Utumwa mpya ndani ya Kanisa


'God' is a human creation and not otherwise..
Tafakari hapo mkuu.. usirukie kuponda watu wakati wewe mwenyewe ni layman katika dhana nzima ya God and Religion..
 
Makanisa yaliojawa na shuhuda.

Huwa sielewi nini maana ya zile shuhuda.

Mtu anatolewa pepo anawekewa mic ili wasikie pepo linaongea.

Siku nzima unashinda kanisani, huna kazi za kufanya.

Upumbavu sana.
Nakubaliana na mtoa mada kwa asilimia zote na pia waliochangia humu wengi sana nakubaliana nao sana.
Labda nianze na hii ya kuwekea watolewa pepo mic ili wasikike.
Unapoinga kwenye mifumo ya kidunia ya kutaka/kutamani faida,LAZIMA utajikuta unapitia barabara zile zile(japo hata pembeni uchochoroni,ila sambamba na hizo njia) ambazo kwa kiasi kikubwa ndizo zaaminika kuwa zaleta hiyo/hizo faida kwa haraka ama uhakika zaidi.Kwa yeyote mtafuta pesa ama faida,kujitangaza hakutakwepeka. Na tangazo litazingatia 'tukio' lenye kuvutia zaidi ama mojawapo ya namna hiyo.
Naamini wapo waongoza kondoo/waumini ambao si feki na hata hutangaza shuhuda kwa nia njema kabisa za kuongeza imani za wasikilizaji (kwani shida nyingi za wanadamu zafanana tu,tofauti ni chache) ili nao waende wakapate uponyaji ama utatuzi wa kiroho.Ila,kama jinsi shetani alivyovamia na kuiga sadaka ya kumwaga damu,leo tunao masanii wa nyumba za ibada wanaotenda haya kwa nia ya kutangaza ili wawapate wahanga(wateja) wengi zaidi.Lengo likiwa ni hela za waumini.Hawa hawana haya,huruma wala kujali.Sera zao ni 'njoo na shida yako,ila leta/uje na pesa tu(ama tuma pesa kwa njia za simu)'.
Hawa utawasikia hata wao wenyewe wakivimba vichwa wasikiapo shuhuda zikutolewa maana wanajua marketing efforts zao likely zitalipa na kuwavuta wengi zaidi.
Huwa nasikiliza mahubiri mbalimbali.Kwa kweli,hata kwa msomaji Biblia wa kawaida utagudua upotoshaji wa ajabu sana wakati mwingine.Neno linaongezewa mbwembwe kibao za kibinadamu ili kuvutia watu.Naamini,neno lenyewe tu likisomwa,lina maajabu na nguvu kwa msomaji.Halihitaji kuongezewa mbwembwe na kihisia za kibinadamu,chumvi wala uongo kamwe.
Hata hao wanaokwenda hizo nyumba za ibada,wengine si ajabu sio kuwa ni wajinga sana wa neno kivile.Ila shida ikikaba,kwa baadhi akili hufa ganzi na kutafuta suluhisho kwa namna yoyote ile,hata kujipeleka kwa wasanii wa madhabahuni kutafuta ama suluhu,ama wachawi wa shida zao au sababu/vyanzo.Na hawa wasimamia shoo,hawakosi sababu na wanajua watu lazima waje tu.na si ajabu huomba shida zisiishe.
Hawa hutumia shida za wengine kuganga shida zao na hasa wanajua watu tunapenda sana njia za mikato,kutafuta wachawi na kutamani miujiza bila ustahiki wa kuipata hiyo miujiza kwa namna sahihi,rahisi na hata mingi mingine iliyo ndani ya uwezo wetu wenyewe.
Sikumbuki kusoma mahala Yesu kudai sadaka ama kuagiza mitume wake kudai sadaka.Ila nakumbuka akielekeza wakienda mahala,watafute kwa wenyeji panapowafaa waingie kwa ,watapata huduma humo;kitu kama hicho.
Sasa hivi,hawa wasanii hawatendi haya.Labda wakati haufanani.Ila,hata wakienda mahala,si ajabu watalala mahoteli ya kifahari zaidi kuzidi hata kiwango cha muumini yeyote wanaowahubiria.Wakitoka humo,wataweka msisitizo mkubwa wa sadaka na mambo yao yanaenda safi tu.Na hapa ndipo ujanja na werevu wa kuweka mashiko kwenye imani ili kuvuta zaidi watu na kuongeza zaidi faida.Mambo ya imani ili kuyawekea faida,yanawekewa 'vitu'.Navyo ni chumvi,maji n.k. maana nadhani walishajua,ama watu walishazoea sana au vipi,kuweka tu mikono,watu hawatoi hela ya kutosha.Mpaka umkabidhi kitu,ndipo pesa ama hutoka zaidi ama ni rahisi 'kuidai' kirahisi zaidi.Upande wangu,naamini wapo wanaofanya haya kwa nia njema na uhalisia,ila wapigaji nao wamehamia humo kibao!!!
Jana tu,kuna jamaa akampigia mmojawapo wa hawa watu kwa shida yake.Akaishia kuagizwa atume 150,000/= haraka sana ili apate ukombozi.Tena ikiambatana na utisho wa ajabu kusisitiza kuhusu chanzo cha hiyo shida.Labda ili hiyo pesa itumwe haraka zaidi.Agizo lilitokea eneo la Kinondoni.Hii ni ajabu,upuuzi na kioja cha hali ya juu kabisa.Hakika manabii wa uongo wamejaa na tunao wengi mno.
Kuna siku nilisikia rais wa Rwanda (ama uongozi wa huko) waliamua kuyapunguza makanisa feki sababu hakuelewa sababu ya uwepo wa makanisa mengi mno huku mengine hata hayaeleweki.Wakati ule,nilikubaliana naye kwa theluthi mbili,ila theluthi moja nikasita kuwa labda kuna walakini.Hatimae nilikuja kuamini,hakika YUPO SAHIHI na hili twalihitaji sana hapa Tz.Tuna wasanii wasio hata na haya,huruma wala kusita na hawana hata huo woga wa Mungu.
Natamani siku moja nchi hii iwe na utaratibu wa kuchuja hizi nyumba za ibada.Najua si rahisi hasa ukizingatia serikali haiingilii mambo ya imani,na labda haitakuja kutokea.Ila,kwa urahisi na wepesi wa kufikia waumini ulivyo mkubwa sasa,hakuna haja ya utitiri wa makanisa ambayo asilimia kubwa sana ni shoo za kuvuta na kupiga hela tu kwa faida ya wasimamia hizi shoo, tena toka kwa walio na hali ya chini,wahitaji na wenye shida.Naamini na kukubali kuwa,sadaka itolewe na kila mmoja.Ila,hawa wengine wanautumia huu mwanya kinyama sana tena bila haya wala huruma.
Kwa kuwa pia nakumbuka mahala kwenye Biblia panasema,ile siku Yesu atawakataa hata wale watakaojitetea kuponya kwa jina lake,hii inaashiria wazi kuwa,kuponya,pamoja na sarakasi za namna hiyo,sio kigezo cha usahihi wa huyo atendaye hayo.
Ila,heshima kwa viongozi wote wa dini (zote) ambao wanazingatia misingi ya imani zao kwa kuweka maslahi ya dini/imani zao na kuongoza na kuelekeza waumini sawa sawa na matakwa ya mapenzi ya Mungu.Hawa waliobaki wanaoenda nje ya mstari,Mungu anawaona.
 
Malisa umenena vyema.
Walokole wengi, wacha hao wanai jiita manabii na mitume, hata makanisa ya TAG, wachungaji wamejigeuza miungu mtu.
Kanisa moja lipo Dar maeneo ya upanga, mchungaji wake ANALAZIMISHWA AIMBIWE "YOU RAISE ME UP" ,sasa mtu unajiuliza, unaimbiwa wewe ama Mungu!
 
naichukia ile system ya kutoa sadaka kwa mstari sijui ni nani aliileta yaani utakuta kwa mfano huna sadaka kabisa afu imefika zamu ya kiti chenu kwenda kutoa sadaka ..yaani kama utabaki inakuwa aibu kuwa wenzio wamesimama afu ww umebaki...i hate this
 
Amen
 


Kwanza unamuongelea Mungu gani?

Ili tujadili Mungu inabidi tujadili tabia zake.

Wewe unapotaja "Mungu" unamtaja Mungu gani? Wa Biblia? Wa Quran? Tabia zake zipi? Jina lake anaitwa nani?

Unaweza kuthibitisha yupo na si hadithi za watu tu?
 
Mpumbavu husema moyoni mwake hakuna Mungu
Mjanja kajiwekea mstari wa "Mpumbavu kasema moyoni mwake hakuna Mungu" katika kitabu ili wapumbavu wanaoogopa kuitwa wapumbavu kuliko upumbavu wenyewe wazidi kupumbazwa.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo? Thibitisha.
 
Mtoa mada na muwasilisha mada mmesomeka vema kabisa na ametoa mawazo ya kweli katika ulimwengu wa leo. ambae hajaelewa ni mlokole mfia dini
 
Kwanza unamuongelea Mungu gani?

Ili tujadili Mungu inabidi tujadili tabia zake.

Wewe unapotaja "Mungu" unamtaja Mungu gani? Wa Biblia? Wa Quran? Tabia zake zipi? Jina lake anaitwa nani?

Unaweza kuthibitisha yupo na si hadithi za watu tu?
Unachekesha kwani wewe unavyotaja au kubisha unabisha juu kitu gani, au kama bado hujajua ni Mungu yupi unapata wapi sababu za hoja zako..?

Kingine tambua dhana ya Mungu ni moja tu duniani na Mbinguni kote ([emoji23][emoji23][emoji23]) najua hapo kichwa kimeuma tena kusikia nataja MBINGU iko hivi jaribu kufikirisha akili yako walau kidogo...

Mfano ebu jaribu kuwaza binadamu/mtu ukiyekaa naye hapo afu sumbua akili yako au weka mitambo ya sayansi na technology unadhani ni bora duniani ukimudu kujua na kutwambia kuwa huyo mtu anawaza nini basi utaanza kulewa dhana ya Mungu Roho.

Ndugu yangu Kiranga siyo kila kitu kinahalisika ili kiwepo, hoja zako huwa ni dhaifu mno kumfikiria Mungu awe mtenda MEMA TUU, na wakati hayo MEMA yenyewe yanategemea ubinadam, mtu na mtu siyo kila chema kwako kwangu ni chema kumbuka Mungu hana tabia za kibinadam/humanity properties.

Mara nyingi unakujaga na hoja ya KIFO na MABARAHA/MAAFA ukisema angekuwepo angeyazuia yasitokee labda una uhakika gani kwa Mungu kama kifo anakiona ni adhabu au kitu kibaya..?

AU ni kwa vipi unaweza kunishawishi niseme mabaraha yanatokea nje ya matakwa ya Mungu au ndani ya mapenzi yake na hayategemeani na binadamu mwenyewe..?

Narudia MUNGU yupo katikati ya UBAYA na WEMA/Mabaya na Mema sasa ubaya wa kitu utatokana na namna mtu atakavyotenda ukizingatia principles rule ni kuwa usiifanyie mtu usichokipenda na ndiyo kilimo cha kitu kibaya au kizuri kwa Mungu.

Ndugu bado sana, level zako kumfikiria Mungu hutaelewa maana Mengine hayategemei elimu gani uliyonayo kumjua Mungu..!

Kitu kimoja nikukumbushe iko hivi uwezo wa akili uliozaliwa nao utabakia kuwa mkubwa maisha yako yote kuliko ujuzi na maarifa utakayojifunza kipindi cha uhai wako hapa duniani.
 
'God' is a human creation and not otherwise..
Tafakari hapo mkuu.. usirukie kuponda watu wakati wewe mwenyewe ni layman katika dhana nzima ya God and Religion..
Unachekesha mno... [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Duniani wajinga ni wengi sana kuliko wenye akili.

Mawatu yanapenda miujiza miujiza tu na njia mkato kupata mafanikio na ni Wabishi sana hata hawataki kuelewa.

Beyonce naye kacheza uchi weeee...afu 2016 kazindua dini yake na biblia yake mawatu yamemfata na yamejazana tele.

Fanyeni kazi jamani mazuri yako mbele kwa mbele na Mungu hana upendeleo wowote.
 
UTUMWA ndani ya MADHEHEBU
 
Umeshawahi kufanya uchunguzi juu ya hayo masuala au ndiyo walewale wavivu hata wa kufikiri na kuishia kutoa majibu mepesi yasihotaji kuchosha akili?hapa sio suala la watu kupoteza muda kwenye hayo mambo bali uhalisia wa hayo mambo.
 
Thibitisha Mungu yupo.
Thibitisha uchawi upo.
Kwa watu wavivu wa kufikiri kama nyie hicho ndio kichaka chenu cha kujifichia,mtu hujawahi hata kushuhudia tukio lenye kuhusishwa na uchawi na ukalichunguza ili upate ukweli ila mnakuja humu kusema tu hakuna uchawi mara hakuna Mungu,jiulize una hoja gani ya msingi inayokufanya upinge uchawi zaidi ya msimamo tu usio na nguzo yeyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…