Utumwa wa Mapenzi...(?) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utumwa wa Mapenzi...(?)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbu, Oct 27, 2009.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hivi,

  inakuaje mtu anakubali kudhalilika na kunyanyasika kisa
  mapenzi.Ni kweli hawezi kula, kulala wala maisha bila huyo mtu?
  au ni false hopes kwamba atabadilika tabia?

  ...Unakuta mwanaume haipiti mwezi anakuja kazini amevimba jicho, halioni sawasawa na damu imevilia. Ukimuuliza anakwambia nimejigonga na mlango.
  Kumbe, jana yake alichezea kipondo cha kumtosha toka kwa mkewe,
  kosa; 'anajitia jeuri sana!'...

  ...au, unamkuta mwanamke kakondeana, hana raha yeye ni kilio tu
  na misononeko... kisa; Mume wa mtu hamjali, wala hana muda naye, eti muda wote anashinda na Mkewe, anakuja kula uroda tu!

  ...au mtu ananyimwa unyumba bure bure tuuu, au kila siku ya mungu unanuniwa bure bure! Kama hiyo haitoshi, mtu huyo huyo anayekutenda linapokuja suala la 'chakula cha usiku', anataka ajipakulie ale halafu akimaliza hafuniki wala kupangusa chombo..

  shida yote ya nini? Utumwa wa mapenzi ni; udhaifu wa maamuzi/kujiamini, ...au ndio; Mapenzi ya kweli ni kujishusha(?)

  Jadili.
   
 2. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Kama kwenye mapenzi ya ndoa kuna utumwa wa jinsi hiyo mie hiyo ndoa itakuja kunishinda, sitaki utumwa kabisaaaaaa, na wala sitaki kumfanya mwenzangu aje kuwa mtumwa wangu.

  Ninachotaka mie kila mtu ashiriki part yake kama mume aelewe wajibu wake, na mie kama mke nielewe wajibu wangu.Sio kufanyiana utumwa tu, na wakati raha ya ndoa ni kuridhishana na kila mtu amfurahie mwenzake.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  hujambo pretty?
  Wanaosema ndoa zitakuja washinda
  wengi wao huwa wanakubali yote.
  Usiape kabisa kuhusu ndoa.
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ngoja waamke, au sijui mgao wa TANESCO upite ...watakwambia hujawahi kupenda wewe...!

   
 5. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Mie mzima tu,
  Hizi ndoa za siku hizi lazima mwanamke uweke msimamo wako kabisaaa, ili mwanaume ajue kabisa ni nini unapenda na nini hupendi. Hivyo mie utumwaaaaa hata siutaki.
   
 6. Q

  Quiet Member

  #6
  Oct 27, 2009
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kama kuna kitu kibaya alichoumbiwa mwanadamu basi ni "hisia za mapenzi" ni bora huo utumwa uliozungumza kuliko binadamu kutawaliwa na hisia za mapenzi. wengi ya wale wanaokubali kunyanyasika katika mapenzi ni wale waathirika wa maradhi haya, ambao wanaamini kwamba kwa kutumia "huruma" basi wanaweza wakambadilisha simba kuwa kondoo. maradhi haya yanamfanya binadamu kuwa king'ang'anizi mpaka kufikia kupoteza heshima yake. nakubaliana na wewe wengi walioathirika na maradhi haya huwa ni wadhaifu wa maamuzi na kujiamini. na mara nyingi huwa wanampa mapenzi yao mtu asiestahiki kupewa.

  Mr. quiet
   
 7. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280

  Mbu bana,,!

  hao wa ki ivyo ujue wameingia kwenye mahusiano ambayo wazi hayakumaanishwa kuwa yao,

  Mfano, mtu anakonda kisa mume wa mtu, si atafute wake? Huyo kajitia kitanzi mwenyewe...sio wa kumhurumia,

  Na mtu anapigwa..awe mke au mume..mapenzi ya kupigana siku hizi yamepitwa na wakati.....mwanamke anapigwa kwa upande wa kanga bana.....:rolleyes:

  Kimsingi, utumwa wa mapenzi ni mtu kujitakia kuwa mtumwa.....mapenzi hayadai kupewa zaidi, huwa yanapenda kutoa zaidi!

  Mapenzi yaso na chembe ya utumwa hayajui kupigana, kutukana isipokuwa 'kutukana', hayajui kupungua!

  Mapenzi ya kweli hayajui kukonda, yanajua kunawiri tu, moyoni na mwilini!
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  There is nothing wrong with being a fool in love.
   
 9. Q

  Quiet Member

  #9
  Oct 27, 2009
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  usiogope, ndoa ni bahati nasibu, muhimu ni kujitahidi kuchukua tahadhari kwa kila linalohitaji tahadhari. baadhi ya wakati ndoa huwa ni pepo (paradise) ya dunia.
   
 10. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Hivyo ukimpenda mtu sana ndio ukubali kuwa mtumwa? Ndio ile ya kusema love is blind au?
   
 11. M

  Malila JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Utumwa ukikufika unaweza usijijue kama ni mtumwa,ila jamaa na majirani ndo wanaweza kukuona kama ni mtumwa wa mwenzio.
   
 12. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mapenzi ni kitu ingine jamani, anayependwa hujisikia faraja lakini asiyependwa kila siku ni majonzi na yupo radhi ajidhalilishe kwa huyo asiyemjali, ndio kupenda huko jamani
   
 13. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mapenzi! mapenzi!Mapenzi! Wasanii wa muziki wanaimba mapenzi,waigizaji nao mapenzi,wabibi kizee na vibabu navyo mapenzi.Hata watoto na wanafunzi nao mapenzi.
  Kwani mapenzi ni nini hasa?
   
 14. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mimi sioni kama ni utumwa.

  Ndio mapenzi yenyewe hayo!
   
 15. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Pole sana .... Katika mapenzi niliyopitia hakuna hata moja ambalo umeligusia! Kama haya yanatendeka basi ni kwa wachache hasa kwa zama hizi! Mie naona kila w/end watu wanafurahi na wenzi wao mpaka basi... Sasa hayo ya kutunguana jicho duh...Hapana... Pole sana.... Pole sana... Pole sana.....
   
 16. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,056
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Hahahaha! ZD bana. Eti kwani mapenzi ni nini? Lol! Unataka kutoka off point ujue.
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  mapenzi ni kupendana jamani si kutesana mmekutana wazima wa afya kwa nini kuumizana na kutiana majeraha yasio na maana
  Kama penzi limeisha si bora kupeana break ili kila mtu atafakari juu ya maisha hayo ya ndoa na kutoa maamuzi kama kuendelea kupo au kila mmoja aanza na 50 zake ..?
   
 18. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Sio off point dia,unadhani nitapewa ziii?.Kama hata hayo mapenzi huyajui utajuaje kama ni mtumwa?Lazima ujue mapenzi ni nini kwa sababu unaweza kufikiri una mapenzi kumbe ndio huo utumwa.mimi kweli sijui Naomba niambie wewe mapenzi ni nini? nayasikia kama njaa au?
   
 19. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,056
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Naona unanitega nitoke out of perimeter. Ni PM nikuelezee kwa kina. Ila kwa kifupi mapenzi ni mhemuko na mtimizo wa uhemkaji katika kiwango kinachotakiwa cha kuhemka. Uhemko huo unahusisha kupenda, kujali, kuheshimu na kutimiza yote yanayohusu hisia za watu wawili waliokubaliana kuhemshana.
   
 20. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Thanks,nitaku-PM ili niulize maswali mengine zaidi.
   
Loading...