Utumwa wa Mapenzi...(?)

...hivi,

inakuaje mtu anakubali kudhalilika na kunyanyasika kisa
mapenzi.Ni kweli hawezi kula, kulala wala maisha bila huyo mtu?
au ni false hopes kwamba atabadilika tabia?

...Unakuta mwanaume haipiti mwezi anakuja kazini amevimba jicho, halioni sawasawa na damu imevilia. Ukimuuliza anakwambia nimejigonga na mlango.
Kumbe, jana yake alichezea kipondo cha kumtosha toka kwa mkewe,
kosa; 'anajitia jeuri sana!'...

...au, unamkuta mwanamke kakondeana, hana raha yeye ni kilio tu
na misononeko... kisa; Mume wa mtu hamjali, wala hana muda naye, eti muda wote anashinda na Mkewe, anakuja kula uroda tu!

...au mtu ananyimwa unyumba bure bure tuuu, au kila siku ya mungu unanuniwa bure bure! Kama hiyo haitoshi, mtu huyo huyo anayekutenda linapokuja suala la 'chakula cha usiku', anataka ajipakulie ale halafu akimaliza hafuniki wala kupangusa chombo..

shida yote ya nini? Utumwa wa mapenzi ni; udhaifu wa maamuzi/kujiamini, ...au ndio; Mapenzi ya kweli ni kujishusha(?)

Jadili.
Mbu hulali? kweli these few days kuna kitu kinakusumbua sana the way i see it.Kwa hiyo natoa pole in advance.
 
Mapenzi ni makwenzi, huwezijua raha ama karaha yake mpaka ukiwa ndani. Aliyemo ndani ya mapenzi hutamani kutoka wakati aliye nje ya mapenzi anatamani kuingia. Moto ni mtamu ukiuota kwa mbali, lakini ukikaa ndani maumivu makubwa na hata kupoteza uhai utayapata.

Mwinjuma alishasema kuwa zamani akiwa mtoto hakujua nini maana ya mapenzi. Lakini sasa baada ya kuonja keshakuwa tayari kufa ili apate, yeye anaita "Tunda special" na Bambo analiita "Tundi". Padri mmoja alishasema wakati fulani, kwamba kila kitu kitamu ni dhambi. Ama kweli huwezi kuamini ila upatapo madhara ya dhami hiyo. Binadamu anatumia mapenzi kama sehemu ya burudiko la moyo wake, nyongeza ya kuzaa na kuongezeka. Mbwa na wanyama na viumbe wengine hutumia mapenzi kama chambo ya kuzaliana na kuongezeka, wala sio kwa burudani isipokuwa binadamu fulani awe amweafundisha kufanya hivyo.

Kwa kuwa binadamu amekirimiwa uwezo mkubwa zaidi wa utambuzi wa mambo, amepewa kuchagua. Umpendaye wewe sio lazima nami nimpende. Juma anaposema hawezi kuishi bila Mwajuma, kumbe Mwajuma kuishi ni lazima hata bila Juma. Mikorogano hutokea kwa sababu wapendanao wameamua kugeuziana vibao, two-way road imegeuzwa one-way road.

Mapenzi yanayoanzia nje huwa mepasi na hutoweka kirahisi, lakini mapenzi yaliyoanzia ndani ya moyo hudumu. Kumpenda mtu sababu ya maumbile huyeyuka pale maumbile hayo yanapopata dosari. Ni nani awezaye kuunganisha mioyo ya wapendanao isipokuwa Mungu?

Enzi hizo za 47 wazazi wa kiumeni walishawishiana na wazazi wa kikeni ili vijana waoane. Mila na desturi zilipofuatwa ndoa zilidumu. Vijana wa sasa huoana hata kabla wazazi hawajapewa taarifa. Harusi za kale zilikuwa haswa! Mume hamjui mke na mke hamjui mme hadi siku ya siku. Harusi za sasa ni fashion, walishayamaliza siku nyingi hata kabla ya kuvaa neti na suti harusini.

Magomvi kati ya wapenzi hutokana na mageuzi ya uchaguzi wa mweza. Demokrasia ya mapenzi huleta domocrisis katika jamii. Kama mme ni ruksa kupiga mke, kwa nini mke asimpige mume? Kama kuna kutesa kwa zamu, sharti pia kuwepo kuteswa kwa zamu. Kwenye mchezo wa karata, kuna kuliwa na kula. Mchezo wa bao pia, ikla kwako leo kesho itakula kwangu.

Watu wasipomgeukia Mungu na kutii maongozi yake, kamwe hatutajitofautisha kwa uzuri na wanyama. Wivu wa mapenzi hata siafu wanao, ndio maana dume likimtafuna malkia hufa ili amani idumu, kwani hatahodhi madaraka na kuwa Mfalme kwa kuwa tu kawahi kwa malkia. Kama kila mtu anaweza, kwa nini wengine wawepo wasioweza?

Mpende akupendae ili uishi, mpuuze akupuzaye ili furaha yako idumu. Kwani vipi wewe utake kupendwa ilhali wewe hupendi? Na wawezaje kupenda usipendwe? Ukitoa matongotongo machoni utawezaona kwamba mpenzi wako mkuu ni moyo wako mwenyewe. Usipojipenda wewe, wengine katu hawatakupenda.

Leka
 
Mapenzi ni juu ya caring, ukinda extra mile kwenye caring watu watasema mtumwa wa mapenzi, Haya ya kutoana ngeu kwenye mapenzi yapo, na kesho yake utawakuta watu wanacheka na kupigana ma busu wewe uliyewaamulia unaonekana mbaya, huo ndo udhaifu wa kibinadamu. Kuna watu ambao wanajisifia sana kwamba wao wake zao hawawafanyi chochote lkn ukienda kwao, utashangaa jamaa alivyo na adabu kwa mkewe au mmewe. Kuna mwana muziki wa sweet reggae aliimba. Love love so nice, tell me why you hurt so much. Wengine wanasema kila shetwani na Mbuyu wake, ukikamatika huna ujanja ndugu.
 
...hivi,

inakuaje mtu anakubali kudhalilika na kunyanyasika kisa
mapenzi.Ni kweli hawezi kula, kulala wala maisha bila huyo mtu?
au ni false hopes kwamba atabadilika tabia?

...Unakuta mwanaume haipiti mwezi anakuja kazini amevimba jicho, halioni sawasawa na damu imevilia. Ukimuuliza anakwambia nimejigonga na mlango.
Kumbe, jana yake alichezea kipondo cha kumtosha toka kwa mkewe,
kosa; 'anajitia jeuri sana!'...

...au, unamkuta mwanamke kakondeana, hana raha yeye ni kilio tu
na misononeko... kisa; Mume wa mtu hamjali, wala hana muda naye, eti muda wote anashinda na Mkewe, anakuja kula uroda tu!

...au mtu ananyimwa unyumba bure bure tuuu, au kila siku ya mungu unanuniwa bure bure! Kama hiyo haitoshi, mtu huyo huyo anayekutenda linapokuja suala la 'chakula cha usiku', anataka ajipakulie ale halafu akimaliza hafuniki wala kupangusa chombo..

shida yote ya nini? Utumwa wa mapenzi ni; udhaifu wa maamuzi/kujiamini, ...au ndio; Mapenzi ya kweli ni kujishusha(?)

Jadili.

nadhani mapenzi tupendane tu na tucpeane na adhabu, hiyo kushindwa kula kulala cwezi sema ni mapenzi, huyo anahitaji conselling......lol
 
kwa upande wa wanawake wapo wengi wanaoteswa na kukondeshwa na waume wao lakini wenyewe wamo tuu...sio kwa sababu ya kupenda saaana, hapana...ukiongea nao unaweza kugundua kuwa mapenzi yaliisha siku nyiiiingi ila anakuwa hana ubavu wa kuondoka kwa sababu

anategemea mumewe ndio amtunze yeye na wanawe,

hataki wanawe walelewe na mama wa kambo au wa experience mambo ya divorce

anaona umri umekwenda na watoto keshazaa, anaona akiwa divorced ktk umri huo vishawishi vitakuwa vingi na kumpotezea heshima yake, anahofia kupotesa heshima ya kuitwa mke wa mtu etc etc
 
...shukran sana Triplets,

yaani hayo uliyosema ndio 'Utumwa' wenyewe huo ninaomaanisha mimi,...
Ukishaamini huwezi ishi bila yeye ujue umekwisha!

Wazungu wanaita 'Self esteem', yote imemuishia mtu huyo!
Hajiamini tena, ana wasiwasi tuuu, yu tayari kujiua 'akimkosa', ...
Utumwa!

Mkuu, kwani nawe u mmoja wao?
 
Mkuu, kwani nawe u mmoja wao?

...thubutuuuuu!

unacheza wewe,...

...hili Draft mkuu, ...unampa kete ale, ale, ale... akishaingia 'kingi' nabandua zote kumalizia Gemu...kila siku ya Mw' Mungu inabidi kuvumbua formula mpya ya kuwa a step ahead...

...hatumwi, wala hatumikishwi mtu hapa kimapenzi.
 
...Unakuta mwanaume haipiti mwezi anakuja kazini amevimba jicho, halioni sawasawa na damu imevilia.
Ha ha ha ha ha
Mapenzi raha kweli njemba inapewa NAKOZI ya jicho na wife halafu inasingizia mlango. Raha sana. Thats why marriage is not a priority today as far as all the services can be obtained under one roof!!! Mbu yashakukumba nini Strike wangu??? I like ur thread
 
usiogope, ndoa ni bahati nasibu,
Wewe koma kabisa. Ndoa ni bahati nasibu??? Unamaanisha nini?? Aisee dont try this anywhere, anyplace na kama bado hujaoa kama mimi kuwa makini sana na umwombe Mola akuepushe na hiyo bahati nasibu akupe kile unachostahili. Come on, Ndoa bahati nasibu?? LOL!!
 
Ha ha ha ha ha
Mapenzi raha kweli njemba inapewa NAKOZI ya jicho na wife halafu inasingizia mlango. Raha sana. Thats why marriage is not a priority today as far as all the services can be obtained under one roof!!! Mbu yashakukumba nini Strike wangu??? I like ur thread

...eeeh,

...baina ya kuta nne za nyumba kuna mambo si kidogo. Unakutana na mheshimiwa sana tu kumbe nyumbani kituo cha polisi, akimjibu maza hausi tu kofi!

...Sikubahatika kumpata mwanamke wa namna hiyo,
nilipokuwa natafuta nilikuwa makini kwenye kuchagua, LOL!
 
Wewe koma kabisa. Ndoa ni bahati nasibu??? Unamaanisha nini?? Aisee dont try this anywhere, anyplace na kama bado hujaoa kama mimi kuwa makini sana na umwombe Mola akuepushe na hiyo bahati nasibu akupe kile unachostahili. Come on, Ndoa bahati nasibu?? LOL!!
ni kweli nilisema ndoa ni bahati nasibu na nadiriki kurejea tena kwa kujiamini kwamba ndoa ni bahati nasibu (either win or loose) , labda ungeliangalia niliemnukuu na ukaichukua sentensi yangu nzima ungelifahamu nimekusudia nini. tatizo limekuja pale ulipochukua kipande cha sentensi.

ndoa ni bahati nasibu kwani unaweza ukategemea utakutana na mazuri ndani ya ndoa lakini ukakutana na mabaya na unaweza ukategemea mabaya lakini ukakutana na mazuri. pia wenza kabla kuowana unaweza ukawaona wana tabia nzuri lakini ndani ya ndoa wakawa visirani na wengine wanakuwa visirani kabla ndoa lakini ndoa inawatuliza akili. hivyo ndoa inabaki kuwa bahati nasibu . after all ukisoma maelezo yangu ulionukuu nimeandika kwamba,kuchukua tahadhari ni muhimu. lakini pia jiandae na lolote utakalokabiliana nalo katika ndoa , aidha likiendana na matarajio yako au vyenginevyo. na ndio maana namfananisha mwandoa na jeshi mpiganaji(soldier) ,kwani ndoa sio lelemama kwamba kila mtu anahimili vishindo vyake.

quiet.
 
Back
Top Bottom