Washkaji wenye Afro mnafanyaje nywele zinakuwa nyingi kiasi hicho

Joyboy

JF-Expert Member
Sep 16, 2023
1,361
3,404
Habari 🖐 🖐 🖐

Kuna jambo naomba mnishauri, najua kuna watu humu mnajua mawili matatu kuhusu nywele.

Mm nywele zangu kwa sasa zipo level hii(picha hapo chini) baada ya kuacha kunyoa takribani miezi nane(nanyoa tuu pembeni)

images - 2023-11-11T235607.871.jpeg


Sasa mm matanio yangu ni kuwa na nywele nyingi sana(afro) kama mshkaji kweny picha hapo chini.

images - 2023-11-11T235102.649.jpeg


Huwaga natamani sana kuwa na nywele nyingi, nikikutana na mtu ana manywele mengi kama picha hapo juu huwa namwoneaga wivu Sana na namwona kama mtu wa kipekee sana(ni kitu ambacho nakipenda toka utotoni)

Matunzo yangu ya nywele ni ya kawaida, huwa naziosha kila siku na napakaa mafuta, ila nikija kuchana nywele zinakatika kinoma, sometimes huwa naendaga kuchana bafuni kwasababu nikichana room chumba kinajaa manywele, muda mwingine nawaza maybe ndo maana hazikui kwa sababu zinakatika sana.

Kama kuna mtu ana hints zozote za kunipa, please share them.
 
Nywele ninazo sio haba ila tatizo ni ngumu balaa ngumu mno. Nikifuga miezi mitatu au minne nakata tamaa naenda kunyoa maana kuchana inakua kipengele.
 
Kosa kubwa kuosha nywele kila cku, watu wanakaa hata wiki 3 hajaosha nywele,

Kingine inategemea aina ya nywele,, kama kwenu hamna asili ya nywele nyingi utakesha hapa na kipilipili,,
Mzee usitie maji wiki tatu, hiko kitakuwa kichwa kweli?

Mm nimechukua nywele za mama, nina nywele nzuri tuu sema zinakatika.
 
1. Unaoshea nini? Osha na Sulphate free shampoo na usioshe kila siku fanya walau once per week.

2. Nywele kukatika means ni kavu..cha kufanya hakikisha unaipa unyevu nywele yako kila siku kwa kunyunyizia maji ndo uchane kifupi usichane nywele ikiwa kavu.

3. Ukishanyunyizia maji paka mafuta upendayo ungekuwa wa kike ningekupa process ila sasa kwa mwanaume najua huwezi so fuata tu hiyo
 
1. Unaoshea nini? Osha na Sulphate free shampoo na usioshe kila siku fanya walau once per week.
Week days huwa naosha nywele na maji mengi sipaki sabuni then weekends kama jpili hivi ndo naosha na shampoo, hio ya sulphate free nilikuwa siijui, naomba unisaidie jina la hio shampoo tafadhali
3. Ukishanyunyizia maji paka mafuta upendayo ungekuwa wa kike ningekupa process ila sasa kwa mwanaume najua huwezi so fuata tu hiyo
Please nipe hio process
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom