WAAFRIKA kiujumla kinachotudumaza ni UTUMWA ambao bado umebaki kwenye fikra zetu kuanzia nyanja za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Na kama taifa la Tanganyika tunahitaji ukombozi wa kifikra dhidi ya nini mahitaji yetu ya msingi, malengo yetu, na miongozo yetu kuyafikia hayo mahitaji ili tuwe taifa.
Tujipime mifumo yetu ya kiutawala, kiuzalishaji, kuishi kama jamii inatufaa kufikia tunayoyahitaji. Mana wasomi wengi Leo wanaimba demkokrasia lakini ukiwauliza ya namna gani hawana jibu la kimahitaji. Vyama vya siasa vingi visivyokuwa na mahitaji ya msingi vya nini?
Kumfundisha mtoto wa shule ya msingi kompyuta na mifumo yake pasipo kuiona hiyo kompyuta na kufanya Kwa vitendo inasaidia nini?
Kuendeleza kutumia pesa za nchi kuzalisha walimu wa masomo ya kijamii na Sanaa ikiwa waliopo mtaani hawajaajiriwa na Kuna uwezekano wakazeeka hawajaajiriwa hatuoni ni matumizi mabovu ya rasilimali muda na watu?
Lakini hivi vyote mizizi ni UTUMWA ambao bado unatawala fikra zetu, tunaiga mifumo ya maisha kutoka waliotutawala katika nyanja zote za maisha alafu Leo hii kina Heche, Lema, Nay wa Mitego na wengineo wanalalamikia ujinga tulionao vijana.
Chanzo ni UTUMWA ambao kiuhalisia bado unaishi TANGANYIKA