Utumishi wa umma unakoma mgombea anapopitishwa na NEC, kiburi cha akina Kafulila na wenzake ni kutambua sheria inawalinda

T2020

Senior Member
Jul 15, 2020
131
328
Anachofanya JPM kutengua nafasi zao viongozi wanaoomba ridhaa ya CCM kugombea ubunge ni kuongeza ghalama kwa Serikali.

Atalazimika kuwalipa mishahara ya vyeo vya uDAS, uDED,uRAS na Ukatibu Mkuu viongozi anaowatengua vyeo vyao wale wote ambao hawatapitishwa na CCM kupeperusha bendera ya CCM na kupitishwa na NEC kupambana na vyama vya upinzani.

Wale watakaopitishwa na CCM ajira yao itakoma hata wale watumishi wengine wa umma wasio wateule wa Rais kwa kulipwa chao. Ubishi wa kutotii kauli yake kuwa hawalidhiki na vyeo alivyowapa upo hapo. Nadhani hakujua kama kauli yake ya kuwatisha aliitoa kimakosa na washauri wake kwa kumuogopa hawakumtahadharisha.

Kama kanuni kuu za utumishi wa umma zimebadilika nishahihishwe. Bado naona Kafulira na wenzake walioingizwa kwenye utumishi wa umma bila usaili bado wako salama.

Akilazimisha kuwanyima mishahara yao wataenda mahakama za kazi na watamshinda. Hata maDED anaowatumbua bado wananufaika na mishahara minono ya uDED hadi watakapostaafu.
 
Ni kweli huyu mtu anaharaka sana

Sijui kwanini? Sijui kwanini hatulii afanye uteuzi wa moja kwa moja, yaani ndani ya siku moja Kuna taarifa 2 za uteuzi. Aibu sana.

Ni kweli wale watumishi wa kudumu

DEDs, DAS, makatibu wakuu na maras wataendelea kulipwa mishahara yao na watapangiwa majukumu mengine.
 
Hawa wakianguka huko ndiyo imekula kwao,.awamu hii sheria, Katiba, kanuni vyote weka pembeni amri moja tu.
Utawala wa sheria ni muhimu kiongozi. Kiburi cha kuvunja sheria za nchi na kanuni zake zitakuja kum-cost baadaye hawezi kuwa Rais milele, Katiba siyo biblia/msaaafu mzee. Wabunge hawahawa watakuja kuweka viraka vya kumumaliza. Ndiyo maana waliomtangulia wako salama waliheshimu katiba.
 
Huyo mtu ana kisasi sana ,yeye aangalii gharama au vipi yeye ni maamuzi ya kibabe tu ili kutisha wengine!! Ndio maana Serikali yake malipo ya mishahara ni makubwa sana kuliko awamu ya jk na ajira hakuna ,nyongeza hakuna ,warsha ,makongamano yote kafuta lkn gharama juu juu.
 
Hivi mtu anaweza kupinga kutenguliwa uteuzi wake kwa mujibu wa hiyo sheria?
 
Wapo wengi tu aliowaacha uteuzi ule wa 2016 mpaka leo wanakula mishahara yao, huku wakifanya majukumu mengine
Hii iko wazi ni kwamba mtumishi wa umma akiteuliwa na Rais kushika madaraka ya kiuteuzi Kama RC, DED,DG,DAS, RAS, DC na n.k Kama mshahara wake ni mdogo basi utapanda kuendana na cheo kipya alichoteuliwa kukitumikia na hata akitenguliwa atarudi kwenye majukumu yake ya mwanzo na mshahara utabaki palepale hautapunguzwa kulingana na kanuni na sheria za utumishi.

Hapa kuna wale wenye mishahara mikubwa na wanateuliwa kuwa Ma-RC ambapo mshahara wao unakuwa mkubwa kushinda cheo Cha URC walichoteuliwa kukitumikia, mishahara yao itabaki hivohivo haitapunguzwa pia, Hawa watakachofaidi ni madaraka na Yale malupulupu ya ukuu wa mkoa na hata wakitenguliwa wanarudi pia kwenye majukumu yao ya awali na mishahara yao Kama ilivyo.

Kwa ambao walio nje ya utumishi wa umma wanapoteuliwa kushika hizi nyazifa za URC wakitenguliwa wanakoma kuwa watumishi wa umma maana hawakuwa watumishi wa umma kabla ya uteuzi, hivyo wanakuwa hawana kazi rasmi na hawatalipwa mishahara ni sawa Kama wamefukuzwa kazi na waajiri wao au wameacha wenyewe
 
Hakuna cha kuona Bwashee

Yaani JPM with the grip he has kwenye taasis zote za serikali alipe mshahara wa DED aliyemtumbua mpaka astaafu???

Thubutuuu
Kwani ni Magufuli au serikali inalipa mishahara? Kanuni za serikali ni kuwa ukiachishwa madaraka utaendelea kupata mshahara wako ule ule hadi ustaafu kwa mujibu wa sheria. Na hii siyo hisani ya Magufuli.
 
Ndio tatizo la One Man Show!!!
Marais waliomtangulia waliishia kuteua nafasi za kisiasa kama u-DC na u-RC yeye akaenda mbali zaidi mpaka nafasi za utumishi wa umma ambazo watu walipandishwa kwa kushindanisha watumishi wa umma. Watu aina ya kufurila asingeingia utumishi wa umma kwa namna ile. Watu wanaojua sheria za utumishi wa umma kama akina Ndumbaro wakamwacha tu, kwa kumwambia yupo sawa. Nadhani ameanza kujifunza kitu naona ma-DED anateua wakuu wa idara kwenye halmashauri siyo makada tena wa CCM. Makada kwa sasa wanaishia kuteuliwa kuwa ma-DC au ma-RC.
 
Back
Top Bottom