombeshombe wenye type 3 hair hadi 4A lakini sisi wa kipilipili kichaa si rafiki kwetu.

Kwa kuongezea, siku hizi nimehamia products za Shea Moisture and i must say zinafanya kazi bora zaidi hasa katika kustyle nywele. Unaweza zijaribu japo bei zake zimechangamka!
 
Sijawahi kutumia t444z ila kutokana na reviews za wengi walioyatumia sikubaliani na sifa utoazo. Unaweza kuwa sahihi though!
 
Nilijaribu kutumia leave in yao harufu yake tuu sio rafiki..ila sikuona kama inatofauti sana na ya aunt Jackie's. ( Labda kwasababu sina kipilipili kichaa
) nilitaka nipate mawazo yako maana nilihisi labda mimi ndo nina kisirani nazo. Shea moisture zimechangamka bei kama cantu??


Mimi ninatumia Bio care products na aunt Jackie's so far it works for me. Ila nime hamu hiyo shea moisture...nitapita weekend nione!
 
Good thing it works for you...ila nywele zinatofautiana at times. It's beautiful ukipata that one product that responds postively...hongera
 
Hongera ndugu...mimi ni kipilipili kile type Z..yani hata nywele ifike mgongoni inajicoil inaonekana kama kiafro kifupi. Kama ziko kama aunt jackies ntajaribu kununua leave in yake nione. Shea moisture ni 45,000 hadi 50,000 tshs ila naona zinastahili sababu hata harufu yake si mchezo na ukitumia kidogo tu inaleta matokeo.
 
Sijawahi kutumia t444z ila kutokana na reviews za wengi walioyatumia sikubaliani na sifa utoazo. Unaweza kuwa sahihi though!

sijui kwa wao wameyatumia vipi. maana hata wao wanakushauri usipake kila siku. yale mafuta hata viuwalaza vinaota nywele. plus ukitaka maximum results wana na products zingine zinazoambatana na hayo mafuta. binafsi mafuta tu yalinipa intended results. shida picha sikupiga ila nywele zillirefuka na kuwa na ubora mzuri kwa muda mchache.
 
Kumbuka si kila product inamkubali kila mtu. So tatizo sidhani kama ni matumizi yao bali product yenyewe.

Binafsi siamini product inaweza kusaidia nywele katika ukuaji au afya bali natumia products katika kustyle na muonekano pekee! Afya ya nywele inaanzia ndani.
 
Ziko kama aunt Jackie's... lakini kama umezoea harufu nzuri nzurii...hio ina harufu ngumu kidogo.
Ooh kama kwa hiyo bei ukitumia kidogo inaleta matokea it worth it...nitajaribu curling jelly yao.

Hahaha kipilipili type Z
 
wewe una kipilipili cha namna gani hicho kisichosikia mafuta
Sina kipilipili ..lakini nywele zangu mafuta ya mgando zimegoma...zinawasha sana. So nimebaki kutumia ya maji tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…