Utunzaji wa nywele za asili

Kwanza inafaa ufahamu ni nini kinacho kusababishia nywele zako kuwa kavu , na kuanza kukatika katika, mara nyingi nywele kuwa kavu inaweza kutokana na sababu mbalimbali. Hapa kuna machache, na kipi unachoweza kufanya ili kurejesha unyevu katika nywele zako kavu:
  1. kutumia vifaa vyenye joto kali kukaushia nywele (hair dry) , vinaweza kusababisha nywele kuwa kavu.
03b44506488e191.jpg


  1. Kuosha nweyele zako mara kwa mara kwa shampoo (Overwashing) bila kuwa na taadhali,
    how-to-shampoo-your-hair3.jpg
  2. kuachia nywele zako kwa muda mrefu kwenye mwanga wa jua,upepo au kutumia maji ya chumvi kwa muda mrefu kuosha nywele zako kunaweza kusababisha ukavu wa nywele pia.
    avoid-exposing-the-hair-to-too-much-sunlight.jpg
  3. kutumia chemicali mara kwa kwa mara husababisha nywele kuwa kavu. (too many chemical Treatment)
    dyinghair.jpg
  4. kutumia brashi mbaya au stairi mbaya ya uchanaji nywele pia husababisha kupoteza unyevunyevu wa nywele na hivyo kufanya nywele kuwa kavu.
    dirtybrush.jpg
NINI CHA KUFANYA KUKINGA NWELE ZAKO ZISIPOTEZE UNYEVUNYEVU

  1. Usitumie shampoo kila mara kuosha nywele zako, kila kitu kizuri ukikitumia kwa wingi kupita kiasi kinakua na madhara hapa jaribu kupangilia angalau siku mbili mbili au zaidi maan hata kutumia shampoo kwa wingi zaidi ina leta madhara, kitaalamu inashauriwa osha nywele zako co-wash angalau mara mbili kwa wiki na mara mbili hadi tatu kwa mwezi kwa kutumia shampoo
  2. Tumia shampoo nzuri inayoendana na nywele Zako, hapa yakupasa utambue una aina gani ya nywele na je, ni shampoo ipi ianakufaa zaidi? usitegemee shampoo za saloon ni vyema hata ukienda saloon ukaenda na shampoo yako mkononi kwani saloon nyingine hata shampoo wanachanganya na maji, usiende tu saloon ukakubali kuoshwa hata kwa shampoo usizozifahamu zingine sio shampoo kabisa
  3. Vaa kofia laini au kitambaa ulalapo, jenga mazoea ya kuvaa kofia laini ya kulalia ili kutunza unyevu nyevu wa nywele zako unapolala bila kuwa na kofia au kitambaa unaweza usababisha nywele kuvurugika na wakati mwingine hupoteza unyevu wake taratibu na huweza kusababisha kuwa na ukavu
    images8.jpg
  4. Punguza mionzi ya kunyooshea nywele zako, siku ukitaka kubadili muonekano au ur hair style ukaamua kuzichoma/kusipasi au kunyoosha nywele zako kwa kutumia moto au umeme…unashauriwa kupunguza temperature au kutumia kinga (mafuta maalum) ambayo inafanya nywele zako zisipate damage wakati ya kuzinyoosha hii itakusaidia kutunza moisture sambamba na kupunguza ukatikaji wa nywele zako
  5. Tumia Moisturizer/Vilainishi Vya Nywele mara kwa mara, Hakikisha unatumia moisturizer kila siku Wengine hawafanyi kila siku. Inategemea na aina za nywele ulizonazo. Wakati wa kuweka moisturizer,hakikisha unapaka kila mahali haswa kwenye ncha za nywele zako(split ends). Mara nyingi huwa tunazisahau zile za juu. Badala yake wengi tunapaka zaidi kwenye ngozi ya kichwa tu. Ndio maana huwa inasisitizwa kuzikata zile split ends kwa sababu huwa zimekauka na dhaifu.
Source : Roy24online
 
Wana Bodi ya Urembo na mitindo
nina nywele Kipilikipili nimetumia mafuta aina ya Oliver oil bila mafanikio.
yaan unachana baada ya masaa mawili zinarudi kuwa Kipilikipili na hazijajaa vizuri nitumie mafuta gani. please wenye uelewa watusaidie najua tupo wengi
wenye shida hiyo.
 
Back
Top Bottom