Utumwa mpya ndani ya Kanisa

Umemaliza hakuna cha kuongezea hapo "asante sana"
 
Dah! namuonea huruma dada yangu fb kwenye page ya suguye huwa ana comment amen napokea lakin haupiti mwezi lazima anipige kidundo sijui huwa wanapokea nini.
 
Hii ni thread bora ya mwaka humu jf. Mwanasayansi Galileo alisema dunia inazunguka dunia, kanisa lilimnyonga , Leo ukweli uko wapi
Tusiogope kutia akili na kutegemea miujiza ya maombi. Dunia inabadilishwa na sayansi so imani za dini , ila dini INA umuhimu wake kwa Amani ya nchi , lakini utajiri ni matunda ya Kazi. Hata ushinde na kulala nyumba ya ibada hutapndpa umaskini wako.
 
Ukishaelewa Mungu hayupo, na habari za kuwepo kwake ni hadithi za watu tu, haya mengine hayawezi kukusumbua sana.
Huo nao ni uvivu wa kufikiri,mmekuwa watu mnaotoa majibu mepesi tu "Hakuna Mungu...hakuna uchawi". Hamjisumbui kufikiri wala kufanya uchunguzi nyie ni kusema tu hakuna uchawi mara hakuna Mungu. Unakuta mtu yupo afrika anakwambia hakuna uchawi lakini hajawahi kufanya kauchunguzi chochote kujua ukweli hicho kinachoitwa uchawi zaidi ya kuwaambia watu kwenye mitandao wamroge,yani hajawahi hata na mtu wa karibu ambaye alikuwa na tatizo lenye kuhusishwa na uchawi na kulifuatilia hadi mwisho na kugundua kuwa uchawi ni kitu kisicho cna uhalisia.

Yani zile story za utapeli kwenye masuala ya kiimani ndio mnazipenda maana zinawapa faraja na ndiyo maana hapo umesema ukijua hakuna Mungu et haya mambo hayawezi kukusumbua.
 
Hahaaa.. mkuu unachekesha kwa sababu unaonesha ushabiki wa kanisa katoliki bila kufahamu mambo mazito.. kanisa lilijengwa kwa jasho na damu za watu kupitia zaka na sadaka. Kuna vichaka lazima vifukunyuliwe ili ukweli ujulikane.. kuna story fake kama hiyo ya Rwanda, tena maarufu nayo ni ya wale mabinti watatu wa Fatima kutokewa na Maria.. miaka ya 1940s.. hiyo story ilikuwa fake na wengi walidanganyika.. walikuwa brainwashed.. ni vile tu watu wavivu kufanya analyses.. Kanisa la Roma nalo lina madudu kibao, japo ya kwao ni ya kistaarabu
 
Thibitisha Mungu yupo.

Thibitisha uchawi upo.
 
Uchawi na dini ni dhana tu.. inategemea unaelewaje haya mambo.. watu wasiyo na reasoning, kwa sababu mbali mbali kama kutokwenda shule, au kwenda shule ila wakapewa elimu ya hovyo ndo hupoteza muda kwenye mambo haya ya mythology.. you could be one, jisearch
 
Hii tungeangalia kwa wawakilishi wa wanainchi.wabunge,marais,na mawaziri nadhani tunvechoka.Hao wachungaji na wanasiasa ndo wanakula maisha huku Afrika.
 
Makala kama hizi zimetolewa sana kwa minajili ya kuzindua akili za wajinga wanaoliwa kwenye mchezo wa karata3 za kekundu na keusi ufanywao na makanisa kutapelia.

Mliisha sema sana, tena saazingine kwa kutaja majina ya hao mumiani wa jina la yesu, lakini wapi!

Kusikia kwa kenge hadi atoke damu masikioni.
Na ndiyo maana Mjerumani alikuwa akitumia mboko kuzindua akili za wapumbafu.

Nchini Rwanda huo mchezo waliisha ushitukia na kuweka masharti magumu ya kusajili haya makanisa ya kilokole na walipotaka kutunisha misuli hao mumiani kwa kutumia maneno waliyozowea kuyaita ya kiroho, walipambana na mkono wa dola na wakashika adabu zao.

Hapa kwetu Tz sijui kwa nini hizi NGOs hazimulikwa kwa kurunzi lenye mwanga mkali wa spotlight?
 
Ukishaelewa Mungu hayupo, na habari za kuwepo kwake ni hadithi za watu tu, haya mengine hayawezi kukusumbua sana.
Teh heheheee! Kutwa kucha unahangaika na uwepo wa Mungu, kila nyuzi inayotaja Mungu upo halafu unawadanganya eti hayakusumbui. Unasumbukaje? Kwa sababu moyoni mwako ukweli unaujua na ndio unaokusumbua!
 
Kuna yule aliyeongea na Mungu kwenye simu, mtafute YouTube.. Huyo naye kiboko, utacheka mpaka ushangae... Hahahaa anauliza hapo ni mbinguni, "is it Heaven?" "yes papa god"
 
Teh heheheee! Kutwa kucha unahangaika na uwepo wa Mungu, kila nyuzi inayotaja Mungu upo halafu unawadanganya eti hayakusumbui. Unasumbukaje? Kwa sababu moyoni mwako ukweli unaujua na ndio unaokusumbua!
Hujathibitisha Mungu yupo, sitaki maneno mengi.

Thibitisha Mungu yupo.

Mimi sijanzisha uzi huu, hivyo huwezi kusema kwamba nahangaika na uwepo wa Mungu.

Mimi najibu uzi ulioanzishwa na watu wengine tu.

Kama mwanajamii bora wa Jamiiforums anavyotakiwa kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…